Washauri wapya

Nadhani kuna kitu bado tunakimiss kwenye mjadala huu.. na Pundit na Sahara mmekigusia kwa mbali...

Wazungu (includes Wajapan) wanasikilizwa zaidi kwa sababu ya 'ngozi' yao siyo elimu. Miaka fulani nikiwa kwenye semina niliuona ukweli huu. Watu waliokuwa wanaendesha semina hiyo kwenye ukumbi wa then Nyegezi Social, walikuwa wanatoka Dar wizara fulani.

Basi semina tukawa tumegawanyika kwenye makundi na watu wakawa wanatoa maoni juu ya kutatua jambo fulani. Sasa kwenye majumuisho kundi kubwa la waswahili wenzangu toka kijijini wakawa wamependekeza jambo fulani ambalo naamini lilikuwa na mantiki. Wenye semina wakalipinga kwa visingizio kadhaa kuwa halitekelezeki bla bla bla.. Na tena walionesha kama kebehi ya aina fulani kwamba "tulithubutuje kufikiria jambo kama hilo huko kijijini".

Uzuri wake ni kuwa tulikuwa na Padre Mmoja toka Bariadi (nakumbuka jina lake Fr. Gappa) amekaa Tanzania kwa karibu miaka thelani na ana kimwaga kisukuma utadhani ni ngosha! basi yeye hakuwa kwenye kundi letu; basi akasimama na kutoa pendekezo lile lile; wakuu wa semina wakalikubali! Sasa inawezekana kulikuwa na sababu nyingine lakini tuliokuwapo tulihisi kitu kimoja tu hatukusikilizwa kwa sababu hatukuwa wazungu siyo wasomi...

Sasa naamini wataalam wa kizungu wakituambia kuwa Takakata ni mbaya mtaani tutasimama kusafisha; lakini akija mbondei mwenzetu na kusema Takataka ni mbaya tutamkodolea macho na kumpuuza!!

Hivi kweli mnafikiri Tanzania ingetaka kupata net milioni tano kwa kila Mtanzania tungeshindwa? Kwanini hiyo impromptu idea ya Bush ilishangaliwa?
 
Kuna hii hoja ya TRA na magari mitumba (used car) mswahili kujinunulia ka mtumba kake inakuwa haramu, sasa gari limekuwa kama kunywa gongo kila chombo cha dola kinawewe, TRA, trafik, sumatra, tbs, parking system.

tunalipa road licence ya 150,000/= kila mwaka na barabara tunachimba wenyewe kwa harambee, siwalipe dar wenye barabara za lami! hili tunasumbiri world bank watushauri kweli? kwangu mie gari ni sawa na baiskeli, tv, friji na pasi, hii sio anasa kama TRA wanavyodhani.
 
Ni wapi tunaweza kupata washauri wa kizungu ambao wana rekodi nzuri na watatusaidia kuendesha vitu kama Benki Kuu n.k.. sitaona ubaya hata tukiomba washauri wa Usalama wa Taifa...

Thubutu Mwanakijiji

Wewe kwa exposure yako uliona wapi hizo nchi makini wakitawanya krimu zao nje. Zile krimu wanabaki nazo, sana sana watatupelekea reject.

Kama mchingia mada alivyodokeza hapo juu, ni nani anayethubutu kuangalia CV zao wanapokuja??

Nimekuwa nikifuatilia vitu anaongeavyo Mengi kwenye public. Nimegundua ana hekima kubwa.

Yeye kila mara huzungumzia tatizo letu kubwa lipo kwenye mindset. Bila kubadilika hapo hatuwezi kufika popote.

Ni kama kinachojengeka ktk vichwa vya watoto wanaokuwa sasa hivi ni dhana ya ufisadi.Watakapokua watu wazima kwao litakuwa ni jambo la kawaida tofauti na mtizamo wetu tuliotangulia.

Tulizoea kulisikia kwa majirani.

Amini nawaambieni hii ishu ya ufisadi na mafisadi itadumu vizazi hadi vizazi na kuviathiri kwa kiwango cha juu.
 
Back
Top Bottom