Wasemavyo wazanzibari

Kwa hakika, baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa Tanganyika nao walifanya jaribio la kuifanya nchi yao iwe na serikali yake ndani ya Muungano. Jaribio hilo halikufika mbali kwani Mwalimu Julius Nyerere alitumia nguvu zake za turufu na kulizima suala hilo.
 
Wazanzibari wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni. Japo nahisi watu wa aina ya Jussa wana ajenda ya siri nyuma ya suala hili la Muungano.
 
Nawashngaa mnaoona ajabu ya hicho kilichoandikwa hapo. Tuliwaona wabunge wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao wakisusia vikao vya kujadili muswada wa sheria za kutunga Katiba.

Hicho walichoandika wa Zanzibar ndio ifikie mpaka muwatusi? tungeona mnaanza kwa kuwatusi chadema kwa kususa kazi yao iliyowaweka bungeni., tungwaelewa kuwa ni watenda haki. Au mkuki kwa nguruwe tu?

nguruwe inahusika vipi na wazanzibari?
 
Hatuwaachii hawa,wataendelea kuwa koloni milele,hawana uwezo wa kujitawala.

Hata Baba yenu wa Taifa alisema maneno kama haya; "Ningekua na uwezo ningevichukua visiwa vya Zanzibar na kuvizamisha katikati ya Bahari ya Hindi". Matokeo yake kazama yeye tena chini kabisa zaidi ya bahari ya Hindi na kuwaachia Wazanzibari na Zanzibar yao bado wangali wanatesa. Zanzibar Daimaaa mbeleee,
 
Tuwaachie wa Zanzibar kivyao waamue nini wanachotaka kwa nchi yao kwa vile hawajaridhika na Muungano huu!!!
 
Zanzibar suala la Muungano ndo jambo kubwa linalozungumzwa Visiwani. Muungano unajadiliwa mijini, vijijini na kwenye vitongoji Unguja na Pemba. Ukiwasikiliza wananchi wa huko utawasikia wanataka irejee Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ikiwa ni dola kamili iliyo huru ikiwa na funganisho na Tanganyika pamoja na nchi nyingine za eneo hili. Tofauti ya mahusiano yaliyopo sasa na hayo wayatakayo ni kwamba wangependelea huo mfumo mpya wa mahusiano ya kufungamana uwe wa mikataba na si wa Katiba.
Msimamo huo ni sehemu ya ile iitwayo Ajenda ya Zanzibar niliyowahi kuizungumzia miezi kadhaa iliyopita. Ni ajenda inayopigiwa debe na wengi wa Wazanzibari wakiwa pamoja na viongozi wao kutoka vyama tofauti vya kisiasa.
Wengi wao wanaamini kwamba kutokana na Hati za Muungano na mambo mengine yaliyoingizwa kuwa ni ya Muungano rais wao amepungukiwa na madaraka. Na si yeye tu bali pia na baraza lao la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi) na Mahakama yao. Mamlaka ya taasisi zote hizo tatu za Zanzibar, ambazo ni mihimili mikuu ya dola, yamepunguzwa katika kipindi cha miaka 47 ya Muungano.
Kilichotokea ni kwamba kwa muda wote huo unaokaribia nusu karne mamlaka au madaraka yote ya Zanzibar yaliyo muhimu yamehaulishwa Tanganyika. Ujanja ulitumika kulifanya Bunge la Tanganyika liwe Bunge la Muungano na kuigeuza Katiba ya Tanganyika iwe Katiba ya Muungano. Ujanja vilevile ulitumika kuifanya Serikali ya Muungano iwe ndiyo Serikali ya Tanganyika na ya Tanganyika iwe ya Muungano. Shughuli za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na za Jamhuri ya Tanganyika zimekuwa zikiendeshwa na Serikali moja.
Kwa upande mwingine, Zanzibar na Serikali yake hazina jukumu kubwa au la maana katika utawala na uongozi wa Muungano. Ingawa kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa na kwa mujibu wa Hati za Muungano, Zanzibar na Tanganyika ni washirika wenye hadhi sawa ndani ya Muungano, mambo yanavyokwenda ni kwamba Zanzibar imewekwa kando.
 
attachment.php


Tatizo la Wazanzibar wanafikiri wanaibeba Tanganyika kumbe wao ndio wanabebwa waacheni muungano usambaratike wanataka kujilinganisha na Scotland etc. Watakoma tu wala siku si nyingi.
 
Tatizo la Wazanzibar wanafikiri wanaibeba Tanganyika kumbe wao ndio wanabebwa waacheni muungano usambaratike wanataka kujilinganisha na Scotland etc. Watakoma tu wala siku si nyingi.

Ajabu ni kwamba hao wanaoonekana ni mzigo ndio ambao wanataka watuliwe lakini wale wanaojifanya wamebeba mzigo ndio wanang'ang'ania na kulawalazimisha watu waamini kwamba wakiutu huo mzigo utapata tabu! Pamoja na malalamiko ambayo hua wanayatoa lakini wanaonekana hawalo tayari kuutua mzigo! Kizungumkuti! Hapa si bure ipo namna, kwa nini muwe na mwangi wa hofu kiasi chote hichi, waacheni waende basi muone kama itatokezea siku watawafata tena hata kwa kuja kuwaomba chumvi na moto.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom