Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,342
- 6,468
Mungu kamuumbia kila mtu wa kwake,ila hatuamini tu,tunakurupuka hatuombi kwa kumaanisha
Kwa sisi RC, ndoa ni sakramenti na kuna sakramenti nyingine kama upadre ambazo huwezi kuwa nazo kwa wakati mmoja (lazima uwe na mojawapo). Sasa ni Mungu tu anatupangia hizi sakramenti aidha ndoa au upadre. Na pia kuna masista wakifunga nadhiri ya maisha hawatakiwi kuolewa.
Tatizo linakuja wanawake (RC) wanasahau kuwa ndoa ni sakramenti na sio fashion. Pia wanasahau lengo la ndoa kama Mungu alivyosema na kuanza kuwa na malengo tofauti kama kutaka mume mwenye pesa/ mali nyingi, kabila fulani, ukoo wenye jina kubwa vitu ambavyo ni rahisi kwa mwanamke kuachwa kwenye mataa.
Pia wanawake waelewe kuwa wanajukumu kubwa la kushawishi kuolewa na sio tu kukaa kimya na kusubiri mwanaume aseme nataka kukuoa - ni lazima kumkumbusha huyo rafiki yako wa kiume. Na mnapoanza mahusiano lazima mwanzo kabisa muulizane hivi ni kwa nini mna hayo mahusiano ya kimapenzi na mwisho wake ni nini? je, ni lifetime relationship au just for pleasure au short term - hit and run? Na mwisho ni kuwa na tabia njema - hivi mwanamke kila siku ana bwana tofauti, lugha chafu, muda wote yuko bar, ofisini board members wote wa kiume wamekwisha chapa, too demanding - kila fashion anataka; kuolewa ni bahata sana, na ndoa kudumu pia ni bahati sana.
Marafiki nao wanachangia wanawake kutokuolewa, mfano hai, mwanamke anamwambia rafiki yake nimepata mchumba, rafiki yake anamwuliza huyo jamaa ana-drive, anafanya kazi ya 'white collar, senior officer sehemu fulani au blue collar. Halafu anamwambia tafuta spare tyre kwani huyo akikuacha unakuwa na mwingine. Sasa ukitafuta spare tyre halafu yule mwenye nia ya kweli akagundua unategemea nini kitokee kama sio jamaa kutokutokea siku ya ndoa!!!
Pia tujiulize, je wanaume wote wameoa ukitoa mapadre, mabruda na matoashi?
Pia walioachika wafanyeje?!!
Hapa nimejaribu ku-unpack alichosema Gaga though not very sure!!