Wasokuwa na upande wowote KISIASA = WAKWELI

Mwambonalgw

New Member
Nov 29, 2011
2
0
Wanasiasa wote wana lengo la vyama vyao na mitizamo yao.
Jamii forum iwe na kipengele cha kuwakosoa na kuwashauri wanasiasa hata wanajamii forum wenyewe.
Kiongozi au mwanasiasa asiyekubali kukosolewa hatufai LAKINI anakosolewa na nani ?
Mimi naona ni vizuri kuwapo na chombo hiki hata katika jamii, kinachoweza kusema kwa busara na ukweli.
 
Ni kweli mkuu... ila kichwa cha mada kimenifanya nijiulize mengi.....
Wasokuwa na upande wowote KISIASA. = WAKWELI
Wanaokuwa na upande wowote KISIASA. = WAONGO??

Ni kweli kwani ushabiki wa vyama unatuziba macho....... hatuoni mabaya yanayofanywa na vyama vyetu.......na tunajaribu kuyafanya mazuri ya wapinzani wetu yaonekane mabaya......
 
Bila shaka mkuu!ila mi naona wasio na chama ndio wanaotuangusha wote tusimame pamoja kutetea nchi na raslimali zetu maana hawa wanasiasa wengine wanaweza kuuza hata wake zetu!
 
Hapo mwanzo enzi za jambo forums kwakweli JF ilikuwa ni kama chombo huru kukosoa na kupongeza chama au kiongozi yeyote kwa jema au baya kwa hoja na fikra huru kabisa

Now days Jf si chombo huru tena cha kukosoa wanasiasa isipokuwa kusifia fulani na kuponda vyama vingine,imekuwa ni kama chama fulani ndio kina hati miliki na kuamua nini kijadiliwe humu.

Leo hii huitaji uGT wowote kuanzisha uzi unachotakiwa ni kusema baya lolote la chama fulani na kukitetea chama kingine hata kwa matusi inatosha kabisa kukufanya GT wa ukweli,
Ni ukweli usiopingika kuwa ingawa wapenzi wa chama fulani wapo wengi humu lakini hii si sababu ya kutusi watu wanaokosoa chama hicho wa si sababu ya kupinga jema la cha kingine, kinachojali ni hoja ya mleta hoja ijibiwe kwa hoja na si matusi na kejeli

Leo hii kuitwa msaliti,umetumwa,masaburi,kilaza nk nk na kuporomoshewa matusi kwasababu tu umekosoa chama fulani humu JF ni kama sheria, watu wametokwa na busara na kuingiwa na upofu wa mapenzi ya vyama vyao na kuwaona viongozi wao ni miungu watu wasiostahiki kuhojiwa wala kukosolewa kwa lolote

Hata hivyo bado tupo wachache ambao tunaamini katika kutoa mawazo huru na tunafanya hivyo tukiamini JF ni uwanja huru kukosoana bila kujali chama gani na kupongeza bila kujali itikadi za vyama

Naamini madhumuno ya JF ni kama hayo unayoyasema mleta mada lakini sasa hali imekuwa sivyo ndivyo, cha muhimu tetea kile unacho amini kwa hoja na si viroja na kejeli
 
Nakuunga mkono.
Watu wanatetea vyama vyao na kuponda vingine bila kuangalia ukweli wa mambo, imefikia mahali mtu akizungumzia mapungufu ya chama fulani hapa jf basi ataishia kupata dhihaka hata kama alichozungumza kina ukweli.
Kwa upande mwingine mtu akikisifia chama "...", ataonekana anaakili na atapongezwa hata kama ameongea pumba.
 
Ni sawa lakini naona kama tumeshachelewa wachache sana wanaweza kutoa mawazo yao pasipo kuwa na mlengo. Kingine, wakati mwingine unaweza kushangaa mtu anayejiona au kuleta mada as if yuko independent ukisoma KATIKATI YA MISTARI unaona hila ndani yake.............................Kimsingi kuna mamluki pia kwenye msafara!
 
Back
Top Bottom