Washabiki wa Kanumba wataka kumuua mama Lulu

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
MAMA mzazi wa supastaa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu,’ Lucresia Karugila anadaiwa kuikimbia nyumba anayoishi kwa kile kilichoelezwa ni kuwakwepa mashabiki wa marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ambao wamekuwa wakivamia na kumtishia kifo baada ya mwanaye kuhusishwa na kifo cha staa huyo kipenzi cha watu.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mama Lulu ameikimbia nyumba hiyo iliyopo Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam tangu Aprili 20, mwaka huu ambapo kwa sasa anaishi Mwananyamala Komakoma kwa rafiki kipenzi wa Lulu aliyetajwa kwa jina moja la Muna.

KAULI YA JIRANI MMOJA “Jamani hivi mna habari kwamba mama Lulu siku hizi anaishi Mwananyamala Komakoma kwa rafiki yake Lulu aitwaye Muna? Nasikia huyo Muna ni ndugu na msanii wa maigizo mmoja mwenye jina kubwa. “Huku Tabata ni kuchungu, tangu mwanaye akamatwe kwa kifo cha Kanumba, mashabiki wa marehemu wamekuwa wakienda kwake na kumtishia kifo. “Lakini pia ndugu wa mama Lulu na marafiki, nao wamechangia huyu mama kukimbia nyumba kwa sababu kila kukicha walikuwa wakijaa tele eti kumpa pole, mama wa watu akaona cha kufia nini, akatimua,” kilisema chanzo hicho.

MALEZI MABAYA YA LULU NAYO YATAJWA
Chanzo chetu kikazidi kudai kwamba mbali na mashabiki wa Kanumba kumtishia kifo mwanamke huyo, pia walikuwa wakimkejeli kwamba malezi mabaya ndiyo kiini cha mwanaye kumfika makubwa. “Halafu hao mashabiki bwana, wakawa wanamwambia mama wa watu kuwa malezi mabaya ya mwanaye ndiyo yamemfanya afikwe na mazito kama yaliyomfika,” kilidai chanzo. SAUTI YA MAMA LULU Baada ya kunyetishiwa nyeti hizo, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilimwendea hewani mama huyo ili kutaka kujua juu ya madai hayo.

Mwandishi: Haloo … natumaini naongea na mama mzazi wa Lulu eeh?
Mama Lulu: Ndiyo baba, wewe nani mwenzangu?
Mwandishi: Naitwa Musa Mateja
Mama Lulu: Unasemaje mwanangu?
Mwandishi: Mama tuna taarifa kuwa umekimbia nyumbani kwako..?
Mama Lulu: Haaa... unasemaje?
 
Gazeti la kiu nimeliona hilo yani wameweka picha za kanumba anakabana na lulu na nyingine kanumba kadondoka kwenye marumaru sasa sijui wametoa kwenye movie gani?
 
Hawa viumbe bado wanamshabikia mwenzao wakati kesha RIP.
Hawajayakubali matokeo kuwa HE IS GONE!
WANA ROHO NNNNGUMU!!!!!
 
Uzungu ndo tatizo,mtoto hayupo nyumbani nane za usiku hata hujali....acha avune alichopanda.Nimejifunza kitu,kama umeachana na mwanamke,hujaachana na watoto wako!
 
hata mwanangu akizaliwa simuiti LULU hili jina washalitia Gundu
 
Back
Top Bottom