Wasanii wa Kiume kujichubua...!

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
Skuizi imekua fashon kwa wasanii wa kiume kujichubua na kujipaka mkorogo...! Hi imekaaje?


Kujichubua.jpg
 
mkuu,

Usiwalaumu sana watu hao, wana matatizo ya kisaikolojia na wanahitaji ushauri nasaha.

Ni aina moja ya uchakachuaji wa nafsi zao. Ni wa kupewa pole.

Kuna wanaJF husema ,"miafrika ndivyo ilivyo". Kasumba zimewaingia na kuwateka akili. Anyway, dunia ni uwanja wa fujo.
Hivi hawajawahi kusikia kuwa kuna black diamond!!?? au...not all that glitters is gold.
 
Hao ni wagonjwa wa kesho, usilolijua ni usiku wa giza. Kemikali wanazotumia zinakwenda kupumzika kwenye viungo muhimu vya mwili, hususan figo na maini. Vikiacha kufanya kazi hivyo na roho inaacha mwili, lakini kabla ya hatua hiyo mateso hata sasa wanayo kwani wanapata shida katika mwanga mkali hususan wa jua kwa vile tabaka ya juu ya ngozi wameiondoa ambayo ndiyo kinga. Lakini inasemekana kuwa ishi kwa raha kwa muda mfupi kuliko maisha marefu ya mateso. Wanapendeza japo wanaashiria kutokuwa riziki. Mwanaume utajirembaje hivyo, unataka nini?!
 
Si wasanii tu hata wasio wasanii tunakutana nao mitaani wengi wamejichubuwa.

Cha kushangaza si wanaume tu, umeshaona wanawake wanavyojichubuwa? mpaka wengine wanakuwa wa pinky sura zao. Hatari kubwa sana hii, nasikia hawa wanawake wanaojichubuwa mwili mzima hutowa harufu mbaya sana, jee ni kweli jamani?

Kama ni kweli kwa nini dada zetu wanakataa Rangi za asili alizotuumba nazo Mwenyeezi Mungu, kuna urembo wa kuzifanya ngozi ziwe nyororo na kuvutia, tena wala hauna gharama ni wa kiasili kabisa wala hauna haja ya kujichubuwa. Vitu kama asali, samli safi, vikipakwa mwilini, ngozi inakuwa na mvuto wa kipekee na nyororo na inabaki na rangi yake ya asili, tazama wasomali, hukuti wamejichubuwa lakini tazama ngozi zao zilivyokuwa laini, ni samli tu wanapaka.

Sasa na hawa wanaume tena hata sijui kwa nini? labda dili kuwa mweupe?
 
Back
Top Bottom