Washikaji yamenikuta...

Camfu

Member
Dec 2, 2008
21
1
washikaji yamenikuta...isssue yenyewe ni kwamba nimekuwa na girl friend wangu katika uhusiano mzuri sana kwa miaka miaka, na kweli nilikuwa na imani naye sana kiasi kwamba hata mara moja sikuwahi kuhisi kuwa anaweza kuwa na mshikaji mwingine. NIlipopaswa kwenda masomoni, alinipa viapo ambavyo hata mimi vilinifanya niwe mwaminifu huku niliko kwa kumkumbuka yeye. Tumekuwa vile na mambo yalikuwa shwari kabisa. One tukiwa out, nislishtuka kuona anapokea simu zinazo mshitua, and then nikachukua simu yake na kuona message eti CHUPI INAFICHA MAMBO MENGI SANA, HATA MIMI NAKUPENDA SANA TENA SANA TU...niliishiwa nguvu na sikuweza kumwuliza chochote kwa kuchanganyikiwa. then once nilipomuuliza alikuwa na kila sababu ya kujitetea, lakini mimi nilipumbaa na kuzidi kumwamini. BAada ya kuwa likizio tena nilimtembelea katika kituo chake cha kazi naye akawa ananitambulisha kwa washikaji zake et mimi ni kaka yake, kitu ambacho sikuweza kukielewa kabisa, na akawa na tabia ya ajabu, kwa mfano hakutaka hata mara moja kunibusu hadhalani nk. Nikaona makubwa na kuamua kuongea naye seriously, bado hakutaka kuniambia ukweli, then nikwambwambia dear if things must be like this then we better stop our relationship, akajidai kulia nk, na kuomba tuendelee kuwa na uhusiano ingawa hataki kunieleza kulikoni, cha ajabu zaidi sasa ni mwezi umepita simpati kwa simu, nahisi kabadili namba namba. naomba ushauri wenu washikaji nifanyeje mimi na kiumbe huyu??
 
Du pole sana!ni ngumu ila MUOMBE MUNGU akutie nguvu inawezekana huyo hakuwa wako amini kuwa utampata mwingine aliye mwaminifu akupendae kwa dhati!
 
Pole sana, jamani tufungue macho hata kama wanasema LOVE IS BLIND. mtu inafikia unatambulishwa kama KAKA alafu unaendeleza libenenke??????!!!!!! pressure nyingine tunajitakia wenyewe, mapenzi ni two way traffic kama hupendwi jua hupendwi na sio mwisho wa dunia. learn to live with it and as time pass utapona vidonda na kumpata uliyefanana naye.

NI HAYO TU.
 
mkuu huyo mtu achana nae huna haja ya kumtafuta katika simu tenda wema nenda zako huwezi kujua huyo aliyenae ametambulishwa kama nani kwa ndugu jamaa na rafiki zake utakuja kuumbuliwa na kupigwa na butwaa kubwa zaidi achana nae tu kuepusha shari wewe ni msomi kijaze zaidi katika taaluma yako achana na mambo hayo yapite kwanza utapata atakayekufaa msee

siku hizi mafataki wako wengi sana angalia usije ukalia na usomi wako umehangaika we mtu anakuja kukuharibia kwa dakika kadhaa tu
 
Haustahili kupewa pole bali wewe ni wa kumshukuru Mungu kwa kuweza kukufunulia tabia za huyo kicheche wako ingali mapema kuliko ungechelewa kumfahamu haya yakaja kukukuta ndani ya ndoa. Hapa kaka hauna mkataba, delete hiyo the number you calling is not reachable, then subiri umalize shule yako kisha utafute kifaa kingine kama unataka kuoa uoe. Lakini uwe makini sana mademu wengi siku hizi ni vicheche.
 
.... cha ajabu zaidi sasa ni mwezi umepita simpati kwa simu, nahisi kabadili namba namba. naomba ushauri wenu washikaji nifanyeje mimi na kiumbe huyu??
Kamanda hapo umeshapigwa chini, maanake hataki kusikia sauti yako wala kusome sms zako, zaidi hata kukuona tena.
 
Hiyo ndio tabia ya dada zetu hawatosheki,bali mshukuru mungu kwa kukufunulia tabia zake mbaya na usije kumrudia,mtafute mwingine na mchunguze kabla ya kuamua kumuoa.
 
Pole sana kaka,
Ninaposikia mambo kama haya kwa kweli huniuma sana roho maana nilishapitia hiyo misukosuko. Cha msingi kama walio wahi kusema, kwa kweli ni jambo la kumshukuru Mungu sana, yawezekana bado unampenda sana huyo binti na yeye akawa anakupenda ni subira tuu ndo iliompelekea kuwa na tamaa na kumfanya kufikia hapo. Piga moyo konde, mtoe kabisa katika mawazo yako, Focus on your career and keep your self busy ikiwa pamoja na kumuomba Mungu sana. Usijali utakuja mpata mzuri hata kuliko yeye.
Kila la heri.
 
Najua unapenda kama Bushoke na kwa huyo dada umefika mpaka uko tayari kwa lolote. Ukipenda kisawasawa unakuwa too blind to see, hata ukitambulishwa wewe ni kaka, unaona sawa tuu as long as unapata kilichokufikisha. Ushauri wangu, hapatikani kwenye simu kwa vile simu yake imeibiwa na moble yako hajaikremu hivyo anashindwa kukutafuta. Keep your hopes high wenzako wakishamaliza zamu yako itakuja tena.
 
Mshiti na just move foward! Ila ningekuwa mimi ningelipa kisasi ili asiwatendee wengine hivyo!

Haina haja ya kulipa kisasi utachuma dhambi bure kwa kitu kisicho kuwa na thamani tena. Kaka endelea na maisha yako hauwezi jua Mungu amekuandalia nini huko mbele, huwa ana makusudi yake kwa kila binadamu. Kumbuka kuwa kila litendekalo hutendeka kwa sababu fulani.
 
Bwana we count your losses and move on... she aint worth your time and breath kama hata kuitwa kaka umevumilia... duh!!! its part of the game wajua but wako utampata when the time and place is right!
 
Najua unapenda kama Bushoke na kwa huyo dada umefika mpaka uko tayari kwa lolote. Ukipenda kisawasawa unakuwa too blind to see, hata ukitambulishwa wewe ni kaka, unaona sawa tuu as long as unapata kilichokufikisha. Ushauri wangu, hapatikani kwenye simu kwa vile simu yake imeibiwa na moble yako hajaikremu hivyo anashindwa kukutafuta. Keep your hopes high wenzako wakishamaliza zamu yako itakuja tena.

duh

Hii kali
ila mkubwa kama walivosema wengine ahpo we angalia mbele, hapo hapakufai tena..Mshukuru Mungu kwa kukuonyesha hilo mapema!

Mi ningepigana the moment ananitambulisha kama kaka! d^amn
 
Pole hawa dada zetu wengi siku hizi ndivyo walivyo. Mtu upo serious na demu then anakuletea za kuleta. Achana neye fuata maisha yako, piga skuli utapata tuuu mwingine hata mimi yalishanikuta.

Ninachokuambia cku si nyingi utamwona hyooooo anarudisha majeshi na kulia kwingi na am sori nyingi kwani yatamshinda huko believe it or not UTAKUJA KUTUAMBIA kwani Malipo ni hapa hapa Duniani na tean wanasema WHAT GOES AROUND .............COMES AROUND
 
Camfu mwanangu, ndo hivyo tena we anza taratibu nyingine, mbona hawa binadamu wapo wapo tu kwa wingi, komaa kaka mbona easy tu!!
 
Pole sana Kaka,
Ushauri wangu utakuwa tofauti sana lakini huo ndio ukweli wenyewe,
Mimi sifahamu tabia za huyo rafiki yako lakini nakuomba jifunze kuwa na uhakika wa jambo ndio uanze kulishughulikia na si kulaumu "mfano baada ya kulaumu sana ujekupata taarifa kuwa mwenzio alipata matatizo mengi ambayo nawewe ukiyasikia unaingiwa na huruma utasemaje,utaanza kufuta lawama zako najua utapata shida sana kufuta lawama zako kwani utakuwa umesema maneno mengi sana ya kumlaumu mwenzio"

Tafuta ukweli halisi na ujue nini kimemkuta mwenzio na hapo ndio utatoa uamuzi mzuri,Pia kufanya mahusiano ya ngono kwa asiye kuwa mkeo ni hatari sana na pia dini zote zinakataza,kama utaona kunamahitaji ya kuwa na rafiki wa mahusiano ya kimapenzi basi nakuomba uanze kufikiria na kuomba Mungu akupe mke mwema wa kuoa na kuanzisha familia yako bora.
 
Penzi lina vizingiti vingi sana. Kwamba ulishawahi kuiona meseji ya utata lakini ukaendelea naye nachukulia kama ishara kwua umempenda huyu dada.
Katika mazingira kama haya huwezi kujua amepatwa na matatizo gani kwa sababu hamjawasiana siku nyingi sana kwani simu yake haipatikani. Nakushauri mtafute, nyumbani au ofisini naye atakuwa na maelezo mazuri kwa haya yaliyotokea... angalie usije ukakosa mwana na maji ya moto, bembeleza ndugu yangu
 
washikaji yamenikuta...isssue yenyewe ni kwamba nimekuwa na girl friend wangu katika uhusiano mzuri sana kwa miaka miaka, na kweli nilikuwa na imani naye sana kiasi kwamba hata mara moja sikuwahi kuhisi kuwa anaweza kuwa na mshikaji mwingine. NIlipopaswa kwenda masomoni, alinipa viapo ambavyo hata mimi vilinifanya niwe mwaminifu huku niliko kwa kumkumbuka yeye. Tumekuwa vile na mambo yalikuwa shwari kabisa. One tukiwa out, nislishtuka kuona anapokea simu zinazo mshitua, and then nikachukua simu yake na kuona message eti CHUPI INAFICHA MAMBO MENGI SANA, HATA MIMI NAKUPENDA SANA TENA SANA TU...niliishiwa nguvu na sikuweza kumwuliza chochote kwa kuchanganyikiwa. then once nilipomuuliza alikuwa na kila sababu ya kujitetea, lakini mimi nilipumbaa na kuzidi kumwamini. BAada ya kuwa likizio tena nilimtembelea katika kituo chake cha kazi naye akawa ananitambulisha kwa washikaji zake et mimi ni kaka yake, kitu ambacho sikuweza kukielewa kabisa, na akawa na tabia ya ajabu, kwa mfano hakutaka hata mara moja kunibusu hadhalani nk. Nikaona makubwa na kuamua kuongea naye seriously, bado hakutaka kuniambia ukweli, then nikwambwambia dear if things must be like this then we better stop our relationship, akajidai kulia nk, na kuomba tuendelee kuwa na uhusiano ingawa hataki kunieleza kulikoni, cha ajabu zaidi sasa ni mwezi umepita simpati kwa simu, nahisi kabadili namba namba. naomba ushauri wenu washikaji nifanyeje mimi na kiumbe huyu??

Pole sana kwa yaliyokukuta. Girlfriend anapoanza kukutambulisha kwa watu wengine kama kaka yake basi ujue kuna jambo kubwa na huna hata haja ya kuuliza kulikoni maana anaficha siri kubwa na ndiyo sababu ya kukutambulisha kama kaka. Usipoteze muda wako bure kuhangaika naye, piga moyo konde na utapata mwingine atakayekupenda kwa mapenzi ya kweli na hatakuwa na tabia za kitapeli kama huyo mwingine.
 
Back
Top Bottom