Washington state sells 2 passenger ferries to Tanzania

Wamarekani ni wauwaji sana wanajua kabisa boti ya mtumba wanawauzia watanzania, ingekuwa imetoka nje ingine sijui ingekuaje humu JF.
 
Phew! JF, truly the Home of Great Thinkers,kwa hili nimejifunza mengi sana. Ninachojiuliza ni kwamba,hizi facts zote tunazozisoma hapa ina maana mnunuzi hakuziona,alikuwa hajui,au ndio kutokujali kama ilivyo tabia ya watanzania? Then yakitokea maafa SUMATRA inazinduka na kutoa ukali wa muda halafu basi.
 
umeanza vizuri, ila mstari wa mwisho ndio umeniachia maswali. Mv Kilimanjaro ilipita muda gani kabla kuzama kwa iyo ferry? Je unafahamu vizuri tabia za bahari? Je sio kwamba inawezekana Mv Knjaro ilipita wakati bahari iko shwali? Sipingi inawezekana iliyozama ni mbovu, lakini kama bahari umechafuka haichagui meli ya kuzamisha, hata kama ni meli mpya or meli kubwa kama USS Enterprise (super carrier) lazima iende chini.Kuna umuhimu kuwauliza Meteorology dept kuhusu hali ya hewa or walionusurika weather ilikuaje hapo+hali ya ferry iliyozama. Tukipata majibu hayo nafikiri mjadala wetu utakua na focus zaidi.
Kuna mtu alie kuwepo kwenye Kilimanjaro 3 akasema: "tulikuwa kwenye boti ya klnjaro 3, tukaipita boti hiyo ya KALAMA{SEAGULL} maeneo ya karibu na chumbe kutoka dar, ilikua inayumba kwa mawimbi makali yaliokua yakisababishwa na upepo wa leo. baada ya dakika kama 25 ikiwa iko nyuma yetu tuliiona ikibiruka na kuzama upande mmoja. watu wote tuliokuwa kwenye k.njaro 3. sehemu ya juu tuliliona tukio hilo. captein wetu hakuweza kurudi kwenda kutoa msaada nadhani ni kwa sababu ya kwamba nayo k.njaro ilikuwa imejaza abiria wengi, hivyo aliona ni bora kwanza kutufikisha znz. tulipofika tu znz akashusha abiria na kugeuza kwenda kwenye tukio. ilituchukua kama mda wa saa 1 na dakika 25 tokea kuiona boti ikiwa inazama hadi sisi kufika bandarini znz." Source: Kuna Taarifa Bodi ya Seagull Yazama Chumbe | Mzalendo.net
 
Dah, hii ni nchi ya laana. Utafikiri viongozi na maFreemasonry wanafurahia damu za wananchi wao wakifa!!
Hivi sisi wabongo ni wazuri kwenye nini?? Michezo vibonde, kodi hatukusanyi, hospitali hazina dawa...tunashindwa hata kukagua ubora wa vyombo vya kubeba abiria!? Aibu hii itatoka kama tutaitosa CCM maana wanapuuzia kila kitu. Kama ushauri ungefuatwa tusingeongelea leo haya maafa.
 
Mpaka serikali itakapojifunza wajibu wake tutaendelea kuwa shimo la taka..ati the boats were made in 1989 and have a life expectancy of 25 years,yet they are bought by Tanzanians in 2011,after 23 years

Mungu saidia nchi hii
 
nadhan wengi hapa tunashabikia kitu tusichokijua the issue hapa ni kwamba hizo boat si salama ktk mazingira ya bahari inayochafuka bila taarifa hasa tukijua uwezo wetu wa kutabiri majanga hatuna vyombo vya kisasa! i will never board such boat thanks i got the tip from here ila najisikia vibaya not all of tanzanians will get this good news!
 
kama tatizo ni passenger comfort tu na siyo sana safety issues hai-mati sana kama mnunuzi ni mtu binafsi. Uroda wa raia wa marekani siyo sawa na wa bongo bana kwa hiyo what's the big deal? Mbona daladala karibia zote watu wanajazana 20 plus beyond normal allowable passenger capacity ya mabasi husika lakini hamna anayepiga kelele?
utawala huu utanunua hata cockroach. Unafahamu mwaka jana ndio walipitisha ile sheria ya kununu vitu chakavu. Wako kwenye project ya kunyonga . Si unaona mv seagul, mv s.islanders, yote hii ni project ya kunyonga . Wabunge wetu bahati mbaya huwa hawafikirii mbali . Wao kazi yao kuuunga mkono hoja 100 kwa 100. Sasa wabongo ndo watajua ni kwa nini serkali ilipitisha muswada wa vyombo chakavu . Mapaka watu wafe bado watu hawagundua tu. Sasa wabunge haohao wameanza kutoa rambirambi wakati mwaka jana walipitisha kinyongeo.
 
Ahsanteni wadau kwa kunifumbua macho hii thread ilianzishwa since 2011 na hatimaye bomu limelipuka, Thanx great thinkers
 
Hivi kumbe ni ferry! Mie nilijua ni boat. Kithungu kinanitesa kweli kutafasiri. Hata sijui kipi ni kipi..pengine nisawa
 
Ndio haya haya. Zitaletwa ferries chakavu hapa zikiua tunaambiwa zilikuwa mpya wakati tayri zimeshaoza na wamarekani hawazitaki tena. Kitu imewekwa mpaka ebay hakuna aliyenunua.

leo wanasingizia upepo mkali, kumbe majitu hayana hata ofisi. Hizi kampuni za mifukoni zinatumaliza watz.
 
Ina maana zimepass test ya kufanya kazi bongo? Au kkiwa kazini mara tutasikia imezamisha abiria huko baharini. wamerekani walikuwa wanatafuta sehemu ya kuzidump naona wamepata
mchawi arifu wewe aiseee.....
 
duh!....
Yaaani nimeona huu uzi ikabidi nianze kuangalia hivi hizi tarehe za kweli au naona vibaya....yaaani unaweza ukazani watu walikuwa wanaandika baada ya tukio.
Nani anasema hii ajali mpango wa Mungu,pumb*** kwa huu uzembe hizi ajali zitakuwa kila siku.Kuna makala nyingi sana ziliandikwa na Mwanahalisi baada ya spice kuzama yaani wangezifuatilia wahusika licha ya meli kuzama watu wengi wangeokolewa na haya mambo ya kutokuwa na uhakika na idadi ya abiria isingekuwepo...
DHAIFU YAAANI UMEFANYA KILA NYANJA DHAIFU,HEBU PUMZIKA MKUU!...
 
Ni jana tuu nilliukumbuka huu uzi niliousoma mwaka jana naona mod wame-ustiki
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom