Wasichana Waliofeli angalao wataolewa

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
Nimesikitishwa sana na kauli ya Mbunge mmoja jionh hii wakati akichangia hotuba ya Mh. Rais, amesema, walifanya mtihani zaidi ya laki 3, lakin walifaulu elfu 38 tu, waliobaki walifeli, akashukuru kuwa, wasichana angalao wamefika f4 kwani wataolewa kwani wamepanda bei. Jamani Mbunge aliyetumwa na wtz anatukana wasichana hv? Kwamb wakifeli poa tu, maana wataolewa. Shame o u such myopic view!
 
Hao ndio waheshimiwa wetu Mkuu, walio wengi ni myopic.
 
ndo upeo wake wa kufikiri umeishia pale.nawapa pole walio mchagua huyo mbunge
 
Yaani kwa kweli anatakiwa awaombe radhi wasichana na wanawake wote kwa ujumla kwa kutudhalilisha. Shame upon him/her, hivi kweli kama ni binti yake wa kuzaa anaweza kusema ataolewa?
 
Naomba namba ya Ananilea Nkya nimwambie. Nadhani labda atamsaidia huyu mjomba wake Tambwe Hiza
 
:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:
 
Halafu kwa kukosa adabu Spika akashadadia eti, Mh, hata wanawake hawapendi mwanaume ambaye hajasoma, kwa kucheka kbs, kama vile kafurahiya alichocema mbunge. Dah
 
Jamani mie naona ni utani mbaya na kejeli kwa masuala ya msingi na muhimu ya maendeleo ya nchi. ELIMU KWA MTOTO WA KIKE NI VIPI- MBONA WANAHARAKATI MKO KIMYA. Hivi wanapowaambia wanapata mimba kwa kiherehere na sasa hili bado mko kimya au yakisemwa na wakubwa sawa.
 
Hayo ni maoni yake kwa sababu ndio uwezo wa kufikiri umefikia hapo!
 
jamani huyo mb ni nani? Na wa jimbo gani? Ili tuweze kumnyambua nyambua what a nonsense speech kawadhalilisha saana kina dada ka ni mwanaume namshauri mkewe amnyime unyumba hadi atakapoomba radhi
 
Mimi sioni kuwa hao wasichana wamedhalilishwa vp! Wanawake mbona hamjiamini? F4 aliyefeli SI SAWA na std 7 aliyefeli, si kweli wandugu?
 
Back
Top Bottom