Wasipokaa vizuri CHADEMA, jimbo la Sumbawanga mjini wanaweza kulipoteza!

Kama kigezo cha kupendwa ni kupeta kwenye uchaguzi wa magamba (NEC), huko wagombea waliopitishwa walitegemezwa na fungu kubwa la rushwa na Aeshy anapendwa kwa mulungula si vingevyo. Lakini kumbuka mulungula ndio uliomng'o ubunge na bado hakomi.
 
Wakisimamisha mtu tofauti na Aeshi wanaweza kuleta upinzani, lakini kwa sasa sioni mtu ndani ya CCM hapa Sumbawanga anayeweza kuleta upinzani kwa CDM.

Katavi,
Naona unajiachia uwanja wa nyumbani.
 
Last edited by a moderator:
MAkinda, Tume ya Uchaguzi inasubiri sadaka na ruhusa toka kwa mkuu wa Magamba ndo uchaguzi usifanyike maaana ni noumer tu.
 
Naöna kwa kiasi fulani uko sahihi, cdm kwa kiasi fulani wameanza kuonyesha dalili ya kuridhika chukulia mfano jimbo la igunga, ccm wameenda mara nyingi baada ya mbunge wao kuvuliwa ubunge, lakini cdm wametulia tu, haya sumbawanga nako akina nape wameenda, cdm mmh! Angalia hata hicho kinachoitwa m4c, mikoa kama kigoma, rukwa, tanga, hakuna! Cdm inabidi wafanye kazi usiku na mchana kwa sababu wao si chama tawala ni chama kinachodhamiria kushika dola, kwa hiyo wasijifananishe na ccm!
Mkuu huko kujipitishapitisha hakuongezi chochote kama huna hoja za msingi kwa wananchi,na zaidi ni kupoteza muda, pesa au kuongeza kuchukiwa na wananchi kama wamekuchoka.

Nitakupa mifano ambayo ni dhahiri tumeishuhudia;

1/Kwa miaka mitatu mfululizo(2007-2010) CCM ilijipitishapitisha jimbo la Moshi mjini tena kwa pesa mingi, pia wakiweka Zonal camp ya makada kibao huku wakisuka mipango na kumwaga propaganda za kutaka kumn'goa Ndesamburo lakini cha moto walikiona na hawatarudia tena (Ubunge ulibaki Chadema na Baraza la madiwani kwa mara ya kwanza likaongozwa na Chadema)

2/CUF kwa kupitia Mtatiro baada ya kuweka kambi Igunga walifanya kama hayo kwa zaidi ya siku 40 mfululizo kabla ya kuanza rasmi kampeni za uchaguzi wa Igunga, lakini waliishia kuambulia kura 2000 toka kwenye mtaji wao wa kura 10000 walizopata 2010.

3/Kule Arumeru Mashariki CCM ikiongozwa na Mwiguru Mchemba iliweka kambi na ilifanya hicho hicho kwa zaidi ya siku30 mfululizo na kutumia zaidi ya milioni 300 kabla ya kuanza rasmi kampeni, lakini mwisho wa siku wakaishia kupoteza jimbo muhimu ambalo lilikuwa ni ngome yao.

*Hivyo mkuu ni bora ukaja ground field ukaona na kucheza mchezo wenyewe na sio kubaki kwenye keyboard kuchungulia tu.

*Tunaposema wananchi wameichoka CCM tunauhakika na ukweli halisi tunauona huku chini.
 
Uchaguzi wenyewe lini sasa...??
Kwa kawaida kisheria uchaguzi unatakiwa kurudiwa ndani ya siku 60 toka siku imetangazwa jimbo kuwa wazi na tume ya uchaguzi.

Kwa issue ya Sumbawanga mjini kuna utata, mara baada ya mahakama kuu kutengua Ubunge wa Aeshi, alipewa nafasi ya kukata rufaa, mara ya mwisho (Zaidi ya mwezi umepita sasa) alipo ulizwa kama amekata rufaa yeye mwenyewe(Aeshi) na CCM(Nape) alisema hapana na wakati huo muda wa kukata rufaa ulikuwa umeshapita!!

