Washikaji yamenikuta...

wazee nawashukuruni sana kwa ushauri, ama kweli inaonyesha umuhimu wa kuwa mwanajamii,asanteni sana ndugu zangu, nitaufuata ushauri wenu wa kindugu kweli mlionitumia. Mungu awarudishie mara dufu na tuzidi kufaana katika jamii forum, ndugu yenu, camfu!!
 
Tena afadhali umeyaona hayo matatizo mapema kulikoni ungeyaona baada ya kufanya commitment kubwa zaidi...omba mungu atakupa mtu anayefaa. Huyo hakufai kabisaaaa
 
pole sana mkuu,that not the end of the world,just jaribu kumsahau na usali sana i know how love pain but jikaze,haikupangwa awe wako Mungu atakupa the right person at the right time just keep pray,sasa nakushauri upambane na elimu kwanza.POLE SANA MKUU.
 
Camfu ningekuwa wewe ningeshamtupilia mbali kuliko mpira wa kona au range. Alishakuonyesha signs zote kuwa si mwaminifu. Huna haja ya kuwa na penzi la kulazimisha. Tena mshukuru sana Mungu amekuonyesha mapema kabla hujaingia katika ndoa. Ila tu kwa uchache ni kwamba siku hizi wake wa kuoa ni adimu bali wanawake wa kustarehe tele. Namaanisha kumpata mama halisi wa watoto wako ni kazi sana. Mabinti wameshapoteza hadhi, wengi wao. Ila jua mke mwema ni zawadi toka kwa Mungu bali utajiri na mali mtu hupewa na babaye.
 
...naomba ushauri wenu washikaji nifanyeje mimi na kiumbe huyu??

...kwakweli mimi nakushauri kwa nia nzuri tu, uende ANGAZA ukapime kama hujaambukizwa virusi.

Kama utakuwa HIV-ve, mshukuru sana mungu, baadae utafute mwingine.
 
"mfano baada ya kulaumu sana ujekupata taarifa kuwa mwenzio alipata matatizo mengi ambayo nawewe ukiyasikia unaingiwa na huruma utasemaje,utaanza kufuta lawama zako najua utapata shida sana kufuta lawama zako kwani utakuwa umesema maneno mengi sana ya kumlaumu mwenzio"
Wewe ungekuwa karibu yangu ningekurushia raba yangu hii ambayo haijui maji mwezi sasa........yaani una akili kweli wewe?
Huyo demu kicheche period.
Demu gani anakutambulisha kwa mates wake kama weye rafiki yake???
Videmu kama hivi mimi navipaga night shift ijumaa tu usiku jumamosi asubuhi nakitimua vinakera sana.......

Mkuu na ww ulikuwa kama vile umelishwa limbwata ndio kupenda gani huko? unatambulishwa hivyo bado tu unakaba? ukabaji gani mechi isiyo na manufaa kwako?......kama timu wewe Mecco ya Mbeya...

Nikushari mkuu hawa viumbe wewe usijiweke kihivyo utajaumia sasa cheki tena inawezekana ulikuwa unamtumia vidola yeye anatanulia na vibongofleva vyake.damn!!
Achana na kicheche hicho....ila usikubali mkomeshe omba game rekodi clip irushe kulee...understood? ndio dawa yao hao mpaka watakoma......
 
wewe ungekuwa karibu yangu ningekurushia raba yangu hii ambayo haijui maji mwezi sasa........yaani una akili kweli wewe?
Huyo demu kicheche period.
Demu gani anakutambulisha kwa mates wake kama weye rafiki yake???
Videmu kama hivi mimi navipaga night shift ijumaa tu usiku jumamosi asubuhi nakitimua vinakera sana.......

Mkuu na ww ulikuwa kama vile umelishwa limbwata ndio kupenda gani huko? Unatambulishwa hivyo bado tu unakaba? Ukabaji gani mechi isiyo na manufaa kwako?......kama timu wewe mecco ya mbeya...

Nikushari mkuu hawa viumbe wewe usijiweke kihivyo utajaumia sasa cheki tena inawezekana ulikuwa unamtumia vidola yeye anatanulia na vibongofleva vyake.damn!!
Achana na kicheche hicho....ila usikubali mkomeshe omba game rekodi clip irushe kulee...understood? ndio dawa yao hao mpaka watakoma......

nafikiri huu ushauri wako tuufanyie backup
 
. Tumekuwa vile na mambo yalikuwa shwari kabisa. One tukiwa out, nislishtuka kuona anapokea simu zinazo mshitua, and then nikachukua simu yake na kuona message eti CHUPI INAFICHA MAMBO MENGI SANA, HATA MIMI NAKUPENDA SANA TENA SANA TU...niliishiwa nguvu na sikuweza kumwuliza chochote kwa kuchanganyikiwa. then once nilipomuuliza alikuwa na kila sababu ya kujitetea, lakini mimi nilipumbaa na kuzidi kumwamini. BAada ya kuwa likizio tena nilimtembelea katika kituo chake cha kazi naye akawa ananitambulisha kwa washikaji zake et mimi ni kaka yake, kitu ambacho sikuweza kukielewa kabisa, na akawa na tabia ya ajabu, kwa mfano hakutaka hata mara moja kunibusu hadhalani nk. Nikaona makubwa na kuamua kuongea naye seriously, bado hakutaka kuniambia ukweli, then nikwambwambia dear if things must be like this then we better stop our relationship, akajidai kulia nk, na kuomba tuendelee kuwa na uhusiano ingawa hataki kunieleza kulikoni, cha ajabu zaidi sasa ni mwezi umepita simpati kwa simu, nahisi kabadili namba namba. naomba ushauri wenu washikaji nifanyeje mimi na kiumbe huyu??

Ni muongo!!... na hakupendi....
mkuu tafuta mwingine kama unataka wa maisha!.. but kama ni wa 'kuzugia' ni poa tu.
 
Issue hiyo mbona simpo sana??? Sidhani kama unahitaji kuomba ushauri.
Piga chini hakuna mapenzi hapo mzee ni WIZI MTUPU!!
 
...kwakweli mimi nakushauri kwa nia nzuri tu, uende ANGAZA ukapime kama hujaambukizwa virusi.

Kama utakuwa HIV-ve, mshukuru sana mungu, baadae utafute mwingine.

mmmmhhh????
Wala usigune, kumbuka kuwa mdada huyo alipotembelewa ofisini kwake alimtambulisha kiboy chake kama kaka yake, hii ina maana pale ofisini wanamjua boy friend mwingine wa mdada huyo. Iwapo hao wote walikuwa wakibanjuka kavukavu...? Ipo haja ya Kamanda kwenda Angaza
 
Achana nae huyoo.
Usipoteze mda wako kumwaza. Waza ni jinsi gani utaboresha maisha yako ili siku ukipata mwingine msiichi dunia 2 tofauti. R/ship za watu wako apart ni ngumu sana.
Pole mdau
 
Mshukuru Mungu sana kwa kukuonyesha alivyo mapema. Kilichobakia pambana na kitabu kwa sana sasa. Amini yupo mmoja aliyeumbwa kwa ajili yako wewe. Muombe Mola akufunulie huyo aliye wako wa milele. Kaza moyo kaka. Wanasema kuachwa ni kubaya sana, ila kubaliana na hali halisi. Wewe mwanaume bwana,,,, ebo!
 
Du pole sana!ni ngumu ila MUOMBE MUNGU akutie nguvu inawezekana huyo hakuwa wako amini kuwa utampata mwingine aliye mwaminifu akupendae kwa dhati!
Huu uzi nilikuwa kigori,hata nilikuwa bado sijazaa. Ila nilikuwa na busara jamani. Mungu endelea kunilinda mpaka miaka 100+
 
Back
Top Bottom