Wasome Wanawake tu: Siri za unyago wa Kimakonde!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Kwa kawaida wasichana hupata mafunzo ya unyago ndani ya nyumba siyo porini. unyago wa wasichana ni mgumu kuuelezea tofauti na ule wa wavulana maana mambo mengi hufanyika na wanawake kwa siri kubwa. Wamakonde wanaamini kuwa kueleza ovyo ovyo mintarafu mafundisho ya unyago kwa wasichana mtu huweza kuandamwa na balaa hivyo basi ni mwiko mkubwa kusema sema hadharani. Kamwe siyo rahisi kumithilisha mafundisho yale wapatayo wavulana na wasichana.

Kwa jumla wasichana wanaohusika yawapasa kuvumilia taabu na magumu mengi pindi wawapo katika unyago. Ni marufuku kwa msichana kulia au kulalamika kwa sauti hata kama angeandamwa na maumivu makali namna gani. Hutawishwa kwa muda fulani pengine kwa muda fulani pengine kwa kipindi kirefu hadi ajaliwapo kupata mchumba.Maisha yote toka utoto hadi umri wa kuvunja ungo kwa msichana wa kimakonde hufuata madhehebu ya unyago yajulikanayo kama chiputu.

Wamakonde wanaamini kuwa kwa msichana bila kupitia mafunzo ya unyago kwa jinsi ya mila na desturi yao matunda ya ndoa hayangefikia au yasingekuwa mema kwa sababu msichana yeyote asiyepitia unyago huhesabiwa kama mwanamke haramu. Mara nyingi hasa siku hizi wasichana hupata mimba kabla kabisa ya kupatiwa elimu ya unyago. Wanao angukiwa na mkasa kama huo hawapatiwi tena mafunzo ya unyago ambayo ni msingi kabisa wa maisha
yao. Hupachikwa jina anahaku popote aendako. Wazazi hushikwa na majuto sana iwapo binti yao ameingia katika mkumbo huu wa akina anahaku.

Anahaku huwa hawana raha maana huwakosa marafiki au huadhiriwa.
Mafunzo ya unyago huanza mapema sana hasa kwa watoto walio watundu na watukutu. Wasichana wengine huwa wamekwisha kulumuka mwongo yaani kuvunja ungo kabla ya kuingia kwenye unyago. Hao hutofautishwa na wenzi wao kwa kuwavisha vidani viitwavyo inano (kundolela inano) kwa kupasua katikati mbegu ya mti uitwao mkangaula.

Kamwe unyago haupangwi hivi ili ufanyike wakati msichana apatapo hedhi mara ya kwanza ili kama imetokea bahati hiyo basi Bi mkubwa yaani Likolo hutengeneza imale. Likolo hujipaka imale maungoni mwake na mwa walombo wengine ili kujikinga wasije wakapata upofu wa macho katika kushirikiana nao.
Kama ilivyo elezwa hapo nyuma kwamba matendo ya madabwa yafanyikayo hayasemwi ovyo. Wasichana wa dini za kikristo hawapatiwi tena mafunzo ya unyago kwa ukamilifu bali hupewa mabugo ambayo ni mafunzo mafupi nayo hudumu kwa muda wa siku saba hivi. Hufundishwa juu ya miiko wajibu na matarajio ya mama wa Kimakonde katika jamii.

Wasichana wote kabla ya kuingia unyagoni hujulikana kama anahaku wengi wanamahaku na baada ya kufundwa hujulikana kama mwali wengi wanawali. Akina mama hujikusanya pamoja na kufanya shauri la kuwapeleka binti zao kwenye chiputu. Wakisha afikiana humchagua Likolo kuwa ndiye mkuu wa taaluma za unyago. Ujira huo hutofautiana baina ya kijiji na kijiji kutegemea uhusiano na uelewa uliopo kati yao. Nyumba ya kutolea mafunzo hayo inande yanole huchaguliwa.Jioni ya siku iliyochaguliwa kuwa ndiyo ya kuanzia mafunzo ya unyago kila msichana atakaye hudhuria mafunzo hushikwa kukamula na wakala fulani ambao wameidhinishwa na wazazi.

Wakala wa kuwakamata wasichana wanaweza kuwa ni wifi nnamuwe wake au mwanamke yeyote yule ambaye anajuana na yule msichana vya kutosha. Mwanamke ambaye ni wakala asiye shemeji yake huitwa ankamwe-nole.
Baada ya kumshika msichana hupelekwa kwa mama yake. Mama binti mwenyewe pamoja na nnombo huenda pamoja hadi kule inande yanole. Wakaribiapo inande yanole huimba nyimbo za kumwandaa yule binti anaye sindikizwa kwenye chiputu. Wanapo wasili hapo wasichana huamkiana kwa kugonganishwa vichwa vyao ikiwa ndio ishara ya kuhimiza uhusiano mzuri kati yao kwa muda wote watakapo kuwa pamoja.

Nitaendelea kuwadondoshea siri zaidi kesho, Inshaallah!

MUENDELEZO....

Uyeyele huwa ni hatua ya kwanza kuendeshwa. Mara hupekelekwa na likolo kwenye inande yanole na huamriwa kuketi katika safu. Ngoma ya nsakata huchezwa mbele ya inande yanole; wake kwa waume hucheza pamoja huku ngoma mbili zikidundwa. Nganga ni ngoma ndogo na ile ndefu na kubwa huitwa Likuti, nakudunda, mikoli n.k., msondo. Ni wapigaji mashuhuri tu hualikwa kupiga ngoma na kucheza ngoma ya ntengu katika sherehe kama hizo kwa mapatano ya ujira fulani. Mbele ya wanawali huwekwa upinde ambao huazimwa kutoka kwa mwanamke yeyote yule wa umri wa kutosha. Shabaha ya kuwa na upinde ni kuunganisha matendo watakayotendewa hivi karibuni tu na tendo la kuuvuta na kuunyoosha.

Wanawali huelekezwa kanuni za kwanza mojawapo ni ile ya kuamka mapema. Wamakonde ni mabingwa sana wa kutoa mafunzo hayo kwa kuwaimbia nyimbo tamu zenye kutaja maadili mbalimbali yampasayao mwanamwali.
"Nditi kulala kwake luwali chichi nahunda vali, nkalabola mawali!"

(Maana yake: tabia njema huleta raha katika jumuiya)

Nyimbo zenye methali na vitendawili hufululiza hata kuamsha usikivu na ari ya kuwa tayari kuyasikiliza mafunzo kwa makini na kuzingatia. Wanawali hutolewa hofu na woga ambao wangeweza kuwa nao iwapo kama mkazo usingefanyika kwa kuwatumbuiza na nyimbo hizo. Waimbaji na wacheza ngoma huhakikisha kuwa maelezo hayo yanawakolea barabara wale wasichana. Mwanamke mmoja mashuhuri huushika ule upinde huku akiuchezea kwa kuuvutavuta na nyimbo zikiporomoka na wale wanawali huongozwa kwenda ndani ya nyumba. Toka saa ile hakuna anayeruhusiwa kuingia kuwaona wale wanawali ila ndugu halisi wa kike na wale walombo. Majirani wengine hawatawaona tena ila baada ya kuhitimu shughuli za unyago.

Usiku wa kwanza, wale ndugu walioruhusiwa kuingia mle ndani huwaandaa mintaarafu mazoezi hatua kwa hatua na yale yatakayofanyika usiku utakaofuata. Kusema kweli wanawali wanatolewa hofu kubwa sana maana mazoezi yenye soni nayo huanzishwa na ndugu zao halisi badala ya kushtushwa na walombo. Wamakonde hutumia methodolojia hiyo ya jadi ya mafunzo ya kupumbaza kwanza mhusika, sawa kama mkondo wa mazingira katika maisha ya kila siku yanavyompumbaza binadamu kabla ya kumwangamiza. Bumbuwazi waipatayo binadamu kabla ya mafuriko, matetemeko au ajali ya gari.

Baada ya kuwapa mafunzo ya mzuzu, wanawali huogeshwa na kutawazwa. Wengi kati yao hawapati lepe angalau moja la usingizi maana ngoma na nyimbo huendelea kuporomoshwa usiku kucha. Usiku huo wa kwanza hupatiwa chakula usiku wa manane. Ndugu wa kila mwali hujitahidi awezavyo kummchangamsha mwali wake ili walao atakapohitimu awe amezingatia maadili yote kutoka kwa walombo.

Usiku wa pili ndugu hawaruhusiwi tena kuwa pamoja na wanawali maana walombo wamekwisha patwa na umori ili kuonyesha uwezo wao. Walombo huwakanya kabisa walichiputu kwamba ni mwiko kabisa kwa kabila lao kumkataa mwanaume anayetarajia kuwaoa. Hivi itawapasa wanawali kuwakirimu wale wote ambao wameonyesha dalili halisi ya kutaka kuwaposa. Walombo huiga pia kazi zifanywazo na wanaume, kama vile kuwinda wanyama kwa nyavu hufanyika ikiwa ni moja ya shabaha ya kuwafundisha mambo fulani fulani ya maisha ambayo watayakabili siku za usoni. Maisha ni kama mtego wa panya, huwanasa waliokuwemo na wasiokuwemo.

Michezo ya kila namna huendeshwa katika kuwapa mwongozo wale walichiputu. Kwa mfano nnombo mmoja hujisingizia kuwa ni mwindaji wa wanyama wa porini na mmojawapo hujifanya kuwa ni mnyama anayewindwa. Hatimaye yule aliyejifanya ni mnyama hunaswa katika nyavu na haraka wawindaji humfunga nguo gubigubi ili wale walichipitu wasigundue ujanja wenyewe. Yote haya hufanyika wakati wa usiku ati! Haya yana shabaha ya kuwatahadharisha kwamba wao watawindwa, na wasipojitunza sawa sawa watanaswa kirahisi katika nyavu za maisha ya kimatatizo. Kwa maneno mengine walichiputu hutahadharishwa kuwa, kwa desturi wanawake wanawindwa na wanaume. Hivyo hawana budi wasimezwe na wanyama wakali (wanaume wakware).

Wanawali yawapasa kuwa waangalifu katika kuwachagua wanaume wenye utu vinginevyo watakabiliwa na mikasa na mateso kutoka kwa wanaume waliowapata kwa pupa. Kwa hiyo yawapasa wawe na ujasiri.
Watakaporudi makwao watakuwa wamekweisha hitimu kwa kutayarishwa katika uadilifu, heshima, ukarimu, wenye bidii ya kazi, ujuzi wa kuwalea watoto na missingi ya mila za kabila. Inapotokea kwa bahati mbaya mmoja wa walichiputu anagunduliwa kuwa hana ubikira, Bi, mkubwa humwita mama ya Mwalichiputu ambaye amegunduliwa. Bi, mkubwa humwuliza mzazi juu ya tbia na mwenendo wa binti yake. Kadiri anavyoeleza mamake huchukuliwa kuwa ni ushahidi murua. Mara nyingi mama wazazi wanauficha ukweli wa mambo yalivyokuwa kwa ajili ya kuogopa aibu ambayo ingewaandama.

Mafunzo huendeshwa na tafrija za kila aina ambazo hufanywa kila mara baada ya kufikia hatua fulani ya mafunzo yao. Baada ya kuhitimu wanarejea makwao ambako itawabidi kuendelea na mazoezi ambayo ni muhimu kwa muda fulani unaopangwa. Daima walichiputu huwa chini ya ulinzi maalum wawapo nyumbani kwa kipindi hiki cha matazamio.

Baada ya kipindi cha matazamio kupita, walichiputu hukusanywa tena kwenye inande yanole ili kumaliza unyago wao. Mazoezi yale yale hukaririwa ili mradi kila mmoja awe wamefaulu kuufikia ujuzi utakiwao. Hukamilishwa kwa kufundishwa mambo mbalimbali ya lazima ya kila siku ambayo kila mwanamke yambidi kuyatekeleza. Hatimaye huogeshwa maji na kuvishwa nguo mpya dinjalukilo baada ya kupakwa mafuta ya mbariki. Sherehe kubwa hufanywa, ngoma za aina mbalimbali huchezwa hasa zile za vinyago, pombe hunywewa na maakuli ya aina aina huandaliwa.

Asubuhi ya siku inayofuata wanawali hutembezwa mahali mbalimbali kwa mfano, kisimani, shambani, mahali pa kupikia pombe ili waelimishwe juu ya madaraka wategemeayo kuyamudu baada ya muda si mrefu katika maisha yao………………

Kesho nitawaletea namna ya kumchumbia Binti wa Kimakonde-Hii itakuwa ni kwa wanaume tu.


 
Wacha vitisho wewe Zinduna, hayo ni malove-malove tu. Labda wanaume wa Kimakonde ndio watakaotishwa na mkwala wako.
Ibrah, wewe subiri joto ya jiwe tu!
 
Last edited by a moderator:
Zinduna nipo shost, si unajua tena mambo ya mkate yamenichukulia muda hasa ukizingatia ni J3, Nimeona ya kimakonde nikitulia ntakuletea ya kimanyema na kitusi ili kukazia.
 
Last edited by a moderator:
Mbona wanawake hawachangii huu uzi jamani,
Nitawaambia MODS wauondoe kama hamtaki kuchangia.....EBO! Cantalisia , Preta , King'asti , Kipipi Asnam TaiJike MwanajamiiOne , na wengineo mko wapiiii!

Hao wote uliowaorodhesha ni ANAHAKU. Lizzy peke yake ndio kifaa.

Na kuhusu mkwara wako hapa umenoa, majipu tayari ninayo, tena makubwa ya haja. Ukitaka naweza kukuruhusu uone yanavyoning'inia chini ya filimbi shaka hayana
 
hahaha Zinduna Jtatu tunakuwa busy ..
Ngoja nisome nitauchangia huu uzi mida ya usiku akili imekaa powah..
Ila kuna mambo itabidi unitumie PM kwa maswali zaidi
 
Back
Top Bottom