Wasifu wa marehemu usio wa kinafki

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi akainuka na kuanza kusema ‘kinachofuata sasa ndugu wafiwa na marafiki wa marehemu ni kusoma historia fupi ya marehemu tuliyemzika hapa leo, karibu ndugu uliyeandaliwa kwa shughuli hiyo’

Msomaji aliyeandaliwa alianza kusoma ‘Ifuatayo ni historia fupi ya marehemu tuliyemlaza ktk nyumba ya milele.
Marehemu alizaliwa juu ya mti amb
apo mzazi wake alijihifadhi baada ya kukimbia mafuriko miaka 26 iliyopita.

Hakubahatika kupata kazi ya maana japo alisoma mpaka kidato cha tano, aliamua kuacha shule mwaka juzi baada ya kuona elimu haina mpango kwake.

Marehemu alikuwa kero kwa familia yake hasa kwa tabia yake chafu ya udokozi wa mboga, uongo, uvutaji bangi, ubakaji wa mifugo na baadae ushoga.

Mimi binafsi mjomba wake nimefurahishwa sana na kifo cha marehemu huyu kwani alishawahi kunipakazia kuwa nimekufa mara mbili kiasi na kufanya ndugu wote wakakusanyika na kunililia msiba.

Mtoto alitutia hasara sana kwani alikuwa mwizi wa vitu vya ndani na pesa! pia tumepoteza gharama kibao kumsomesha lakini aliishia kuwa shoga tangu tarehe 06/04/99.

Marehemu hakuugua bali kifo chake ni cha kujitakia kwani kajiua baada ya kukosa nauli ya kwenda Mombasa kuhudhuria onyesho la vikundi vitatu vya mduara. Kwa niaba ya familia, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu tunatoa pongezi za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kutupunguzia kero na asiilaze roho ya marehemu peponi wala asimpumzishe, kama kuna mkong'oto huko ampe kiaina'.

AMINA
 
Nakuhakikishia haitatokea historia ya marehemu kuwa namna hiyo hapa Tanzania labda nchi nyingine. Tunaenzi sana utu na heshima za marehemu wetu.
 
Hiyo historia ya marehemu ni ya kuigwa hakuna sababu ya kusifiana uongo kama matu alikuwa jambazi akifa jamii lazima ielezwe kwamba huyu tunaye mzika leo alikuwa hafai katika jamii na bora amekufa na mungu akampe adhabu ya kutosha huko ahera.
 
Nakuhakikishia haitatokea historia ya marehemu kuwa namna hiyo hapa Tanzania labda nchi nyingine. Tunaenzi sana utu na heshima za marehemu wetu.

lakini we unadhani ni vizuri kuficha ukweli?
 
Hiyo historia ya marehemu ni ya kuigwa hakuna sababu ya kusifiana uongo kama matu alikuwa jambazi akifa jamii lazima ielezwe kwamba huyu tunaye mzika leo alikuwa hafai katika jamii na bora amekufa na mungu akampe adhabu ya kutosha huko ahera.
mkuu mi naona ni idea nzuri....mana wenye wasifu mbaya wanapowekwa wazi jamii inajifunza
 
tulikuwa tunamzika jamaa mmoja watu walicheza kamari ndani ya kaburi na kumzika na sigara!
 
lakini we unadhani ni vizuri kuficha ukweli?
Wasifu wa marehemu unaandaliwa na familia iliyofiwa.Ukweli wa maisha ya marehemu alipokuwa duniani usemwe au usisemwe ni uamuzi wa familia. Kama familia itaamua ukweli usemwe bila kuficha kwa kutumia tafsida nyingi litakuwa jambo la kimapinduzi na huenda familia nyingine zikaiga jambo hili jipya. Misingi ya kusema ukweli yaweza kujengwa kwenye haya yafuatayo:

1. Kuonya walio hai waache mienendo inayofanana na ya marehemu.
2. Familia kujiondoa kwenye lawama za kuhusika na kifo cha marehemu.
3.Kufundisha jamii kusema kweli.
4.Kuondoa minong'ono na tetesi juu ya chanzo cha mauti ya marehemu
5.nk nk.
 
turuu.
 
Back
Top Bottom