*Ni kazi ya mahakama kulitaarifu bunge kama jimbo liko wazi kisha spika kuutangazia umma na kuitarifu tume ya uchaguzi.
Hivyo hapo tume ya uchaguzi ndio itatakiwa kutangaza rasmi jimbo lipo wazi na uchaguzi utatakiwa kufanyika ndani ya siku 60.

*Ufafanuzi kutoka ofisi ya spika(ulitolewa mwezi mmoja uliopita) kupitia Naibu spika Ndugai ilisema suala hilo lina utata na atatoa tamko kwenye kikao cha bunge mwezi huu wa Oktoba.
 
Mimi wasiwasi wangu 2015 ni Iringa Mjini.Kweli sificha wasiwasi Manake na hisi kuna kazi ya ziada.
 
hivi wewe kwani.nec ni ubunge au hujui kuwa walomchagua ni haohao magamba.kwavovote vile kama wanafaidika nae lazima apite tu.nauliza hivi hayo maeneo uliomkuta si maeneo yenye msemo musemao"shina la wakereketwa wa chama cha mapinduzu"
 
Naöna kwa kiasi fulani uko sahihi, CDM kwa kiasi fulani wameanza kuonyesha dalili ya kuridhika chukulia mfano jimbo la igunga, CCM wameenda mara nyingi baada ya mbunge wao kuvuliwa ubunge, lakini cdm wametulia tu, haya sumbawanga nako akina nape wameenda, CDM mmh!

Angalia hata hicho kinachoitwa M4C, mikoa kama kigoma, rukwa, tanga, hakuna! CDM inabidi wafanye kazi usiku na mchana kwa sababu wao si chama tawala ni chama kinachodhamiria kushika dola, kwa hiyo wasijifananishe na CCM!

Hapo kwenye red mkuu umepotoka, Slaa na Kasulumbai walifika pale siku moja baada ya hukumu kuwashukuru wananchi kwa michango yao iliyofanikisha ushindi wa kesi, na mkutano ulifurika watu ile mbaya, Slaa alichepuka tokea Morogoro ambako mikutano ya M4C ilikuwa ikiendelea
 
Sijajua mtoa mada ana lengo gani...Aeshi hata akigombea yeye na chama kingine kama tlp kamwe hawezi shinda.....usipende kuleta mada kishabiki shabik usokua na mpango...
 
Nyie wenzangu mmemuelewa mtoa mada alikuwa anajaribu kusema nn?MM nimerudia tena na tena kuisoma habari yake hii lkn sijaona any rationale aliyojaribu kutuambia!

Nisadieni tafadhali mtoa mada alijaribu kutupasha nn?
 
Mleta uzi huu ni mwongo na mnafiki.mi nimekaa sumbawanga mjini toka aeshi kavuliwa ubunge na nina wiki 1 tu toka nimeondoka.vijiwe vipi huyo aeshi anaongea na vijana?hata kile kijiwe cha tax pale kwa sumry hawamtaki.aeshi amekuwa mtu wa kugawa bia kila weekend pale greenview bar kantalamba na baa nyingine kibao.
 
Bado rufaa haijasikilizwa, kwa hiyo tarehe ya uchaguzi bado.

Mkuu, CCM hawakukata rufaa na muda ulishapita, ni kama issue ya Igunga hadi sasa hawajakata rufaa na sidhani kama watakata rufaa tena Igunga
 
Wadau asalam aleykum?

Mi kama mpenda demokrasia hapa Tanzania kwa sasa nikiwa Sumbawanga, naona kuna mbinu chafu anaziandaa Aeshi Khalfan Hilary i.e CCM kuweza kutetea kiti chao.

Nasema hivi kwa sababu naonana na Aeshi mara nyingi na THE WAY ALIVYO 'SOCIAL' kwa watu na jinsi vijana wanavyomkubali compared to Yamsebo Norbet wa CHADEMA. Mi nilijua wengi hawamtaki kutokana na kesi iliyomvua ubunge. DAH! Kwenye uchaguzi wa NEC alipita kwa kishindo kikubwa.

