Tumbo
JF-Expert Member
- Oct 21, 2013
- 282
- 347
Wana wa Tanzania wenzangu; tumejaaliwa kuwa na wasomi na wataalam wa fani tofautitofauti katika taifa letu. Tuna ma Profesa, Dakta, Injinia, pamoja na wengine wengi tu..! Swali ni je, kwa ujumla wao wanalisaidiaje taifa kutatua ama kukabiliana na changamoto mbambali zinazolikabili taifa? Je; ni mimi peke yangu ndio sioni mchango wao au hiyo michango yao tafiti, ugunduzi ama nasaha zao ndio haiko wazi ili kila mtanzania yeyote aweze kuona kile wanachokifanya na kuondoa walakini juu ya wasomi wetu? Katika nchi za wenzetu hususan Ulaya, Asia na America, tunasikia na kusoma kwenye vitabu; mara msomi flani kagundua hiki, mwingine kile nk, nk. Kila mmoja kwa nafasi yake anataka kuacha historia hata siku akitangulia mbele ya haki jina lake liendelee kuishi daima kutokana na kile ama mchango wake kwa taifa lake na dunia kwa ujumla. Hadi mtu unahisi raha na kujivunia wasomi wa taifa lako. Pengine mimi ndio sijui ama sielewi, naomba tujadili pamoja wana jamvi wote.