Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
JK achochea moto
*Wasomi, wanasiasa wasema naye amegeuka kuwa mlalamikaji
*Wadai angeeleza serikali itakavyokabili genge la wahuni
Tumaini Makene na Grace Michael
HOTUBA ya Rais Jakaya Kikwete ya kuadhimisha miaka 34 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi imechochea moto na
mijadala nchini, huku kauli kuwa hakuna uharaka wa kuilipa Kampuni ya Dowans sh. bilioni 94 ikiibua maswali zaidi kuliko majibu.
Wasomi na wasiasa waliozungumza na Majira jana walisema Rais Kikwete ameungana na wananchi wa kawaida na kuwa mlalamikaji, badala ya kutoa mwongozo wa nini cha kufanya kuondokana na suala hilo na kueleza jinsi ya kulikabili 'genge la wahuni wanaotafubna rasilimali za nchi na kuteka mamlaka ya taifa'.
Miongoni mwa waliozungumaia hotuba hiyo, ni Mhadhiri Msaidizi Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bw. Bashiru Ally alisema kuwa hotuba ya rais ilipaswa kujikita katika kuzungumzia masuala yanayolikabili taifa kwa upana wake, kwani Dowans ni dalili tu ya tatizo kubwa nchini.
Alisema mathalani badala ya kuzungumzia Dowans, kwani kama alivyokiri mwenyewe tayari ilishazungumziwa na wasaidizi wake, rais alipaswa kuliambia taifa kupitia sherehe hizo za CCM, kuwa serikali yake itakabiliana vipi na genge la watu wachache walioteka mamlaka za nchi.
Alisema kuwa hotuba ya juzi ya kutimiza miaka 34 ya CCM ilipaswa kujikita katika kuangalia malengo makuu ya chama hicho kikongwe, masuala ya itikadi, sera na mwelekeo wa taifa, badala ya kuangalia maslahi ya muda mfupi kama vile kushinda uchaguzi, kila baada ya miaka mitano.
"Kwangu mimi issue si kulipa au kuilipa Dowans, Dowans ni dalili ya ugonjwa mzito unaolikabili taifa...ugonjwa wa kutowajibika, kikundi cha watu wachache kujilimbikizia mali, mfumo wa sheria kutofanya kazi, tatizo la kuuza na kununua kura, watu wanachukua posho zinazozidi mishahara yao.
"Hivyo hotuba ya jana (juzi) ilijikita zaidi katika kuangalia ushindi wa hali ya uchaguzi, msukosuko ambao CCM inapata kutoka kwa wapinzani kwenye uwanja wa CCM, kuwatia moyo wana-CCM na suala la kufanya mageuzi ndani ya chama...hivyo kulikuwa na imbalance (hakukuwa na uwiano sawa) na mambo mengine ya mtazamo mpana juu ya mweleko wa taifa.
"Hata ukisema chama kinafanya mageuzi, unajiuliza mageuzi kutoka wapi, CCM imepita katika vipindi mbalimbali, malengo makuu ya CCM zamani haikuwa kushinda uchaguzi, ilikuwa ni kujenga taifa huru, lenye usawa na heshima kwa watu, uzalendo, maadili. Taifa ambalo lilikuwa linazungumzia juu majirani na Bara la Afrika zima kwa ujumla.
"Kuna changamoto ya kuangalia masuala ya itikadi, sera na mwelekeo wa taifa, chama si mashine ya kutafutia kura, ni uongozi, na uongozi ni dira...masuala ya kushinda uchaguzi ni malengo ya muda mfupi sana, hakuna dira ya miaka mitano, la sivyo CCM nacho kitakuwa kimetumbukia katika mtazamo finyu," alisema Bw. Ally.
"Kwa kweli badala ya kuzungumzia Dowans tu kwa sababu Pinda na Chiligati walishasema kama alivyosema, basi rais alipaswa kuzungumzia bigger picture (mtazamo mpana) si smaller picture, juu ya matatizo yetu, angetuhakikishia namna gani serikali yake imejipanga katika mapambano dhidi ya ufisadi.
"Itapambanaje na genge la wahuni wanaotumia fursa zao za kiuchumi kuteka mamlaka ya nchi...ufisadi unaoangamiza sekta karibu zote, energy (nishati), ardhi, huduma za jamii, mfumo wa utawala, ufujaji wa rasrimali za umma," alisema Bw. Ally kwa kirefu.
Aliongeza kuwa hotuba hiyo ingeweza kueleza mwelekeo wa taifa katika wakati huu ambapo makatibu wakuu au wakurugenzi wa idara, wanajitwalia fedha na marupurupu mengi, huku wakitembelea magari ya kifahari, wakati wanafunzi vyuoni na shuleni hawana uhakika wa chakula.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), Bw. John Mnyika alisema kuwa Rais Kikwete hawezi kuepuka mzigo wa tuhuma dhidi ya Dowans. Pia anapaswa kuwaeleza Watanzania jinsi serikali ilivyoweza kuingia mkataba na kampuni feki, ambayo hatimaye iliuhamishia kwa mtu mwingine.