SO CHADEMA KAZI KWETU!

Unasahau kama kule NEC tunachaguana sisi kwa sisiem ! so, the kishindo that you are trying to tell is the kishindo within the party !
 
Ukipokea kila ushauri, utakuwa mjinga!! Huu ushauri una uzuri gani? Mtu kamwona jamaa anacheka na watu kwenye kikao cha kahawa anampa ushindi kwenye jimbo!! Ubunge ungekuwa hivyo, me ningeshinda bila kampeni!

Nakubaliana na wewe lakini huyu yuko kwenye eneo husika na kwa hivyo anajua kinachoendelea, kwa taarifa tu ndugu yangu nguvu ya chadema inaanzia kwenye hivyo vijiwe unavyovidharau na kwa nnavyofahamu yamsebo ni mtu mzima kwenye 50-65 wakati wa ccm ni below 50.
Kama huyu wa ccm anajichanganya na vijana kuliko wa chadema ana nafasi nzuri ya kushinda kama mwenzake hatachangamka..maoni tu
 
Mfalme Daud,
Unapima upepo nini? Waambie wajaribu na Mgamba yao waone Sumbawanga ilivyo ilivyo moto na Chadema.Wanaombeba Aeshi ni wale vijana wachovu.Niwale hapo awali walionunuliwa kadi za Magamba na kumpitisha kama mgombea wao na dio waliompa U-Nec unaousema.Jaribu maeneo yote sasa yamebadilika na wanauelewa mkubwa juu ya siasa.Acgha mchezo kabisa huku!!!!!!!!!!!!!
 
Wadau asalam aleykum?

Mi kama mpenda demokrasia hapa Tanzania kwa sasa nikiwa Sumbawanga, naona kuna mbinu chafu anaziandaa Aeshi Khalfan Hilary i.e CCM kuweza kutetea kiti chao.

Nasema hivi kwa sababu naonana na Aeshi mara nyingi na THE WAY ALIVYO 'SOCIAL' kwa watu na jinsi vijana wanavyomkubali compared to Yamsebo Norbet wa CHADEMA. Mi nilijua wengi hawamtaki kutokana na kesi iliyomvua ubunge. DAH! Kwenye uchaguzi wa NEC alipita kwa kishindo kikubwa.

SO CHADEMA KAZI KWETU!
Kwani Mkuu, CDM Nao walipiga kura kwenye hiyo NEC????
 
Hapa Sumbawanga mjini hata kama CCM watamsimamisha Pinda na CHADEMA wakamsimamisha mtu yoyote yule(hata kichaa anaye okota makopo hapa mjini) bado nina uhakika Chadema itashinda tu.

Sababu kuu ni kwamba CCM haipendwi kabisa kabisa lakini pia kitendo cha kuchakachua matokeo mwaka 2010 kiliwaudhi watu wengi sana na mwisho kauli na vitendo vya kimaudhi(kiutu na kiimani)alivyofanya Aeshi mwaka 2010.

Na kwa taarifa yako CCM kwa sasa wanaumiza kichwa sana juu ya nani wa kumsimamisha kugombea kama uchaguzi utatangazwa kurudiwa kwani huyo Aeshi anatafsiliwa vibaya sana na viongozi wa juu wa chama kutokana na matukio fulani fulani ambayo yamekipa chama wakati mgumu sana.

Halafu wewe mleta mada ni mzushi sana, huyu Aishe japokuwa ni kijana na mtu mwenye pesa lakini hana tabia kabisa ya kujichanganya na watu wa kawaida zaidi sana anaonekana bar na night club akikamua pombe na malaya tu, kama kuna mtu anabisha aje hapa Sumbawanga mjini ajionee mwenyewe.

nimependa "hupenda kwenda night club na kujichanganya na malaya" kumbe hadi swanga kuna night club za kutosha tz imeshaendelea bana!
 
Back
Top Bottom