Washindwa kulimia matrekta kisa hayajazinduliwa na Rais

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
Karume%2832%29.jpg

Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.



Wakulima 417 katika bonde la mpunga la Mtwango, Zanzibar, wamekwama kutumia materekta mapya katika msimu wa kilimo unaomalizika mwezi huu kwa sababu hayajazinduliwa na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Uchunguzi wa Nipashe umegundua kwamba matrekta hayo yaliwasili Zanzibar tangu Julai mwaka jana kutoka Italia.
Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wakulima walisema wamekwama kutumia matrekta hayo baada ya watendaji wa Wizara ya Kilimo kudai hayawezekani kutumika kabla ya kuzinduliwa na Rais.
Walisema kwamba msimu wa Kilimo umeanza tangu mwezi Machi mwaka huu na mwisho wa mwezi huu ndio mwisho wa kupanda jambo ambalo litaathiri kalenda ya kilimo ya mwaka huu
Aidha walisema kutokana na kuchelewa kulima mashamba yao tayari wameanza kupata wasiwasi wa kushindwa kuvuka malengo waliyokuwa wamejipangia katika msimu wa kilimo mwaka huu
“Tumeambiwa kwamba sasa matrekta haya yatazinduliwa na Mheshimiwa Rais Juni 6, wakati mwisho wa mwezi huu ndio mwisho wa kupanda,” alisema mkulima mmoja toka katika bonde hilo la Mtwango.
“Toka kuanza kwa msimu wa kilimo mwaka huu, tumekuwa tukitumia matreka mawili ya mtu binafsi na gharama zake ni kubwa tofauti na matrekta ya serikali,” aliongeza.
Rais wa Jumuiya ya wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda Zanzibar, (ZNCCIA), Abdalla Abass Omar, alisema hana taarifa kuhusu kutotumika kwa matrekiana na suala hilo na kuahidi kufuatilia kwa watendaji serikalini.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira Zanzibar, Khatib Suleiman Bakar hakuwa tayari kuzungumizia swala hilo na kutaka atafutwe Kamishina wa Kilimo Zanzibar .



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom