Wasanii wetu wa Bongo Fleva na Bongo Movies kasomeni English Course

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,939
517
Natoa ushauri wa bure kwa wasanii wetu kina Diamond, Ney, Kiba, Kingwendu, JB, Wolper na wengineo waende English Course ili angalau watoe kazi kwa lugha ya Kiingereza au Kifaransa. Tunafahamu wanakwama hapa kwa sababu ya lugha gongana.

Tunajua wasanii wetu kina Diamond na wenzake wakipata mialiko Ulaya huishia kuwatumbuiza Watanzania wachache waishio kule, lakini ni nadra kuwakuta Wazungu kwa sababu wanakua hawajui muimbaji anaimba kitu gani?

Wakijua atleast Kiingereza na Kiifaransa itasaidia kuwapush up kidogo hasa kimataifa.

Nawasilisha..
 
Sawa ila sio muhimu sana sababu sanaa nitofauti na hotuba..na ata hotuba ukighaili unaongea lugha yako watafute wakalimani wenyewe ndio kutangaza lugha yetu..wasanii wengi wanjee uwasilisha sanaa zao kwa lugha zao..why sisi tuwasilishe Sanaa yetu,mziki wetu kwa lugha yao alafu tutaitwa wakina Nani..Sanaa uwa Haibaguliwi kwa lugha..na ndio mana wazungu walicheza mnanda wingereza bila kujua nin Kinaimbwa vivyo ivyo sis uwa tunapenda na wengine at a kukalili maneno ya baadhi ya nyimbo za kizungu bila kujua maana.tunaangalia sinema zao nakuzipenda bila kuelewa nin kinasemwa me naona tungeongeza bidii kuitangaza lugha yetu ili nawao wakataman kuijua lugha yetu"...yangu ayo naihati wakwanza Mimi..
 
Mtoa mada ni mtumwa wa fikra. Jikubali.

Unakumbuka Rais wa china alivyokuja nchi wakati wanasaini mikataba alikuwa anaongea kwa Lugha gani, Rais wetu je?

Mchina kaongea kichina ila mbongo kaongea kiingereza wakati waliokuwa wanafuatia ni wabong na wachina kwa asilimia kubwa.

Sambaza lugha yetu ijulikane kimataifa.


Cabo Snoppy alikuja bongo akaimba kama mtoto mchanga anajifunza kuongea ( aba ba ba ba aba aba Zagala ) na bado tulicheza wala haikutupungizia kitu.
 
Mbona wakorea wanatoa za movie za lugha yao na zinauzika tu

Mwambie huyu mtumwa wa fikra, nashangaa wanaowacheka wabongo wanaoongea broken kimataifa na kitaifa, mambo ya kawaida sana hayo.Angekuwa hajui Lugha ya Taifa hapo sawa.
 
wakongo wanaimba kilingala na wanapiga show nje balah,uliza bongo man alivyokuja bongo.

ata uko ulaya na america wanapiga sana show.

kuna awa wana njenje muda mwingi wanapiga show ulaya mbona wanaimba kiswahili na wanajaza watu
 
Nenda Manzese, Mbagala, Kimanzichana na kwingineko utasikia nyimbo za Beyonce, Rihanna, Bob Marley e.t.c na sina uhakika kama hawa watu walipitia swahili course.
 
Wakongo toka 19kweusi wanatumia lugha yao na watu tunapenda sauti na midundo haya mambo ya tafsiri ni miaka hii zamani iwe avalon, empire au new chox watu walijaa kuangalia picha za kihindi na mtu anakusimulia utadhani anaijua lugha.
 
Sema warudi shule wakaongeze ujuzi ili kazi zao kuwa na ufanisi zaidi maana kama bongo movie ukiangalia nyingi zinachefua picha na sauti zinakera hata waigizaji hawavai uhusika ipasavyo kuendekeza ubishororo tu
Bongo fleva mtu akitoa single moja ikahit anabweteka kitambi hikoooo juhudi haweki ni yeye na club, pombe na vimada
 
Mtoa mada in mtumwa wa fikra na kimitazamo,jikubali na ukubaliwe,acha fikra za kimaskini mtoa mada.
 
Sema warudi shule wakaongeze ujuzi ili kazi zao kuwa na ufanisi zaidi maana kama bongo movie ukiangalia nyingi zinachefua picha na sauti zinakera hata waigizaji hawavai uhusika ipasavyo kuendekeza ubishororo tu
Bongo fleva mtu akitoa single moja ikahit anabweteka kitambi hikoooo juhudi haweki ni yeye na club, pombe na vimada

hiyo ni hoja ya msingi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom