Washiriki wa kudumu kipindi cha malumbano ya hoja

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Kuna Washiriki fulani wanaojirudia rudia kila kipindi cha ‘Malumbano ya Hoja ITV’ kama vile, Ibrahim Dimoso (aka mwananchi wa kawaida), Ole, ndg. Aweda, ndg. Ngowi n.k. Je, ina maana hao ndio ‘role models’ wa malumbano ya nguvu au kwamba wao ndio wenye ujuzi mpana wa kila aina ya mada na uzoefu (jack of all trades) au nayo imekuwa forum fulani ya kuuza sura?

Mtu anaweza kuwa mzuri katika eneo fulani lakini akachafua sana kwa kuchangia katika eneo asilokuwa na utaalamu nalo kwa undani. Mfano Dimoso kukataa kuwa kondomu si chochote katika kinga dhidi ya ukimwi ni mchango unaoweza kuwa janga la upotoshwaji sana kwa Taifa.
Hali halisi iko wazi juu ya uambukizwaji magonjwa ya zinaa (STIs) kama Kaswende n.k kati ya miaka’ya 1980 na kurudi nyuma na zile za miaka ya 1990 kwenda mbele.

Ni kweli, hatutegemei kuwa na watu wajuzi tu katika kipindi kama hicho cha malumbano lakini pia hatutegemei kuwa na washiriki fulani ambao wapo karibu kila kipindi bila sababu za msingi!
 
Nadhani tatizo lipo kwenye kuwapata hao washiriki, na huenda ikawa na ITV wenyewe hawazitangazii hizi
nafasi lakini kama ulivyosema huwezi ukawa unajua kila kitu! mambo mengine ni ya kitaalam zaidi sio
ya kuporoja tu! hasa hayo ya kondom! ni very sensitive issue inayoambatana na mambo ya kijamii, itikadi n.k.
 
Kuna Washiriki fulani wanaojirudia rudia kila kipindi cha ¡®Malumbano ya Hoja ITV¡¯ kama vile, Ibrahim Dimoso (aka mwananchi wa kawaida), Ole, ndg. Aweda, ndg. Ngowi n.k. Je, ina maana hao ndio ¡®role models¡¯ wa malumbano ya nguvu au kwamba wao ndio wenye ujuzi mpana wa kila aina ya mada na uzoefu (jack of all trades) au nayo imekuwa forum fulani ya kuuza sura?

Mtu anaweza kuwa mzuri katika eneo fulani lakini akachafua sana kwa kuchangia katika eneo asilokuwa na utaalamu nalo kwa undani. Mfano Dimoso kukataa kuwa kondomu si chochote katika kinga dhidi ya ukimwi ni mchango unaoweza kuwa janga la upotoshwaji sana kwa Taifa.
Hali halisi iko wazi juu ya uambukizwaji magonjwa ya zinaa (STIs) kama Kaswende n.k kati ya miaka¡¯ya 1980 na kurudi nyuma na zile za miaka ya 1990 kwenda mbele.

Ni kweli, hatutegemei kuwa na watu wajuzi tu katika kipindi kama hicho cha malumbano lakini pia hatutegemei kuwa na washiriki fulani ambao wapo karibu kila kipindi bila sababu za msingi!

uko sahihi kuna watu kila kipindi hawakosi na kupretend they know everythg its absurd! Wameanza kukifanya kipindi kiwe kama sport kizaazaa ambapo members ni walewale.halafu kila ishu wamafanya siasa,mtu anachangia ishu ya aids lakin ana base kwenye ishu ya uzalendo wat a joke! Nadhan wafanye mchakato wa kushoot vipindi na nje ya dar itasaidia kuona watu wapya na michango tofauti na kupunguza tabia ya baadh ya watu kukigeuza kipindi kama sehemu yao ya kujipatia umaarufu 4political reasons.
 
Tatizo wanaoendesha vipindi vingi vya televisheni na redio wamekariri kuwa watanzania wako Dar tu! Angalia hata maoni kwenye kipima joto ITV kila siku maoni yanachukuliwa kutoka kwa wakazi wa Dar tu wakati wana waandishi/wawakilishi wao kila mkoa. Huu ni upuuzi na ni janga la Taifa na linaongeza ufa na matabaka miongoni mwa watanzania.
 
Watafanya nini zaidi ya hapo?? elimu yao haiwafanyi wawe wabunifu na kwamba uwezo wao kufiri umefikia hapo.
 
A JACK OF ALL TRADES IS A MASTER OF NON. kipindi kinakera sana kuanzia waendeshaji wa kipindi na wageni wanaoalikwa. ni kelele tu!
 
Back
Top Bottom