"Rais hapaswi kulalamika kama anavyolalamika mwananchi wa kawaida...Katika hotuba ya jana, Rais Kikwete kakiri mwenyewe kuwa Richmond ilikuwa kampuni feki, yeye mwenyewe anasema kuwa alikuwa ameishtukia, sasa ilikuwaje kampuni hiyo ikaendelea kufanya kazi na hata ikaweza kuhamisha mkataba wake kwenda Dowans.
"Ilikuwaje serikali yenye vyombo vyenye mamlaka...vyombo vya dola vilivyokuwa na taarifa kuwa Richmond ni kampuni feki, ziliruhusu kampuni hiyo iingie mkataba na serikali, kisha vyombo hivyo vikaruhusu kampuni hiyo feki ikahamisha mkataba kwenda kampuni nyingine...atuambie iwapo uhamishaji wa mkataba huo ulipitia katika baraza la mawaziri, ambalo yeye ni mwenyekiti wake.
"Lakini pia Rais Kikwete anapaswa kutuambia ni lini hasa mkataba ulihamishwa kwenda Dowans, tarehe ngapi na mwezi gani...na upande wa pili wa serikali (TANESCO) walipewa taarifa na kuridhia lini. Maana katika mkataba wa Richmond na TANESCO ilikubaliwa kuwa mkataba huo hauwezi kuhamishwa kwenda kampuni nyingine bila makubaliano ya pande hizo mbili.
"Lakini kulingana na taarifa zilizopo kutoka vyanzo mbalimbali zinaonesha kuwa Richmond na Dowans walifikia makubaliano ya kuhamisha mkataba kabla hata upande wa pili wa serikali (TANESCO) haujaridhia suala hilo...sasa rais atuambie ni lini mkataba ulihamishiwa Dowans na lini TANESCO waliridhia kuhamishwa kwa mkataba huo.
"Kwa sababu kuhamisha mkataba wa Richmond na TANESCO kwenda kwa mtu mwingine bila pande hizo mbili kukubaliana kama ilivyokubaliwa katika mkataba, kisheria ni batili...sasa ilikuwaje mamlaka zikaruhusu kuhamisha mkataba ambao tayari ulisema lazima kuwe na makubaliano ya pande mbili.
Naye Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafurila amesema kuwa maelezo hayo yameongeza utata, hatua inayolazimu suala hilo kurejeshwa bungeni kujadiliwa upya.
Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu, Bw. Kafurila alisema kuwa hotuba ya rais aliyoitoa akiwa mjini Dodoma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imezidi kuongeza utata katika sakata la malipo yanayodaiwa na Dowans.
"Maelezo ya Rais yamezidi kutuonesha kuwa kuna umuhimu sasa wa suala hilo kujadiliwa bungeni...hawezi akatuambia eti hawajui kabisa wamiliki wa Dowans huku akitaka wanasheria waangalie uwezekano wa kupunguza deni hilo au kulikwepa kabisa, wanapunguziana deni na nani huyo ambaye hajulikani? alihoji Bw. Kafurila.
Alizidi kuhoji kuwa inakuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) asimjulishe rais wamiliki wa kampuni hiyo baada ya kupitia hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC) iliyoitaka TANESCO kulipa fedha hizo, mpaka ifikie hatua Rais anasimama mbele ya maelfu ya Watanzania na kusema kuwa hawajui wamiliki hao.
"Mwanasheria Mkuu baada ya kupitia hukumu alishauri walipwe, na siku chache baadaye Waziri wa Nishati na Madini Bw. Willium Ngeleja alitaja wamiliki wa kampuni hiyo, hivyo tutaaminije kama hao waliotajwa ndio wamiliki halali na wakati Rais anasema hawajui?" alihoji.
Bw. Kafurila alisema kuwa haiwezekani rais aeleze kutowafahamu wamiliki wa Dowans na wakati serikali ilikuwa ikiwalipa fedha wakati wakizalisha umeme hapa nchini.
"Rais ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na tangu Dowans ianze kuzalisha umeme hadi leo ni lazima suala hilo liwe limepitia kwenye Baraza la Mawaziri hivyo hakuona kweli umuhimu wa kuwafahamu wamiliki hao?" alisema.
Kutokana na utata huo, Bw. Kafurila alisema kuwa malipo hayo yalipwe au yasilipwe lakini serikali haiwezi kukwepa kuwajibika katika suala hilo kwa kuwa Watanzania wamengia gharama kubwa ya kujadili jambo hilo huku serikali ikiwa kimya lakini pia kutumia gharama kuwalipa mawakili na kuendesha kesi hiyo.
Alizidi kuihoji Serikali kuwa imeshindwaje katika kesi hiyo na kampuni ambayo hata wamiliki wake hawajulikani lakini mbali na kutojulikana kampuni hiyo ni feki na yenye mkataba batili.
"Serikali katika hili haiwezi ikajitoa kwenye kitanzi hiki ni lazima iwajibike kwa namna yoyote kwani suala hili limechukua muda wetu mwingi katika kulijadili badala ya kushughulikia mambo mengine," alisema Bw. Kafurila.