Wasanii wa Miziki na na Maigizo waibiwa kweupe Jijini, wenyewe waishia kupiga mizinga!

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,753
7,075
Kama kuna jambo la kusikitisha ni hili la wasanii wa mziki na maigizo katika luninga. Wasanii hawa hujituma sana kubuni njia ya kujinasua na umaskini kwa kutumia muda mwingi na pesa kibao kutunga video za maonyesho na miziki, lakini ku-ulaini watu udurufu na kusambaza bila kukamatwa, utitiri wa maduka mengi yanayodurufu na kuuza copy kama original yamefunguliwa mengi. wasambazaji hawa wanaonekana kuhodhi fedha nyingi kwani hata frem za mbele huchukua kodi ya kwaka kwa millioni 12. Hadi kufikia jana kuna maduka 30 ya video feki kutoka kwa wasanii wa kibongo pamoja na za kichina. Kumekuwa na utapeli wa kutuuzia CD feki na CD hizo hupata mikwaruzo kiraisi sana hivyo kukulazimu kuangalia kwa mara moja tu. Hata hivyo hapa wakati naingia mitamboni nimeona vijana wengi sana mitaa ya kariakoo wakiwa wamejaza miziki ya wasanii wa kila haina ya video na sauti , mziki mmoja mpya huuzwa mia tano mpaka 200 hukitaka CD collection ya wasanii bora katika DVD collection ni 3,000.00. Kwa ubande wa vijana walioweka Computer Barabarani humpa mgambo sh 5,000.00 hadi 3,000.00 kwa siku ili waachie waendelee. vijana hawa hufanya hata pakingi kuwa ngumu kwani wamechukua eneo kubwa la kupatiki na kuweka komputer zao. Kuhusu hawa wa maduka kuna polisi wa msimbazi huwa wanapitia chao jioni. Kuna haja ya serikali kukataza kopi zote, hasa zinazohusu technologia ya SIM na CD kwani wananchi wanapata hasara sana.
 
Kuna ukweli, ila si nilisikia wasanii wakishereka baada ya kuambiwa sa serikali ya kwamba kutakuwa na sheria ya hati miliki ya kazi zao, na watapewa TIN kuanzia mwakani. Ngoja tusubiri.....
 
Mimi nyimbo zote huwa nazipata hapa Tubidy Mobile Video Search Engine kupitia simu yangu

Ni kweli hata Darhotwire nayo inaendekeza kugawa nyimbo za wasanii bure, tukemee hali hii kwani wakifa njaa ni wakwanza kuwacheka, hata hii kampuni ya wahindi Step Entertainment siiamini sana , haiwezekani CD inunuliwe mia tano iwekewe kava na baadaye ihuzwe 1000.00
 
hiii ndiyo hali halisi ya nchi yetu... Mnyongr mnyongeni haki yake mchukuwe
 
Ni kweli hata Darhotwire nayo inaendekeza kugawa nyimbo za wasanii bure, tukemee hali hii kwani wakifa njaa ni wakwanza kuwacheka, hata hii kampuni ya wahindi Step Entertainment siiamini sana , haiwezekani CD inunuliwe mia tano iwekewe kava na baadaye ihuzwe 1000.00

Siku hizi hizo ndizo njia azitumiazo msanii kusambaza kazi yake kwenye mitandao, mfano wasanii wengi wanapotoa kazi zao huwafikishia bloggers pia ili waweze kuzisambaza bure mtandaoni
 
wasanii hasa wa bongo movies wajipange tena sana hvy watu wakianza kuweka video youtube kuna haja ipi ya kwenda dukani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom