Wasira aingilia mzozo wa polisi, waandishi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAZIRI katika ofisi ya Rais Kuratibu Uhusiano na Jamii, Steven Wasira amemshauri Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye kumaliza tatizo la waandishi wa habari kupigwa na kuharibiwa mali zao na askari polisi katika maandamano ya wafuasi wa Chadema ya Januari 5 mwaka huu.

Wasira alisema hayo juzi mjini Arusha katika kikao cha pamoja cha Maaskofu, watumishi wa Jiji la Arusha, wakuu wa Wilaya, Polisi na Maofisa Usalama wa taifa.

Wasira alisema hayo baada ya mwandishi wa Abood Media kanda ya Kaskazini Fortunatus Ruta kutaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu kitendo cha Polisi kuwakamata na kuwasweka ndani waandishi waliokuwa kazini siku ya tukio na kuharibiwa vifaa vyao vya kazi.

Alisema “vita havina macho, lakini kitendo hicho si kizuri hivyo RPC unatakiwa kukaa na waandishi wa habari kumaliza tatizo la kuharibiwa mali zao,” alisema Wasira.

Akifanya majumuisho ya mazungumzo na Maaskofu juu ya sakata la mauaji ya Vijana watatu na uchaguzi wa Meya, Wasira alisisitiza kuwa tatizo la kanuni humalizwa kwa kanuni na uchaguzi wa meya hauwezi kurudiwa kama Chadema wanavyodai bali wananchi wanatakiwa watulie na kuijenga nchi kwa kuwa uchaguzi huo si wa mwisho wajiandae kwa uchaguzi ujao.

Alisema hata kama uchaguzi ukirudiwa Chadema hawawezi kushinda kwa kuwa CCM ina viti (16) na Chadema ina viti (14), lakini muda wote wa tamko la Waziri huyo Maaskofu hao
akiwemo Askofu Thomas Laizer (KKKT), Askofu Josephat Lebulu na kiongozi wa madhehebu ya Kikristo mkoani Arusha Mchungaji Kimaro walikaa kimya bila kuzungumza lolote.

Hata baada ya kikao hicho hakuna kiongozi wa dini aliyekuwa tayari kufuta kauli yao ya
kutoutambua uchaguzi wa meya uliomweka madarakani Gaudence Lyimo wa CCM.


HabariLeo | Wasira aingilia mzozo wa polisi, waandishi
 
Anyone who seeks to destroy the passions instead of controlling them is trying to play the angel. Wasira is attempting to play an angel!
 
Back
Top Bottom