Wasanii 10 wa filam na Muziki wenye mafanikio Bongo

jamani ivi kuwa na nyumba ni utajiri, hiyo si basic needs??? lol basi na mie tajiri na kibanda changu chanikaaaaa
 
Jana kwenye clouds tv wametoa majina kumi ya wasanii wenye mafanikio Bongo kwenye muziki na filamu. Majina ni kama ifuatavyo.

1. Mzee Yusuf
2. Lady Jay dee
3. Kanumba
4. Ray
5. Rose mhando
6. Professa Jay
7. AY
8. Diamond
9. JB
10. Ali kiba

Kwa ukweli sijui wametumia vigezo gani haswa labda kama ni ukongwe/umaaraufu/pesa/heshima/mchango etc hawakubainisha wazi.
Kwa ku-assume vigezo vyote hivyo au kimojawapo kwa maoni yangu nahisi kuna wasanii waliostahili zaidi kuwepo top 10 lakini hawajawekwa, mfano Mr. II . Hakuna ubishi katika wasanii wote wa kizazi kipya huyu bwana kapata mafanikio kuliko wasanii wote, mchango wake kwa muziki wa kizazi kipya, kwa wingi wa albamu alizitoa na mafanikio zaidi alipoutwaa uheshimiwa, huyu alistahili kuwepo kwenye top 10! Wasanii wengine ambao nahisi nao walistahili kuwepo top 10 ni Monalisa, Juma Nature, Ray C, Khadija Kopa, Kapteni John Komba

Unaonaje wewe hiyo list ya clouds? Msanii gani hakustahili kabisa kuwepo top 10, na msanii gani alistahili zaidi kuwepo top 10? na wewe je unaweza kutupa top 10 yako ya wasanii 10 wenye mafanikio Bongo?

Wolper ametoa USD 10,000 na asiwepo hapa???
I need my head examined???
 
Wolper ametoa USD 10,000 na asiwepo hapa???
I need my head examined???

tetesi zinadai wolper sio pesa zake alizotoa, zile ni pesa za mchumba aliyempata, ambaye huyo mchumba inasemekana ana pesa ile saana,
In short nabaki suprise wametumia vigezo gani , hivyo vigezo vilivyomuweka mzee yusuff kuwa no. 1 !!!
 
jamani eh huyo mzee yusuf anastahili namba moja nakaa nyumbani huku ana scania kama uchafu!nyumba ndo ucseme!maduka kibao!hotel 3 star mbili!ila huwa apendi kujisifia
 
tetesi zinadai wolper sio pesa zake alizotoa, zile ni pesa za mchumba aliyempata, ambaye huyo mchumba inasemekana ana pesa ile saana,
In short nabaki suprise wametumia vigezo gani , hivyo vigezo vilivyomuweka mzee yusuff kuwa no. 1 !!!
Huyu jamaa hata kama ni mafanikio ya hela alitakiwa kuwa nayo maana ana vitu vingi sana vinavyohusiana na mziki, anapiga vyombo vya mziki takribani vyote, anatunga nyimbo, anaghani, anaimba na bado anamiliki bendi, kwa hiyo kama kawa wa kwanza mimi sishangai. Kwa kifupi Mzee Yusuf ni full vipaji acha awe na mafanikio.
 
tetesi zinadai wolper sio pesa zake alizotoa, zile ni pesa za mchumba aliyempata, ambaye huyo mchumba inasemekana ana pesa ile saana,
In short nabaki suprise wametumia vigezo gani , hivyo vigezo vilivyomuweka mzee yusuff kuwa no. 1 !!!

wapo watu wanadai wolper yupo fremason
 
Ushauri wangu, twende tra tukaangalie nani anaongoza, otherwise tutakuwa tunazinguana tu, wengine wana za unga wengine za kuongwa wengi za kuazima!
 
wapo watu wanadai wolper yupo fremason

UTAJIRI WA HARAKA WATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, tangu Wolper amejiunga na imani hiyo inayosambaa kwa kasi nchini Tanzania amekuwa akipata mafanikio makubwa tena kwa haraka.
"Wee kama unataka kuamini, angalia tangu mwaka huu (2012) umeanza, Wolper mambo yanamyookea tu. Awali alikuwa akiishi eneo ambalo halimfai kama staa, sasa amehamia Mbezi, tena kwenye jumba zuri sana," alisema mtoa habari huyo.
Aliendelea kuweka wazi kuwa, magari na miradi mingine aliyonayo si ofa kutoka kwa mchumba wake aitwaye Abdallah Mtoro ‘Dallas' kama anavyodai mwenyewe Wolper bali ni ‘baraka' ya Freemason.
Akasema: "Mmekuwa mkiandika eti kanunuliwa magari na mchumba wake, nani kasema? Ile ni kama njia ya kukwepea tu, lakini ukweli ni kwamba Freemason ndiyo wanambeba kwa sasa."
Akaongeza: "Wazazi wa Wolper wapo katika wakati mgumu, mama yake amepata fununu za mwanaye kujiunga na Freemason na ndugu wakamweka chini kumwonya kama ni kweli ajitoe mara moja."

source: FREEMASON... - Global Publishers

focus.gif
UHALALI WA YUPI KUWEPO TOP 10
 
kwa Diamond hapo nakubali,coz uyu dogo ana ingiza pesa ndefu sana kwa wiki....fikiria show yake moja haipungui mil tatu,kwa wiki anapiga show zisizopungua tatu na kila siku anapokea offer ya show.....je kwa mwezi anaingiza kiasi gani?
 
kwa Diamond hapo nakubali,coz uyu dogo ana ingiza pesa ndefu sana kwa wiki....fikiria show yake moja haipungui mil tatu,kwa wiki anapiga show zisizopungua tatu na kila siku anapokea offer ya show.....je kwa mwezi anaingiza kiasi gani?
Anapiga hela nyingi sana za show, but hana muda mrefu kwa game, ni miaka takribani mitatu tu toka atoke kisanii. hatuwezi jua atadumu kwa miaka mingapi kwenye peak. huyu angepewa miaka 5 labda ndio awekwe kwa list ya wasanii wenye mafanikio, kama kweli ataendelea kuwa kwenye peak ndio ingekuwa kweli anastahili.
 
Inawezekana wapo wanaozijua kuna siku watatuwekea picha,
lakini hata kama ni vibanda bado kajitahidi mkuu.

inategemea hizo nyumba zake ni za gharama ya kiasi gani-kama wangetoa na picha za mijengo yao ingekuwa jambo la maana-maana kuna nyumba na vibanda
 
Bobi Wine's Mansion



FIRE BASE NA LO!

Hawa wabongo waweke viambatanishi kama hivi sio porojo na kanga moko!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom