Washili wampa onyo kali mwigulu nchemba huko arumeru mashariki.....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
..Ni kama upepo umeanza kuwageukia CCM,baada ya kuwazushia wazee wa ARUMERU kuwa awamtaki LEMA sasa hali imeanza kuwa tofauti kabisa..habari zinasema kuwa wazee wakishili wamempa onyo kali kiongozi wa kampeni za CCM ndugu Nchemba juu ya tabia zake walizosikia alifanya kule Igunga..."Tumesikia huyu kiongozi wa kampeni wa CCM anakashfa mbaya sana alifanya kule Igunga,sijui kama ni kweli au la,ila tulisikia,tunamuonya hapa sio Igunga tutamfundisha adabu" alionge Mzee Alisante elirehema...Alipotafutwa ndugu Nchemba kudhibitisha onyo hilo simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa...

Source: Amani jumapili.
 
Nchemba awe makini sana Arumeru. Wameru hawana mchezo na wajinga wajinga. Anaweza kujikuta anakula maembe machachu ohoo!!
 
Wameru wako so smart kwny kusimamia mambo yao. Nawakubali kwa ujasiri na msimamo ktk kutetea mambo yao. Mwigulu Nchemba chunga zipu yako huko Meru. Watakugeuza bucha, chunga sana ndugu yangu. Chezea Wananyiramba lakini sio Wameru.
 
Yeye mwenyewe anajiona ndio jembe lao la kulimia vibaku.
 
Mi naona hao washili ni ganga njaa tu, mara Lema hatakiwi, mara Mwigulu ole wako....

Ni promo za kisiasa sana, kama wangekua muhimu sana wangeshazuia arumeru kuwa genje la ufisadi wa ardhi:A S-frusty2:
 
Hivi washili ni akina nani au ni nani? Kuna wakati nilisikia kwamba washili hawamtaki Lema huko Arumeru; nakumbuka alisema mzee mmoja. Hapa tena kuna mzee mmoja amesema lakini kichwa cha habari kinasema Washili. Hivi kila mtu mmoja mmoja ni WASHILI siyo MSHILI? Napata tabu kidogo. Kama kuna mtu anaweza kunisaidia hilo naomba anisaidie. Bado nipo njiani kuelekea Arumeru huenda nikapata ufafanuzi.
 
Wameru wako so smart kwny kusimamia mambo yao. Nawakubali kwa ujasiri na msimamo ktk kutetea mambo yao. Mwigulu Nchemba chunga zipu yako huko Meru. Watakugeuza bucha, chunga sana ndugu yangu. Chezea Wananyiramba lakini sio Wameru.

Nilidhani mnakerwa na utoaji rushwa anaoufanya, rushwa inaharibu ufahamu wa wamama na vijana wenu, ingekuwa vema mumlie timing mumnyake live msisubiri polisi, mumtende mtakavyoona inafaa. nasema hivi nikikerwa na uharibifu wa fikra kwa vijana wa iramba aufanyao kwa rushwa zake sambamba na afanyavyo dewji pale singida town. Tunamuomba mungu a-bugi step ili mumtende.
 
Hivi washili ni akina nani au ni nani? Kuna wakati nilisikia kwamba washili hawamtaki Lema huko Arumeru; nakumbuka alisema mzee mmoja. Hapa tena kuna mzee mmoja amesema lakini kichwa cha habari kinasema Washili. Hivi kila mtu mmoja mmoja ni WASHILI siyo MSHILI? Napata tabu kidogo. Kama kuna mtu anaweza kunisaidia hilo naomba anisaidie. Bado nipo njiani kuelekea Arumeru huenda nikapata ufafanuzi.

aliposema tendwa uliuliza hili swali! taulo ndo lishadondoka tena ukichutama, ukiinama ulichukue, au ukitimua mbio sisi tutaamua wenyewe tucheke au tunyamaze kwa aibu!
 
Mimi ninajiuliza hivi kweli huko CCM HAKUNA msafi hata mmoja? Huyu Mwigulu Nchemba alisahatikana na kashfa ya kutembea na Mke wa kada mwenzake kwenye uchaguzi wa Igunga. Hilo tu lilitosha kumuweka pembeni, lakini wao (CCM) leo tena ndiyo wanamuweka kwenye SPOT LIGHT kwenye uchaguzi wa Arumeru Mashariki. Hivi hii CCM, JK anaipeleka wapi?

Yale MAADILI ya VIONGOZI siku hizi hayana maana yoyote tena ndani ya CCM?
 
Hivi washili ni akina nani au ni nani? Kuna wakati nilisikia kwamba washili hawamtaki Lema huko Arumeru; nakumbuka alisema mzee mmoja. Hapa tena kuna mzee mmoja amesema lakini kichwa cha habari kinasema Washili. Hivi kila mtu mmoja mmoja ni WASHILI siyo MSHILI? Napata tabu kidogo. Kama kuna mtu anaweza kunisaidia hilo naomba anisaidie. Bado nipo njiani kuelekea Arumeru huenda nikapata ufafanuzi.

Mkuu Arumeru unafuata nini au unaenda kujiunga na Ben kuzindua kampeni za CCM?. Ukweli ni kwamba Mwigulu Mchemba asipoangalia watamtega na mwanamke halafu utasikia habari yake kama si kampeni za CCM kufikia mwisho.
 
Mwigulu kwa jinsi ninavyomjua na ulafi wake wa wanawake, mpaka kampeni zikamalizike lazima ipo siku watamtembeza uchi mtaani!
 
..Ni kama upepo umeanza kuwageukia CCM,baada ya kuwazushia wazee wa ARUMERU kuwa awamtaki LEMA sasa hali imeanza kuwa tofauti kabisa..habari zinasema kuwa wazee wakishili wamempa onyo kali kiongozi wa kampeni za CCM ndugu Nchemba juu ya tabia zake walizosikia alifanya kule Igunga..."Tumesikia huyu kiongozi wa kampeni wa CCM anakashfa mbaya sana alifanya kule Igunga,sijui kama ni kweli au la,ila tulisikia,tunamuonya hapa sio Igunga tutamfundisha adabu" alionge Mzee Alisante elirehema...Alipotafutwa ndugu Nchemba kudhibitisha onyo hilo simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa...

Source: Amani jumapili.

Ccm kumsaidia nchemba aende na mke itasaidia kumsogezea siku
 
Back
Top Bottom