Gobret
JF-Expert Member
- Jun 11, 2010
- 320
- 88
Hii ni hatari kweli. Lkn pia sishangai kusikia kuwa wsomi uchwara wa Udom wanamfagilia huyu mbayuwayu. ikumbukwe kuwa udom ni chuo kilichoanzishwa katika mazingir ya siasa. KAma watu tunaodhani kuwa watatoa mwanga kwa wale waliogizani ndio wa kwanza kutuhadaa na kutupoteza unadhani nini kimebaki? Malipo ni hapa hapa DUNIANI. KAMA ULIMCHAGUA MBAYUWAYU KWA SABABU ZA KISHABIKI AU KWA SABABU NZURI TU TUVUMILIE KWA SABABU TUNAPOKEA MSHAHARA WA MAWAZO YETU KUWA FINYU. Watu hawaelewi maana ya siasa wala hatuna utashi wa siasa. Tuna kukuruka tu. Mara utasikia: huyu ni kijana mwenzetu au mzuri bwana au kichaa wangu; hatuangalii maslahi ya nchi na watu wake. Vijana hatupigi kura tunashabikia siasa tu kwa nje. Akina mama wanapiga kura kwa wingi wakifuatiwa na wazee lkn vijana NONE of OUR BUSINESS. Vijana ni taifa la leo, sisi ndio tuamue nani tunayemhitaji na tushiriki katika hatua zote za uchaguzi. Sisi tuonyeshe kuwa tunakerwa na hii hali kuwa wazee tu ndo wanaweza. Hakuna kitu kama hicho sisi ndo wahitaji zaidi na tutawale kwani ni kipindi chetu kutawala. Kwa nini wazee watutawale na hali kipindi chao kimepita? Wao watupe mawazo na hekima ya kutawala."Lets take action as of today". Tuache blablaa nyingi wakati wa uchaguzi. Tujiandikishe kwa wingi zaidi sisi pamoja wenzi wetu. Tuwashauri wazee na wazazi wetu watuunge mkono kwa sababu nao wanatutegemea kwa sasa. Sasa kwa kukosa kazi wanaitwa Karimjee kumshangilia mbayuwayu. Hawana kazi.Kila kheri watu wangu.