Washauri wa Rais wanamdhalilisha, au hashauriki?

NI KWELI WAPO VIONGOZI wabovu ambao kwa namna moja ama nyingie wanamuangusha AMIRI JESHI MKUU WA NCHI YETU JK, katika hili Mh Jakaya anatakiwa kuwamulika kwa jicho la tatu watu wa namna hii hawafai kuwepo katika serikali yake kabisa, liko suala la KISIASA liliingia hapo kwamba wateule wengi huku serikalini kama MAWAZIRI/NAIBU/MAKATIBU WAKUU/ WAKUU WA MIKOA WAKUU WA WILAYA, WAKURUGENZI, WAKUU IDARA wengi walikuwa walichomekwa kinyemela na Ndugu LOWASA EDWARD hilo ni gumzo kuuuuuuubwa mitaani kwamba walikuwa ni watu wake hasa katika serikali ya kipindi cha kwanza cha JK.

AWAMU YA PILI YA JK MWANGAZA UMEANZA KUONEKANA..........wabovu wengi wamepumzika tu vizuri hii hata ukiangalia bungeni wengi wao wabunge wamepumzika, kwenye idara mbali mbali pia wameenza kuondlewa, juzi juzi hapa MAKATIBU WAPYA WAMETEULIWA naamini watafanya kazi vizuri bila kuingiliwa katika utendaji wao, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA naamini itakuwa hivyo watafanya kazi zao kwa ufanisi zaidi. NAAMINI HATA WAKUU WA MIKOA WAPYA NA WAKUU WA WILAYA WAPYA WATAFANYAKAZI KWA UFANISI ZAIDI.

JK anajua anachokifanya anajua wapi pabovu wapi panahitaji mkazo ndio maana watendaji wengi wameanza kuamka sasa ombi langu ni kwa hao WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA watakaokuja muda utakapofika WACHAPE KAZI KWELI muda wa lelemama umekwisha katika ardhi ya Tanzania, wananchi wanahitaji msaada wao wa karibu zaidi kutoka kwao, so wachape kazi kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria za nchi.

Jakaya songa mbele zaidi ninaimani na wewe, piga chini viongozi wa serikali wabovu, wengi waliwekwa na jamaa yako aliyekuangusha mmasai feki kumbe ni MMERU tu mjinga sana LOWASA chakachua wote weka TEAM WORK yako itakayofanya kazi sawa sawa.

HASA WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA.

NAKUTAKIA AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Siyo tu kumwangusha wanafanya kazi kadiri ya uwezo wao, isopokuwa yeye anawaangusha. Mpaka sasa naona hili la kukamata watu ni dogo mno ukiringanisha na hali halisi. Hali halisi ya Tanzania kama taifa ni mbaya sana
 
Walisema rais hataki kushauriwa, na akishauriwa kesho hugeuka. Masikini alianza vizuri lakini sasa jahazi linamuelemea.
 
Mimi napinga kabisa hii falsafa ya eti Rais wetu anapotoshwa na washauri wake. Mwalimu Nyerere alisema "Mtu mwenye akili akikushauri kitu cha kipumbavu huku akijua kuwa kitu hicho ni cha kipumbavu halafu wewe ukakifuata, atakudharau". Sasa kusema kuwa washauri wake hawampendi, hatumtendei haki Rais wetu na pia tunawaonea bure washauri wake hao.

Tujiulize maswali marahisi ambayo wala hayahitaji kutumia akili sana;
- kwani ni nani ambaye anawateua hao wasaidizi wa Rais?
- Je, hao wasaidizi wa Rais wana akili sana kuliko Rais wetu mpendwa?
- Sasa kama wanamshauri mambo ya kipumbavu kwanini yeye anakubali?
- Ni nani mwenye mamlaka ya kuwaondoa hao washauri wa Rais wetu mpendwa?

Ama kweli KAMANDA LEGELEGE HAWEZI KUTENGENEZA JESHI IMARA
 
Back
Top Bottom