Wasanii 13 wa taarab wafa ajalini

Kuna tetesi kwamba kundi la 5 * taarabu wamepata ajali huko kibaha na inasadikika robo ya watu wamekufa..!!

Source: clouds fm

Inaumiza kwa kweli, kifo cha ghafla jamani! Mungu tusaidie tuwe tayari wakati wote.
 
Idadi ya marehemu 13 majeruhi 9 majina bado, ZENA MOHAMED ALLY JUMA RAJABU KOMBO MWANAHAWA NA SHABANI HAMIS ndio miongoni mwao, weka mkato kila baada ya majina mawili na walitokea Kyela, maiti zimeharibika sana maana walichanwa na mbao baada ya coaster hii kuigonga lorry hilo kwa nyuma, sehemu ni DOMA-.MIKUMI: Source: WAPO RADIO na imethibitishwa na kamanda wa usalama barabarani morogoro

Bi Mwanahawa Ali ni mzima amelazwa tu katika Hospitali ya Morogoro na hali yake ni inaendelea vizuri na asubuhii hii nimeongea nae na imetumwa gari na wanae kuchukua huko kumleta Dar. Tunategemea Inshallah mchana atakuwa Dar kwa uchunguzi zaidi.

Mungu waweke pahala panapo stahikhi waiti wote
 
speed zinaendelea kutumaliza jamani ..Vijana wadogo na machachari katika ulimwengu wa muziki wa mipasho wametutoka
Very sad:shock::shock::pray::pray::pray::pray::pray:RIP
 
Wana jf, watu wamepata ajali mnaleta siasa! Hivi kuna akil hata tone hapo. Mnachobishania ni kitu gani? Tuwe wastarabu.
 
Kikundi cha taarabu cha Five Stars kimepata pigo baada ya kufiwa na jumla ya wanakikundi 10,
wakiwemo waimbaji, mafundi mitambo na mkurugenzi wa bendi. Katika ajali ya gari iliyotokea usiku
wa kuamkia leo Mikumi, Mkoani Morogoro, wakitokea Kyela,Mbeya ambako walikuwa na ziara ya
kimuziki. Katika ajali hiyo, alikuwemo pia mwimbaji mkongwe Mwanahawa Ally ambaye alinusurika
baada ya kuumia vibaya, aliungana nao kama mwimbaji mwalikwa akitokea Melody ModernTaarab. Pia
mwanamuziki mwingine mahiri, Hammer Q, ambaye alikuwepo kwenye msafara, alinusurika baada ya
kubaki Iringa wakati wenzake wakiendelea na safari.. Yafutayo ni majina ya wana Five Stars waliothibitishwa kufa hadi sasa:

Issa kijoti - mwimbaji
Husna mapande-mwimbaji
nasoro madenge - mkurugenzi
Sheba juma - mpiga solo
Omari hashimu- mpiga bass
Omari tall- fundi mitambo
Hamisa mussa - mwimbaji
Rama kinyoya - mwimbaji
Tizo mgunda - mcheza shoo
Haji mzaniwa - fundi mitambo
 
AJALI mbaya ya aina yake kuwahusisha wasanii, imesababisha vifo vya wasanii 13 wa kundi la muziki wa taarabu la Five Star’s Modern Taarab na kujeruhi wengine saba.
Miongoni mwa waliofariki wamo wanaume kumi na wanawake watatu na wengine saba kujeruhiwa kati yake mmoja vibaya katika ajali iliyohusisha gari yao aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 351 BGE iliyokuwa ikiendeshwa na J
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Adolfina Chialo, akiongea na majeruhi wa ajali ya wanamuziki wa Five Star’s Modern Taarab.

uma Hassan aliyesalimika na kutoroka.
Imeelezwa kwamba ajali hiyo imetokea baada ya gari lililobeba wasanii hao wakitokea Mbeya, kuelekea jijini Dar es salaam kuacha njia na kulivaa lori lililokuwa limesimama na kupinduka kabla ya kulikwepa na kukutana uso kwa uso na lori lililokuwa likija mbele yao.
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro Ibrahim Mwamakula, aliwaambia waandishi wa habari mjini Morogoro kwamba ajali hiyo ilitokea Jumatatu ya Machi 21, saa 2.30 usiku, ndani ya eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, kilometa karibu sita kutoka lango kuu la kuingilia hifadhi hiyo kutoka upande wa Dodoma.
Kwa mujibu wa Mwamakula aliyefika eneo la tukio na hospitali kusaidia kuhifadhi miili ya watu hao, chanzo cha ajali hiyo ni Mwendo kasi wa gari hiyo aina ya Costa iliyokuwa imewabeba wasanii na uzembe wa dereva Juma kujaribu kulipita gari jingine bila kuwa na uangalifu.
Ajali hiyo ilitokea baada ya Costa hiyo kujaribu kulipita lori aina ya scania lililokuwa limebeba mbao lililokuwa limesimama barabarani baada ya kuharibika lenye namba za usajili T848 APE na tela namba T 556 BDL mali ya Meshack Rajab Mvamba, na kukutana mbele yake na lori aina ya scania lenye namba T 182 BKB na tela namba T 530 BHY ambalo katika kuikwepa Costa hiyo na lenyewe lilipinduka.
Aidha Costa hiyo ilichuna upande mmoja wa lori la mbao, na lenyewe kuharibika upande huo vibaya na kupinduka.
Raisi wa bendi hiyo Ally Juma (25) maarufu kama “Ally J” ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika, alisema gari hiyo ilikuwa na watu 24 wakiwemo wasanii 21, madereva wawili na abiria mmoja, na walikuwa wakitokea Mkoani Mbeya kwenye maonesho ambapo Jumapili walifanya wilayani Kyela mkoani humo na kabla, siku ya Ijumaa walifanya maonesho Makambako, Mikumi siku ya alhamisi na Kilosa Mkoani Morogoro siku ya jumatano. Miongoni mwa waliopoteza maisha yumo mwanamuziki Issa Kijoti na kiongozi wa bendi hiyo Nassoro Madenge ambaye ndugu, jamaa na marafiki zake walijitokeza kwa wingi usiku huo katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro wakitokea jijini Dar es salaam,na kukesha hadi majira ya saa 10 alfajiri wakiendelea kusaidia zoezi la kushusha miili iliyokuwa imeharibika vibaya kwa kuchanwa na kukatika baadhi ya viungo.
Wengine waliokufa ni waimbaji wa bendi hiyo Husna Mapande na Hamisa Omary ambaye ni mke wa msanii Mussa Mipango, mpiga solo Shebe Juma, mpiga gitaa la base Omary Hashim, mbeba vyombo Omary maarufu kama Toli, Mfanyakazi wa bendi hiyo Ngereza Hassan, wapiga kinanda Tizzo Mgunda na Hamma Kinyoya, mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Maimuna na mcheza shoo wa kundi la “Kitu Tigo” la Ilala ambaye jina lake halijaweza kujulikana mara moja na hao wote walikufa papo hapo katika eneo la ajali.
Mwingine aliyekufa akipelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu ni Haji Mzaniwa (32) mkazi wa jijini Dar es salaam ambaye ni mbeba vyombo katika bendi hiyo.
Majeruhi katika ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro ni pamoja na mwimbaji Mkongwe na mgeni aliyekuwa amefanya onesho moja tu katika bendi hiyo, Mwanahawa Ally (55), Suzana Benedict (32),Zena Mohamed (27), Samila Rajab (22), Ally Juma (25), Rajab Kondo (25), Mwanahawa Hamis (38), Shaban Hamis (41) na Msafiri Mussa (22) wote wasanii na wakazi wa jijini Dar es salaam.
Ajali hiyo ilisababisha msururu mrefu wa magari zaidi ya 100 yakiwa yamekwama katika pande zote za njia na kushindwa kupita upande mmoja kwenda mwingine kutokana na ajali hiyo kuzuia njia, huku jitihada za kuwaokoa maiti waliokuwa wamenasa katika Costa hiyo zikiendelea kufanywa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Mikumi, watu waliokuwa ndani ya magari yaliyoshindwa kupita na askari polisi waliofika muda mchache baadaye wakiongozwa na Mwamakula.


Source:
Wasanii 13 wa taarab waliokufa ajalini watambuliwa | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

UA:F [1.9.7_1111]
 
pole sana wafiwa.

Kwa turiobaki barabara za Tanzania hazifai narudia tena hazifai kuendesha 120km/h, tena kwa usiku ndiyo hatari kubwa sana unless maisha yako huyataki.

mbishe msibishe huo ndiyo ukweli, Majonzi tunayo ila ukweli lazima tuambiane na hili linajulikana hata Tanrods wenyewe wanapendekeza 80km/h max.
 
IMG_6617.JPG


Walio pona kwa kweli Mungu mkubwa
 
Back
Top Bottom