WASOMI: Tatizo si Mawaziri ni Mfumo!

Ufafanuzi ni muhimu sana ili kuondoa mkanganyiko uliowapata watanzania wakiwamo wanafunzi wanofundishwa tofauti na wanayoyaona wakitendwa.
 
Hapa tunahitaji wanasheria walipo kwenye mjamvi watupe shule hiyo. Nivifungu vip vimevunjwa japo issue hii inaonekana kuwa wazi kutozingati taratibu. Malezo ya kina yakutuelimisha wadau ni muhimu. otherwise peopleeeeeeeeeeee ................................!
 
Kwenye mfumo mbovu hata mtu mwaminifu anakuwa mwizi, lakini kwenye mfumo imara hata mtu mwizi anakuwa mwaminifu !

Serikali za ulaya hazikumbani na matatizo kama haya kwa kuwa mifumo yao ni imara.

Kwetu TZ mfumo imara ni ngumu kupatikana kwa kuwa mifumo mibovu ina manufaa makubwa kwa hao wakubwa wenye hiyo dhamana ya kubadili mifumo.

From me Goodrich, 05 May 2012.

Nakubaliana na wewe Goodrich. Mifumo mibovu ya UDHIBITI na utawala ukiwa inclusive, ndiyo imetufikisha tulipo sasa. Mfano wa ubovu huo na Kiongozi mmoja kuwa mwenyekiti wa chama na pia kuwa Executive wa serikaqli. Excessive power. Then anakuwa na mamlaka ya kuteua watendaji ambao ni wa chama chake kuchukua nafasi serikalini. Anawateua viongozi wa taasisi za kuchunguza rushwa, kukagua, haki(mahakama), magereza etc. Ukitaka kuona ubovu wa mfumo huu, ni pale kiongozi kama wa uwaziri au ukatibu mkuu anapokuwa na scandal. Ni vigumu kama siyo haiwezekani, kwa wateuliwa kushughulikiana. Wa rushwa kuchunguza, mdhibiti na mkaguzi mkuu, hakimu and etc, wote kumshughulikia mwenzao wakati huo huo wote wakiwajibika kwa aliyewateua. Ikumbukwe pia ya kuwa katika mazingira ya scandal kunakuwa na personal interests za anayeteua, chama chake, taasisi, marafiki, ndugu, jamaa etc. Si rahisi kwa interests za umma kukumbukwa na ndiyo maana maovu mengi makubwa makubwa ama yanashughulikiwa kwa shida na au hayashughulikiwi kabisa. Kwa ubovu wa mifumo hii, yeyote regardless ya moral stance yake kabla ya kuingia kwenye mfumo huu, atabadilika tuu na kwenda kama mfumo unavyotaka pindi aingiapo kwenye mfumo huu. Yanakuwa yale yale ya "the way we do things around here"-utamaduni. Ni wakati sasa mifumo ya udhibiti na utawala kubadilishwa through katiba, sheria. Lakini pia hata utoaji wa elimu ya maadili unatakiwa kuongezwa sana na kutiliwa mkazo tena kuanzia kwenye mitaala ya elimu ya msingi hadi vyuoni na makazini.
 
Elimu ya Uraia ndio ufunguo kwa haya yote. Ikiwa watu wetu watakuwa wamepata elimu ya uraia ya kutosha wao wenyewe watajua jinsi ya kuweza kukataa ujinga wa aina yoyote hata kama unatokea Ikulu. Kwa hiyo kazi kubwa mbele yetu tulio na mwanga kidogo ni elimu ya URAIA vijiweni, kwenye misiba, kwenye harusi, vijijini, shuleni, vyuoni na hata kwenye vituo vya kusubiri mabasi. Sema kwa anayesikia, tumia ishara kwa asiyesikia. Elekeza, elimisha, elezea ili wengi wakielewa tutaweza simamia haki sio kwa serikali hii tu, bali hata nyingine zijazo.
 
tuelezeni vifungu vya katiba ili tujue vzr ili la muungano.Hivi kuna kipengele gani kimevunjwa kwa kumteua mtu ubunge saa 8 kutangazwa uwaziri saa 10?mfumo wetu ndo unazalisha viongozi wabovu
 
Mbowe alisema kuwa uteuzi wa Dk. Hussein Mwinyi anayeingia bungeni akitokea Jimbo la Kwahani Zanzibar kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, haukuwa sahihi, kwani wizara hiyo si ya Muungano.

huo uteuzi hata mimi siuelewi...wakati mwingine naonaga kama vile sisi watanganyika tumeolewa na wazanzibari..tuko tayari kufanya chochote mradi tuwafurahishe wao...but si mnajuaga hata kwenye ndoa ipo siku mke anamchoka mume anaomba talaka..and that day is around the corner.
 
Mwenye idea na mfumo mbadala naomba anijuze, wapi kuna tatizo na nini kifanyike. Na je, mfumo wa utawala uko katika ilani ya chama au ndani ya katiba. Kama unpashwa kubinishwa katika katiba basi isiwe siri, tujuze ili tulisistize hilo katika mchakato wa katiba mpya. Tusilifanye hili sili kama jando! ( alisema JKN). Tujuze watendaji wateule, na wale wasio stahili uteule wa mkuu wa nchi. Mamlaka wa waziri mkuu na ukimeo wa kuwepo kwake. Please!:flypig:
 
Mwenye idea na mfumo mbadala naomba anijuze, wapi kuna tatizo na nini kifanyike. Na je, mfumo wa utawala uko katika ilani ya chama au ndani ya katiba. Kama unpashwa kubinishwa katika katiba basi isiwe siri, tujuze ili tulisistize hilo katika mchakato wa katiba mpya. Tusilifanye hili sili kama jando! ( alisema JKN). Tujuze watendaji wateule, na wale wasio stahili uteule wa mkuu wa nchi. Mamlaka wa waziri mkuu na ukimeo wa kuwepo kwake. Please!:flypig:
 
Msisahau kama tunatofautisha Siasa na Utendaji, kama utangalia anachofanya Raisi wetu ni Siasa na kwa upande wa Mawaziri wanashindwa kufanya katika utendaji mwema. Kwa Mfumo wa Tanzania nafikiri tuache siasa hapo tutafika maanake hata hawa wasomi wanafundishwa na wanasiasa Vyuoni mwao ,Kikubwa kuwa WAZALENDO WA INCHI YETU ukiona mtu haendi vizuri aambiwe na si kumuondoa .:flypig::mimba:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom