Wasomi - CCM: Tuna mafisadi 100; Wataka chama chao kiwatimue haraka

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Hellen Ngoromera na Irene Mark



UMOJA wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi kutoka vyuo vikuu nchini, umesema hatua ya CCM kujivua gamba kwa kufanya mabadiliko ya kiutendaji haitoshi kwani ndani ya chama hicho na serikali yake kuna magamba (mafisadi) zaidi ya 100 yanayotakiwa kuondoshwa.
Kauli ya wasomi hao imekuja huku Mjumbe wa Mkutano Mkuu UVCCM wilaya ya Moshi Mjini, Paul Makonda, akibainisha kuwa uongozi wa kitaifa wa jumuiya hiyo nao unapaswa kung’olewa kwani nao unafanya ufisadi wa kutumiwa na mafisadi ambao unazidi kukiua chama hicho na jumuiya yake.

Makonda alisema kinachofanyika ni kuhakikisha mafisadi wote ndani ya chama wanaondoka kwa kuunda ‘UVCCM Maadili’ na kukiondoa ‘UVCCM Maslahi’ chini ya uongozi wa Benno Malisa na ushawishi wa Hussein Bashe.

Umoja huo pia umetangaza kufanya operesheni maalumu nchini kumsaidia Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, kuwaondoa mafisadi ndani ya chama hicho.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu wa Umoja huo Leoni Mboya na Mwenyekiti wake Nestory Chilumba, walimpongeza Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete kwa ujasiri aliouonyesha wa kufanya mabadiliko hayo na kutaka mfumo mzima ndani ya chama hicho kubadilishwa.

“Sisi kama vijana wasomi tunaamini kwamba CCM kujivua gamba si tu kujiuzulu kwa sekretarieti wala kufukuza wanachama wanaokipotezea umaarufu bali kufanya mabadiliko ya mfumo mzima wa chama kuanzia mwenyekiti taifa hadi shina pamoja na katiba ya chama.

“CCM kuna magamba zaidi ya 100 hivyo kuna haja ya kutoa gamba moja hadi jingine, wembe uliotumika kwa sekretarieti utumike kwa watu wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya chama …tumechoshwa na kelele za wapinzani,” alisema Chilumba.

Alisema wao kama wana CCM wapenda maendeleo wanamwakikishia mwenyekiti wao kuwa watakuwa bega kwa bega naye kwa kila hatua anazochukua ndani ya chama hicho ili kukiwezesha kuwa na wanachama wenye maadili, uadilifu na nidhamu.

Aliishauri sekretarieti kuu ya chama hicho kutekeleza ahadi yake ya kuwashughulikia wanachama mafisadi na kusema wana matumaini nayo katika kukiletea chama hicho mabadiliko makubwa.

Kuhusu kutaka uongozi wa umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM) kujiuzulu kutokana na kushindwa kazi, Chilumba alisema kwa kuwa kuna sekretarieti mpya wameona ni busara wakaonane nayo ili kuona njia za busara zinazofaa katika kuhakikisha UVCCM inajisafisha.

Wanachama hao hai wa CCM walisema kwa sauti moja kuwa hawao
gopi nguvu yoyote ya mafisadi na kama wana pesa nyingi waanzishe chama chao.

Akizungumzia kuhusu operesheni kokoro ambayo wamepanga kuifanya hivi karibuni Katibu, Leoni Mboya, alisema itakuwa na lengo la kuwaondoa mafisadi wote.

“Tunataka umma uelewe kuwa kuna operesheni kokoro inakuja, hii itakuwa maalumu kwa ajili ya kumsaidia mwenyekiti wetu kuyaondoa mayai na ‘mapapa’ ndani ya CCM ikiwa hawatafanya hivyo wenyewe,” alisema Mboya.

Kwa upande wake Makonda alisema mfumo mbovu wa utawala na kusubiri vikao ndani ya chama hutoa mwanya kwa matajiri wachache wenye maslahi binafsi kukiharibu chama na jumuiya zake.

Katika hilo alipongeza uamuzi wa mwenyekiti wao Kikwete kubadili uongozi wa sekretarieti na kutoa changamoto kwa viongozi wapya chini ya Katibu Mkuu Wilson Mukama kuunda mfumo bora wa uongozi ili kukiimarisha chama na kurejesha imani ya wananchi kwa chama hicho.
“Inahitaji utashi na uamuzi mgumu kubadili uongozi katikati ya safari… haijawahi kutokea tangu kuanza kwa CCM, baada ya mabadiliko hayo naamini sasa changamoto kubwa ipo kwa hiyo sekretarieti mpya ihakikishe inabadili mfumo, itoke kwenye sera za kitamaduni tulizorithi ikipeleke chama kwenye sera za kisasa.

“…Sekretarieti iliyopita ilikuwa inasubiri vikao na taratibu bila kujali madhara yanayokikumba chama kwa kuchelewa kutoa maamuzi kwa wakati. Ilifika kipindi chama kinafanya mabadiliko kutokana na kauli ya wapinzani.

“Naishauri sekretarieti mpya kurejesha heshma na imani ya chama… tunategemea mabadiliko makubwa sasa,” alisema Makonda huku akiongeza kwamba kinachotakiwa ni kubadili mfumo.
Alisema UVCCM maadili ipo kwenye mchakato wa kuunda umoja mpya utakaosaidia kukuza na kukiimarisha chama huku akibainisha kwamba wanaruhusiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.


h.sep3.gif


 
Hhahaaa........zungukeni tu tuwapige Supplimentary za kufa mtu.........

Ninapoona haya mambo yote najivuna kuwa kijana ndani ya CHADEMA....nimewapa changamoto "UVCCM Maslahi" kuanza kuwaza kujisafisha na kuchukua sura mpya...............Nimewaamsha CCM kujua umuhimu wa vijana kupewa kipaumbele cha juu katika kuendesha na kuleta mabadiliko

Vive le CHADEMA..........
 
Sielewi kwanini hawa watu wa MAGAMBA wanaona kitendo cha kubadili uongozi wa chama ni kitu cha KUPONGEZWA SAAANA!
To mee, this is too personal, na hatuhitaji kuiamplify sana!,....
Kazi yetu ni moja tu...kuking'oa chama hiki...basi!
 
Mfumo wa uendeshaji wa chama cha CCM ni mbovu uliopelekea serikali ya CCM kutokuwajibika kwa wananchi,ukweli CCM ndio gamba lenyewe inapaswa kuondolewa maneno maneno na matamko hayatatubadilisha wananchi
 
nngu007
MAGAMBA 100?kwenye hiyo taarifa sijaona list ya hayo majina ya magamba 100,mi nakubali kweli magamba yapo ila si 100 tu,ni zaidi ya hayo,sasa kwa kuwa yeye anayajua hayo 100 angeyataja hadharani vinginevyo ni kutafuta umaarufu tu wa kisiasa.mbona cdm waliyalist mwembeyanga 2007?

"ukitaka kupanda ghorofani bila lift tafuta ngazi imara si ya mabua!"
 
Wanazunguka sana lakini ukweli ni kwamba CCM ndio GAMBA lenyewe inabidi watanzania tuelimishane tujivue!!!
 
nngu007
MAGAMBA 100?kwenye hiyo taarifa sijaona list ya hayo majina ya magamba 100,mi nakubali kweli magamba yapo ila si 100 tu,ni zaidi ya hayo,sasa kwa kuwa yeye anayajua hayo 100 angeyataja hadharani vinginevyo ni kutafuta umaarufu tu wa kisiasa.mbona cdm waliyalist mwembeyanga 2007?

"ukitaka kupanda ghorofani bila lift tafuta ngazi imara si ya mabua!"
Nusu ya wanachama wa CCM ni magamba, ila wanatofautiana ukomavu wa magamba yao
 
Hapana wasitoke walipo wataenda wapi kama sio kuja kwetu walae nao waliwalea
 
CDM tutawachokonoa mauozo yenu mpaka mtupe nchi.Hakuan UVCCM maslahi wa UVCCM Maadili wote watoto wa mama mmoja hamna la kutuambia.Letu ni moja tu,kukizika ccm!!!end of the game,tumechoka kuimbishwa mashairi mabovu....CCM ovyoooooooooooooooooooooo!!!!!!
 
Moto chini, moto ndani, moto nje. Tutapiga kushoto kulia katikati na juu mpaka CCM ife.

INatia hasira sana wapotokaji wanapo -politcize sentive issues. Ufisadi ni CCM. Ondoa CCM umeondoa ufisadi. Ua CCM umeua Ufisadi...simple.
 
Chama kimeoza, kuvua magamba haitoshi...kife kwanza then kizaliwe upya kwa jina lingine tofauti na CCM...maana watanzania tunapo sikia hilo jina Linatonesha vidonda vyetu walivyotupa...WAKAE KANDO, wameshndwa kazi
 
...................Tunaomba majina yao plz...sio 100 tu watupe na majina tuwajue...............
 
jaman watu mia moja du ccm mnatisha siku nikisikia ccm imekufa hatakama itazikwa marekani lazima nikahudhurie mazishi yake manake chama hiki ni hatari kuliko bomu la nyuklia
 
Back
Top Bottom