QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115
Maajabu!!!!!
Wakati aliyekuwa Rais wa Senegal amekubali kushindwa Urais na mpinzani wake Macky Sall, wale wote waliokuwa wakimshabikia Wade, wamejitokeza mtaani kushangilia ushindi wa Sall. Hii ukiiangalia kwa haraka, unaweza kuchanganyikiwa. Sababu unaweza kuona watu wamekuja kwa wingi kukusikiliza, kula nawe, na kushangilia, ukadhani hao wanakuunga mkono kumbe wapi... Inawezekana wanashangilia kwa vile kuna faida wanayoipata kwa kupiga makofi hata kama ni ya muda mfupi.
Watu hao hao walishiriki kupiga kura! mara ya kwanza, wagombea wakashindwa kufikia idadi ya kura. Kura zikarudiwa, Wade aliendelea kupata watu wengi wanaomshangilia kwa bidii. Siku ya kura ikafika, zikapigwa na matokeo yakaonesha Sall ameshinda kwa kura 30,000 wakati Wade amepata kura 11,000. Kumbuka waliokuwa wanamshangilia ndio waliopiga Kura. Jua kuwa wakati uchaguzi unafanywa, Alikuwa bado na madaraka yote na dola ilitumika lakini hayo yote hayakuweza kuizuia nguvu ya Umma kufanya kazi.
Sasa kwa JK ambapo maroli hutumika kusomba wananchi ili wamsikilize hata wakati ambao siyo wa Uchaguzi, hali itakuwaje? Mwezi Feb Rais Kikwete alikuwa Mwanza kwenye sherehe ya CCM kutimiza miaka 35 ya kuanzishwa kwake alipochinja ng'ombe 55 wakati watu wanakufa muhimbili, wananchi wakiona haya yote. Siku hiyo maroli yaliyosomba wananchi kuwaleta Kirumba kula, hayahesabiki. Kwa hiyo utaona wananchi wengi kwa sababu ya Lift, fedha na chakula!
Asije akashangaa mwaka 2015 ya wade yakimpata!
Quality
:scared: