Wasiomjua Dr. Slaa soma mada hii, kabla ya uanasiasa na baada

Mbona unaeleza vitu nusu nusu mkuu, ujasema kama Dr Slaa ana wake wawili ujasema Dr ana watoto wa ngapi ebu tufahamishe, umetaja mambo ya kanisa tu.

Kuna anayejua kama Ritz ana mke, watoto au ana kimada? Jibu hapana, tunachojadili mada zinazohusu shughuli za kisiasa, mambo binafsi ya kifamilia tunawaachia wenyewe, hayatuhusu.
 
Mkuu pandisha kiwango tujadili mada; ni afadhali ya mbichi zinalika hizi zimevunda na kuoza kabisa; mkuu tunakula vitu FDA approved hivi vya majalalani hata Matonya (R.I.P) vilimshinda.

Chama
Gongo la mboto DSM

Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM, baada ya kuombwa na Wanakaratu agombee ubunge kule baada ya kuchoshwa na mbunge aliyekuwepo wakati huo, CCM iliendelea na mizengwe ile ile kama iliyotokea juzi pale Dodoma kuwaengua watu wanaofaa kwa uongozi. Wanakaratu wakiamua hawataki longolongo, wakamsihi kwamba wameamua awe mbunge wao na wakamwomba achague chama kingine agombee kwani hawamtaki kabisa mbunge aliyepo. Kwa ridhaa ya wananchi akaamua kujitoa CCM na kujitosa kujiunga na Chadema ili agombee ubunge kuridhia matakwa ya wanakaratu.

chama hii paragraph inakucheua, maana inagusa jipu lililoiva karibu kupasuka, wanifurahisha sana Chama/Gongolamboto leo.
 
Kuna anayejua kama Ritz ana mke, watoto au ana kimada? Jibu hapana, tunachojadili mada zinazohusu shughuli za kisiasa, mambo binafsi ya kifamilia tunawaachia wenyewe, hayatuhusu.

Ndio maana nakuambia usilete habari nusu mie sio kiongozi wa kisiasa uwezi kunifananisha na Dr Slaa, mkuu kiongozi ni kioo cha jamii wananchi wanatakiwa wamfahamu kwa undani wasije kuongozwa na mtu ambaye sio makini...ukishaamua kuwa mwanasiasa ni lazima watu ambao unataka kuwaongoza wakufahamu kiundani.
 
Mtoa uzi kwa uchambuzi wako umeonyesha kuwa Dr Slaa ni mzuri sana katika kubuni mambo na kuyasimamia.Hii inadhihirisha pia kwenye siasa jinsi anavyoonyesha umahiri na kipaji chake cha uongo na uzushi.Bado TEC inahitaji utumishi wake arudi akajenge kanisa na taasisi zake kwani siasa inamtupa mkono.
 
Ndio maana nakuambia usilete habari nusu mie sio kiongozi wa kisiasa wala, mkuu kiongozi ni kioo cha jamii wananchi wanatakiwa wamfahamu kwa undani wasije kuongozwa na mtu ambaye sio makini...ukishaamua kuwa mwanasiasa ni lazima watu ambao unataka kuwaongoza wakufahamu.

Kwako kuona ni habari nusu nusu ni kwa mtazamo wako tu, lakini wachangiaji wengi wameielewa na kuiona imekamilika.

Ritz mimi sikijui, ninachokijua kuhusu mtu huyu ndicho kilichokiandia. Kwa bahati nzuri hapa ni uwanja unaofanana na kijumbe kile kwenye kilima cha Aleopago kule Ugiriki wanafalsafa maarufu kama Socrates, Aristatle na wenzake walijifunzia kutoka kwa wazee mahiri na baadaye kuja kuwa mahiri wa kimataifa kwa sababu ya ustahimilivu na usikivu wao kwa wazee wale wazoefu kwa falsafa.

Saa Riz hicho unachoniulizia ambacho mimi sikijui ndichouchangie hapa. Thanks.
 
Mtoa uzi kwa uchambuzi wako umeonyesha kuwa Dr Slaa ni mzuri sana katika kubuni mambo na kuyasimamia.Hii inadhihirisha pia kwenye siasa jinsi anavyoonyesha umahiri na kipaji chake cha uongo na uzushi.Bado TEC inahitaji utumishi wake arudi akajenge kanisa na taasisi zake kwani siasa inamtupa mkono.

Umesikia au uliulizia kama TEC wanamhitaji?
Kwani aliyoyaanzisha wameshindwa kuyaendesha?
Hutaki afanya hayo kwa taifa ili vijana tuje kuyaendesha kwa ufanisi zaidi baada ya kutuonyesha njia kama alivyofanya TEC?
Au haya niliyoonyesha yanaanza kuwaogopesha waliodhani hana back ground ya ubunifu katika maendeleo?
 
Kila kinachochangiwa lazima kiwe kizuri tuu.Msisahau yeye pia ni binadamu ana mapungufu yake
 
Huu upuuzi mbona haueleweki molemo na timu jipangeni upya mnaleta mada kama vile mnawapelekea wanafunzi wa vichechekea

Chama
Gongo la mboto DSM
Mimi nafikiri ni vizuri wameleta upande mzuri wa Dr Slaa

Ule upande mwingine vipi, maisha yake yakoje na familia?

Mtu haindi ikulu peke yake, ana familia, tupeni mapambano yake ya kutoka upadiri, maisha ya ndoa , na hata maadui aliojitengenezea katika kubadili CV yake kimaishs.
 
Umesikia au uliulizia kama TEC wanamhitaji?
Kwani aliyoyaanzisha wameshindwa kuyaendesha?
Hutaki afanya hayo kwa taifa ili vijana tuje kuyaendesha kwa ufanisi zaidi baada ya kutuonyesha njia kama alivyofanya TEC?
Au haya niliyoonyesha yanaanza kuwaogopesha waliodhani hana back ground ya ubunifu katika maendeleo?

Hana sifa,muflisi.
 
Candid Scope,
Unasema wachangiaji wengi wamekuelewa na kuona bandiko lako limekamilika sababu hawakuhoji Dr Slaa ana watoto wa ngapi na ameishaoa..

Sawa mkuu naona unachagua mazuri na kuyapamba na yale ambao utaki kuyasikia kuhusu Dr Slaa, utaki kuyajadili.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nafikiri ni vizuri wameleta upande mzuri wa Dr Slaa

Ule upande mwingine vipi, maisha yake yakoje na familia?

Mtu haindi ikulu peke yake, ana familia, tupeni mapambano yake ya kutoka upadiri, maisha ya ndoa , na hata maadui aliojitengenezea katika kubadili CV yake kimaishs.

Ndiyo sababu nimemuomba candid scope apandishe kiwango tujadili mada

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Candid Scope,
Unasema wachangiaji wengi wamekuelewa na kuona bandiko lako limekamilika sababu hawakuhoji Dr Slaa ana watoto wa ngapi na ameishaoa..

Sawa mkuu naona unachagua mazuri na kuyapamba na yale ambao utaki kuyasikia kuhusu Dr Slaa, utaki kuyajadili.

Hoja zako kuhusu mambo binafsi ndani ya familia yake mimi hayanihusu na siyajui kwa vile siishi ndani ya familia yake. Ninayoandika na kuyajua yale anayofanya katika jamii ya watu wanaomzunguka na taifa ambalo yanaonekana. Ndani ya nyumba kama anasaidia kuosha vyombo na kubadilisha nepi ya mtoto au la hayo siyajui kwa vile siidhi naye.
 
Mtoa uzi kwa uchambuzi wako umeonyesha kuwa Dr Slaa ni mzuri sana katika kubuni mambo na kuyasimamia.Hii inadhihirisha pia kwenye siasa jinsi anavyoonyesha umahiri na kipaji chake cha uongo na uzushi.Bado TEC inahitaji utumishi wake arudi akajenge kanisa na taasisi zake kwani siasa inamtupa mkono.

Pole..
 
Back
Top Bottom