Wasanii THT waalikwa na Usher USA

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
usher.jpg

BAADHI ya wasanii nyota kutoka kituo cha Tanzania House of Talents (THT), wamealikwa na msanii nyota nchini Marekani Usher Raymond kupitia taasisi yake ya New Look Foundation iliyopo katika jiji la Atlanta.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana, ziliwataja wasanii hao kuwa ni pamoja na Mwasiti, Amini, Barnaba, Ditto, Linah pamoja na mpiga kinanda Mose Delema.



Mwanzilishi wa THT, Ruge Mutahaba



Mtangazaji wa kituo cha redio 88.4 Clouds FM, Hamis Mandi aka B-Dozen

Nyota hao ambao wataambatana na mwanzilishi wa THT Ruge Mutahaba, pamoja na mtangazaji wa kituo cha 88.4 Clouds Fm Hamis Mandi ‘B Dozen” wakiwa huko watapata kutumbuiza katika jukwaa moja na Usher
 
Kualikwa? mafanikio? Kama yale yale yaJK kuwa rais wa kwanza wa kukutana na Obama ikulu ya white house! So what? Ongezea basi na .... wa kwanza kualikwa na Usher USA. Mitanzania bana....!
 
Kualikwa? mafanikio? Kama yale yale yaJK kuwa rais wa kwanza wa kukutana na Obama ikulu ya white house! So what? Ongezea basi na .... wa kwanza kualikwa na Usher USA. Mitanzania bana....!
toa credit panapohitaji credit .. sio kila kitu ulete u snitches
 
Hongera zao wakaipepelushe bendera ta Tz vyema wakiulizwa kuhusu mgao wa umeme wasema wao sio wasemaji wa nchi,maana juzi juzi nilikuwa uko nkagongwa ilo swali majibu siri yangu
 
ukweli wasiwasi wangu kwenye communication, na hivi wasanii wetu wengi wameishia form two, sijui itakuaje, au wamemchukua mkalimani?
 
Ila hawa watoto wanaimba jamani; acheni tu wapate mialiko. Hasa Linah na Barnaba; mpaka burudani.....!!!
 
wabongo sisi kama kawaida yetu ni kukandiana tu, hakuna anaekubali mwenzake akienda angalau step ahead kidogo..tutafika kweli????
 
ukweli wasiwasi wangu kwenye communication, na hivi wasanii wetu wengi wameishia form two, sijui itakuaje, au wamemchukua mkalimani?
Kujua lugha ya kigeni ni kitu katika maisha lakini si jambo la kumkosesha mtu usingizi,ndio maana viongozi wakuu duniani karibu wote wanajua zaidi ya lugha mbili,lakini tazama popote wanapokwennda lazima atakuwepo mkalimani...na kwa desturi mtu anathamini kwanza chake ndio maana ukiwa katika nchi ya kigeni,mfano Ujerumani,Ufaransa na ukawa una shida hata kama unajua kiingereza kuliko Queen Elizabeth basi usishangae kama utakosa mtu wakukupatiliza,na hao utakao wauliza sio kuwa hawajui,miongoni mwao wengi wanaongea kiingereza wanachofanya ni kuthamini cha kwao.
 
kualikwa? Mafanikio? Kama yale yale yajk kuwa rais wa kwanza wa kukutana na obama ikulu ya white house! So what? Ongezea basi na .... Wa kwanza kualikwa na usher usa. Mitanzania bana....!

hater .....!!!!!!
 
Hongera kwa Kupanda ndege jamani ,hope Russel Simmon kwa kupitia kwa Ruge mnaweza bahatika na na label za hapo ATL.

Najiuliza huyu Brazameni haina majotro mtangazaji sijui itakaje, haswa ukizingatia huko ATL ni kinda like a Chocolate city ,wale ma handsome boyz wa jiji hilo, sijui jama ata data kiasi gani, maana anavyo penda ma handsome boys, sasa hapo ndio peponi kwa ma handsome light skined dudes wa ukweli, na dhani ata data kinoma, kama huku tuu TZ msanii yeyete akiwa handsome tuu jamaa amesha jiweka karibu yake, hehehehehee!
 
Back
Top Bottom