wasichana wengi wanaomaliza vyuo vikuu hawaolewi

Ndokeji

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
698
474
katika utafiti niliofanya kwa miaka 2 wasichana wengi wanaosoma hadi vyuo vikuu huwa wankuwa na umri mkubwa , wachambuaji wa wachumba hali ambayo huwafanya wavulana wengi kuwakimbia(kuwapiga chini) hivyo kuishia kupigwa mimba na kuzaa watoto wasio na baba kitu ambacho huwa ni tatizo baadaye .Ili kukabiliana na tatizo hilo wasichana wa vyuo wamegundua mtego wa kuwanasa wanaume hasa wanachuo wenzao ambao ni mimba
 
teh teh....kama Me,utakuwa umemdunga mtu mimba unastress now...kama ke,umeporwa mpenz na mwanachuo...duuh..!..
 
Yani wewe utafiti ulio ufanya ndo huo!!!!

Yani umepoteza miaka miwili hivi hivi dogo, bila faida yoyote!!

Pole sana.
 
katika utafiti niliofanya kwa miaka 2 wasichana wengi wanaosoma hadi vyuo vikuu huwa wankuwa na umri mkubwa , wachambuaji wa wachumba hali ambayo huwafanya wavulana wengi kuwakimbia(kuwapiga chini) hivyo kuishia kupigwa mimba na kuzaa watoto wasio na baba kitu ambacho huwa ni tatizo baadaye .Ili kukabiliana na tatizo hilo wasichana wa vyuo wamegundua mtego wa kuwanasa wanaume hasa wanachuo wenzao ambao ni mimba

Ume-publish kwenye journal gani tukajisomee wenyewe??

Babu DC!!
 
Hiyo miaka miwili,kama unasoma ungetengeneza GPA ya maana na kufikiria future yako,kitaa kigumu ukiwa huna job...ooh,mfanyakazi hawezi kuongea hayo maneno.
 
Dah!hizi tafiti zingine upotoshaji tu!mbona wanaolewa wengi tu!hebu uctuchurie km dada zako ndio wametoswa kimpango wenu,shule tumeenda na tutaolewa kwa jina la yesu,ebo!
 
Kwan ni lazma waschana waolewe?kama ndo hvyo bas ucthubutu kuwapeleka wanao shule 7bu hawataolewa na kukuletea ng'ombe za mahari
 
Ukweli jamaa kaanika mfupa hapa na nionavyo wengi katika uchangiaji wanaumauma meno tu, dalili za ukweli huo ni mkubwa, ingawa kuna wanaoolewa, lakini idadi kubwa hawaelewi.

Dhana hii inatokana na ukweli wa mapokea katika jamii zetu za kitanzania kwamba msichana mwenye umri mkubwa hafai kuolewa, na zama hizo alitakiwa kuwa mke wa pili akishapitisha umri mzuri wa ubichi. Pengine wengi wetu ni ule woga wa ukweli kuhusu usawa na haki za mwanamke ndani ya nyumba. Wanaume wasiokuwa tayari kwenda na wakati wanaona bora kwenda kuoa asiyeelimika au ambaye yuko tayari na mfumo dume wa mapokea. Lakini kazi anayokuwa nayo ni kubwa katika familia tofauti kama angemwoa msichana msomi wangetegemezana vizuri katika kujenga familia yao.

Wasichana waliohitimu vyuo vikuu wanatakiwa kujieleza kwa uwazi ubora wao kama mwanaume atawaoa na advantage tofauti na akioa msichana ambaye hana elimu na ana umri mdogo.
 
Sizitaki mbichi hizi, kapige punyeto dogo kama umeshindwa kuwapata dada zetu wenye Bachelors, kwa kifupi ilichoandika ni uongo
 
Hiyo miaka miwili,kama unasoma ungetengeneza GPA ya maana na kufikiria future yako,kitaa kigumu ukiwa huna job...ooh,mfanyakazi hawezi kuongea hayo maneno.

Ninyi ndio mnaorudisha nyuma maendeleo na tafiti zenye kutusaidia katika maisha. Hata wanafalsafa maarufu duniani walijitolea hata kuoa mke wake kwa minajili ya utafiri ili kutusaidia sisi wengine. Bila tafiti mbalimbali tusingekuwa na ilmu tuisomayo vitabuni leo kutujuza mambo mbalimbali.

Mwanafalsafa Sokrates ambaye alijaliwa bongo zuri lililojipanga vizuri ndani ya kichwa kilichokosa sura yenye mvuto kwa wamwonao (uggly guy), aliamua kuoa mwanamke ambaye kitabia alikuwa ameshindikana, na hashikiki. Walipomwuliza kwa nini anaoa mwanamke ambaye anashindikana kabisa na wengine, Sokrates alijibu kuwa ameamua kuishi na mwanamke huyu kwa kuwa akifaulu kuishi naye anajua kuwa anaweza kuishi na mtu ye yote duniani. Na katika kumbukumbu za maisha yake mwanamke huyo alimwendesha kama gari bovu, lakini Sokrates alivumilia ili kupata ilmu ya maisha ya kutufunza wengine..
 
Back
Top Bottom