Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,515
- 6,489
Kwa jinsi ninavyosoma kwenye vyombo vya habari (sijawahi hudhuria mahakamani), na kama kweli ndivyo ilivyo, nina wasiwasi ubunge wa Mnyika- Ubungo nao utatenguliwa. Sio kwa rushwa, matusi au kuiba kura ila kwa ushahidi uliotolewa mahakamani na aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi husika, na ushahidi ambao haujapingwa na upande wa Mnyika kuwa kuna kura kumi na nne elfu (14000) ambazo ni hewa na haijulikani ziliingiaje, japo ya kwamba Mnyika alimzidi mpinzani wake kwa kura 15000.