Wasiotaka Muungano wasikilizwe - Sheikh Mkuu

Mufti wa Tanzania, sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba, kilichotikea Zanzibar ni mambo ya siasa hivyo basi kama kuna Wanzanzibari hawautaki muungano wanastahili kusikilizwa ili kuepusha balaa.
Chanzo: Gazeti la Nipashe la leo
Nilitegemea Sheikh mkuu angekuwa na uwezo wa kuona kuwa vurugu zinazojitokeza Zanzibar si kwasababu kuna watu hawataki muungano bali ni kwasababu kuna kikundi cha waislam wanaochukia wakristo kwahiyo wanatumia nafasi ya kupinga muungano kueneza chuki na kutekeleza hujuma zao. Kama umebahatika kusikiliza mahubiri ya hawa wana uamsho utaweza kujua kwamba swala hili halijatokea kwa bahati mbaya, ni maandalizi ya siku nyingi. Uzuri mahubiri yao yanapatikana katika CD na DVD.
Inasikitisha kuona kiongozi wa dini akitoa tamko kama hili wakati mgogoro wa Zanzibar si kuhusu muungano bali ni juu ya kikundi kisichopenda wakristu ambacho kinatumia kisingizio cha muungano kuharibu makanisa ya wakristu.
Kama tatizo ni muungano kwanini waandamanaji hawakwenda kuchoma ofisi za serekali ya muungano?
Makanisa yamekuwepo Zanzibar kabla ya muungano. Kanisa la kwanza Afrika mashariki lilijengwa Zanzibar. Kipindi hicho Muarabu aliyeleta uislam Zazibar akiwa bado yupo, na hayakuchomwa moto.
Sasa leo hii haiingii akilini kwamba Muungano unapingwa kwa njia ya kuchoma makanisa ambayo yalikuwepo kabla ya muungano.
 
Back
Top Bottom