Wasomi UDOM waandamana kumuunga mkono JK kuwa mgombea pekee CCM, akerwa na Zitto!

Huyu msanii {JK}Kweli mbali na kushindwa kumuelewa kwa kauli zake anaendelea kutushangaza kwa ngojera ngonjera mpaka lini sehemu yake sio ikulu ni kwenye vikundi vya sanaa bora ajiunge na John komba TOT anazungumzia kumpyuta wakati asilimia kubwaza mashulea hazina hata madawati,walimu mahabara,na wanafunzi wanasoma chini ya miembe wavuti - Video kweli tunakazi.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
"

Imefikia wakati ambapo badala ya kumbeza rais wangu inabidi nianze kumsikitikia kwa kuwa ana safari ndefu, urais ni kazi ngumu.

Ni kweli Luteni, kuna thread moja hapa sikumbuki ilikuwa ni ya nini, Mwanakijiji alisema amefika stage anahisi kama tunamwonea rais. Niko na feeling hiyo hiyo mimi pia, frankly ninahisi kana kwamba tunamuonea mr president. Kuna vitu kwa kweli anaviongea halafu masikio yangu yanagoma kupokea kwamba no hajasema pamoja na kwamba ni kwenye luninga na ninamwona kwa macho yangu. Wale madaktari wa Cuba i doubt majibu yao kwa kweli.

Unajuwa nimefika mahali ninashindwa kuimagine hivi Kikwete asiyekuwa na serikali (mawaziri, makatibu wakuu na wengineo),washauri lukuki, usalama wa taifa, jeshi, chama tawala na mengineyo yasiyo na idadi anafananaje? Huyu mtu ana hizi organs zote nilizotaja na nisizotaja kumfanya ajuwe exactly what's going on na ni kipi cha kusema na kufanya ili nchi hii iende mbele lakini still kila siku ni kutusononesha tu tuliomchagua. Kwa wale tunaoamini Mungu kama mimi nadhani ipo haja ya kumwomba Mungu sana katika hili jambo, its more than serious.
 
Heh heh wanafunzi wa Vyuo Dodoma ati ndio viongozi watarajiwa,sijui viongozi gani hao wanadanganyika kiurahisi eti kisa vijisenti walivyopewa na Mzee wa Lushoto,hakika kumbe hata wasomi hawana maono na wanashindwa kupambanua hali halisi ya mambo yanavyo enda nchini,hao wasomi ni sawa na akina Profesa J wanachoimba hakiendani na wanachokitenda,sasa nimeamini maneno ya Kardinali Pengo kuwa tunapiga kelele kuwa kuna mafisadi,kwa kuwa tumeshindwa kuipata hiyo nafasi,kwa maana nyingine tunayoyafanya hadharani ni unafiki tu,ni njaa za wakati huo tu mtu akija na vijisenti vyake hakuna asiyenunulika,hata angekuwa ni msomi wa PHD!.
Naweza nikawapuuza hao wanamziki wanaoipigia debe CCM kwa kuwa shule kwao imewapitia kiasi mbali lakini kwa wanafunzi wa vyuo ni aibu kubwa.
 
I think UDOM ipo for political credits,ila inasikitisha sana kuona wasomi wetu ndo wanakuwa majuha number one,any way,kuna mtu alisema vilaza wanaokosa chance UDSM hufanya UDOM ndo kimbilio lao,nilikuwaga siamin,..ila kwa hili...ninin kitanizuia nisiamin hivyo...

Nadhani hauko sahihi, hizo ni hisia tu, huna facts, na hapo ndipo ninapoquestion usomi na ujuvi wako pia. UD wamefanya nini mpaka sasa?
 
Ni kweli Luteni, kuna thread moja hapa sikumbuki ilikuwa ni ya nini, Mwanakijiji alisema amefika stage anahisi kama tunamwonea rais. Niko na feeling hiyo hiyo mimi pia, frankly ninahisi kana kwamba tunamuonea mr president. Kuna vitu kwa kweli anaviongea halafu masikio yangu yanagoma kupokea kwamba no hajasema pamoja na kwamba ni kwenye luninga na ninamwona kwa macho yangu. Wale madaktari wa Cuba i doubt majibu yao kwa kweli.

Unajuwa nimefika mahali ninashindwa kuimagine hivi Kikwete asiyekuwa na serikali (mawaziri, makatibu wakuu na wengineo),washauri lukuki, usalama wa taifa, jeshi, chama tawala na mengineyo yasiyo na idadi anafananaje? Huyu mtu ana hizi organs zote nilizotaja na nisizotaja kumfanya ajuwe exactly what's going on na ni kipi cha kusema na kufanya ili nchi hii iende mbele lakini still kila siku ni kutusononesha tu tuliomchagua. Kwa wale tunaoamini Mungu kama mimi nadhani ipo haja ya kumwomba Mungu sana katika hili jambo, its more than serious.
Bobby

Unajua huwa nakaa nashindwa hata kujiuliza inakuwaje rais ambaye najua ana uelewa mkubwa wa hali halisi ya watanzania kuliko mimi aweze kupanga mambo makubwa ambayo hata nchi zilizoendelea ndiyo kwanza yako kwenye pilot stage.

kama ulivyosema inawawezekana organs zote zilizomzunguka hazimsaidii au zimeoza iwe kwa ushauri au utekelezaji, kama wangekuwa wanamshauri vizuri haiwezekani awe anakataa kila kitu kizuri na kuzungumzia mambo yakufikirika.

Mfano wa shule zetu zilivyo na huu mpango wa IT, inawezekana anapotaka kukagua shule huwa anapelekwa Mzizima sec, Shabaan Robert, Benjamin Mkapa sec na kujiridhisha kuwa tunaweza kufundisha kwa IT, wasaidizi wake wangekuwa wanampeleka shule kama hizo hapo juu nadhani hata wazo la kutumia IT asingelisema.
 
don't abide with J.K's porojo! jamaa ni bingwa wa porojo sijawahi kuona, halafu anazitamku mbele ya wanafunzi wa chuo kikuu (hivi wanavyuo wa siku hizi wapoje?).
 
Kwa bahati mbaya chombo kinaenda mrama na mbaya zaidi kiongozi wa chomba hajui kuwa tunaelekea tusikokutarajia, tunapotea! Mpaka tupate nahodha anayejua tulipo, tuendako, na nini kifanyike tufike tuendako. Kikwete ameomba tena achaguliwe, akapige picha na akina Drogba, Boys II Men, Kaka, n.k. huyu ndiye nahodha tunatarajia kuwa naye kwa miaka mingine mitano, kufikia 2015 Zimbabwe ya 2005 itakuwa Adeni ukilinganisha na Tanzania ya wakati ule.
 
Kwa kweli "rahisi" tunaye. Nashindwa kuelewa ni utoto, ulimbukeni, au ni nini? Hivi kweli "rahisi" anajua kila analoongea!! I doubt!!
Hizo kompyuta anazosema watoto mashuleni watatumi, zitatumia nini kama hata umeme wa kuaminika tumeshindwa kuwa nao pamoja na kuwa tuna kila rasilimali za asili tunazoweza tumia ku-genereate power!! Au ndo zile ndoto za EL kuleta mvua ya kichawi!!!

Ni wazi shule zote vijijini ziko kama mkuu Luteni ulivyotuletea...!! Halafu anakuja kuota huku anahutubia kuwa amepata strategic partner wa kufunga inteneti watoto wasome kwa techno hii!!!

Mr. Prezidaa, naona unaendelea kutuhakikishia na kutuondolea mashaka kuwa HUNA UWEZO and so ili kulinda heshima yako acha 2010. Acha baba!!! Umeshindwa.
 
Niko Dodoma jamani; it was not that big and am sure wengi wao sio UDOM students kwani wawili wanatoka mtaani I know them!
 
Kwa kauli zako na Lugha yako (kiingereza cha mtaani), ni dhahiri kwamba wewe siyo Nkunya tunayemfahamu.

Si vizuri kutumia majina halisi ya mtu fulani wakati wewe siye. Maana unaweza kumharibia mtu sifa yake na kumgombanisha na watu wake wa karibu. Napendekeza moderator achunguze kwa makini uhalisia wa jina hili.

Lakini kwa upande wa hoja yako ya wasomi kumuunga mkono Kikwete, napenda kuungana na wewe kwamba wasomi walipaswa kuwa ndiyo chachu ya mabadiliko. Maana wakulima kule vijijini, pamoja na shida zote wanazopata, wakiona wasomi wamemuunga mkono Kikwete, hawatakuwa na lingine tena.

Lakini pia ni jambo zuri kutambua kwamba hawa ni wanaCCM, hawana lingine la kufanya zaidi ya hilo la kuunga mkono kinafiki. Ukikaa nao mmoja mmoja utakuta wanalalamika, lakini wakiwa katika chama wanalazimika kufanya hayo wanayoyafanya. Ni haki na wajibu wao.

Hao si wasomi bwana . Tanzania wasomi wote si makini na labda wasomi wa JF wana maana zaidi kuliko tunaodhania kwamba ni wasomi wote wana anadaa mazingira ya wizi wizi baadaye ni kuwabana tu hakuna namna .
 
Nadhani hukufanya sahihi kutumia maneno makali kiasi hiki.

Jamaa anayo hoja ya msingi, juu ya jina la mwanaJF mwenzetu. M.M. Nkunya siku alipojiunga wengi tulisisimka na binafsi niliamua kumuuliza kama ni M.M.Nkunya tunayemjua (huenda wewe humjui ila alikuwa Chief Academic Officer wa UDSM kwa muda mrefu, baada ya hapo (mpaka sasa nadhani) ni CEO wa Tanzania Commission of Universities. Kutokana na madaraka yake huyu ni mtu muhimu ktk jamii. Jamaa kaona lugha iliyotumika haiwezi kutumiwa na Prof. M.M.Nkunya.

Nami naonelea kuwa si vema kutumia jina la mtu mwingine (kama unatumia nick name). Itakuwa si vema mtu akijitokeza jamvini kujiita J.K. Kikwete au M.L. Luhanga au I.H. Lipumba nk. Haya ni mawazo na mapendekezo binafsi, wala hakuna haja ya kuitana wajinga.

Asionewe lakini.....nadhani Nkunya wako wengi tu.....for the benefits of our doubts hajatumia title ya Professor othewise namjua mtu anaitwa Juma Mohamed Kikwete....sasa huyu akijifupisha si J.M.Kikwete?.....kumbukeni watawala hawamiliki majina wala ubini au mmesahau issue ya Mzee Kimiti kudai Fataki ni babu yake?
 
Kushindwa kujitambua na kujitegemea, cheap students. Na mtaendelea kununulia kwa bei ndogo hadi siku zenu za maisha yenu yenu na hata vitukuuu vyenu.
 
Zitto,zitto,zittooo na jakaya hapa si kama tyson na matumla. Hivi ilikua sahihi kweli jk kumjibu zitto kwa swala alilouliza bungeni? Sasa atajibu mangapi? Na sisi humu jamvini tuna muuliza au tunauuliza hao watoto waliokuchangia pesa wametoa wapi?kama raisi mbona hujauliza, douuuu ccm inatoa damu mpaka maiti
 
Kushindwa kujitambua na kujitegemea, cheap students. Na mtaendelea kununulia kwa bei ndogo hadi siku zenu za maisha yenu yenu na hata vitukuuu vyenu.

Wanajipendekeza tu unafikiri kuna kingine hapo? ni hicho tu,
 
Siasa za geuka mipasho

Raisi anataka kuifanya siasa na kuwa mipasho maana si kuja kujibizana kwa vijembe na mafumbo yaliyo wazi. Ni ukweli kwamba ni ilani ya CHADEMAiliyotamka wazi wazi kuifanya dodoma kitive cha elimu. Kama CCM wamelioli lilikua jambo jema na wakatohoa, wangekiri tu kwamba vichwa vya vijana vinafikiri haraka kuliko mawazo mgando ya kina Ngasongwa waliotunga ilani yao.
Kwa raisi kujibizana na mbunge , tena kwa kuhoji matamshi ya mbuge bungeni nje ya bunge, ni upunguani na sishangai kwakua limetoka kwa mtu tunaemjua. Anyway labla alikua anatania Soon atakuja Salva Kurekebisha
 
Akili ileile ya utegemezi..

Halafu hizo kompyuta zitawashwa na nyasi au udongo? Umeme wenyewe coverage iko less than 15 % na hakuna plans za kuongeza capacity.

Nadhani wakuu wa Makampuni wamemhakikishia JK kwamba kuna Computer zinawashwa na samadi ya Ng'ombe au kuni!

JK - I hate you!
 
Hivi tunategemea nini kutoka kwa wanafunzi waliojiunga uni kwa kuiba mitihani ya kidato cha sita? hatuwezi vuna ngano kwenye shamba la bangi!
 
Back
Top Bottom