Wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga wametakiwa kuzingatia unyeti wa jukumu la kusimami

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,836
Wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la kalenga wametakiwa kuzingatia unyeti wa jukumu la kusimamia uchaguzi,kuzingatia katiba,sheria,kanuni na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi kikamilifu ili kudhihilisha demokrasia na kuepusha malalamiko yasiyo ya msingi.

Hayo yamesemwa leo katika ufunguzi wa semina ya mafunzo ya msimamizi wa uchaguzi,wasimamizi wasaidizi ngazi ya jimbo na kata ya jimbo la kalenga pamoja na wandishi wa habari na mkuu wa wilaya ya Iringa RETISIA WALIOBA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa siasa na kilimo uliopo manispaa ya Iringa.

Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya tume ya uchaguzi mawakala wa vyama vya siasa hawapaswi kuwepo katika vituo vya kupigia kura jambo ambalo litasaidia kudhihirisha uwazi katika zoezi zima la uchaguzi.

Amesema kuwa wajibu wa mawakala wa vyama vya siasa ni kuangalia sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa na tume zinazingatiwa katika mchakato wa kupiga kura hadi wakati wa kutangaza matokeo.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wahamasishwe na elimu ya kutosha itolewe kwa wapiga kura wote huku akitoa wito kwa wananchi kujiandaa kwa ajiri ya uchaguzi na kuhakikisha wanatunza kadi za kupigia kura na wajiepushe kurubuniwa kwa namna yoyote ili wasiweze kupiga kura.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi inaendesha program ya elimu ya mpiga kura ambapo mabango,vipeperushi na matangazo kwa kutumia vyombo vya habari huku akiwataka wasimamizi kutopendelea chama chochote wala kuonesha ushabiki wa chama chake bali watumie demokrasia.

Akitoa ratiba ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi PUNDENCIANA KISAKA amesema kuwa muda wa kuanza kuchukua fomu ni kuanzia tarehe 9 hadi 18 na kufanyika kwa uteuzi kabla ya saa kumi,kampeni zitaanza tarhe 19 hadi 15 mwezi wa tatu na upigaji kura utafanyika tarehe 16 mwezi wa tatu .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom