Wasakwa kwa kumvisha mbwa fulana ya Kikwete

SIASA zetu bana,dunia ya kwanza mbwa anathamani sana,yaani hapo kwa sehemu zingine yaani ndio umempa kura kikwete,lakini poor me kumbe kwa tanzania ni kashfa!!!!!!!!
 
Huenda walifanya kwa nia nzuri ya kupromoti chama. Mbona wanaoweka bendera kwenye makaburi na vyoo hawatafutwi?
Au hawa wanasakwa wapewe zawadi?
Mie ninawashauri wasijitokeze hadi Dr. Slaa aapishwe.
Mimi niliyeifanya tambala la kupigia deki wananitafuta pia?
Kikwete hawezi kuvaa T-shirt yenye picha ya mbwa?
Ingekuwa nguruwe hata mimi ningepigia hilo kelele.
 
uhuru wa maoni...au sio? Ni kosa la jinai kuvalisha mbwa nguo za chama cha siasa?
 
For me sioni kosa lao!! Labda ilikuwa ndo stail yao ya kufanya kampeni na ikiwa zaidi ni mbwa anaezagaa mitaani kwani ujumbe utafika kwa wengi!! Kwani CCM si wanagawa hizo t-shirt ili zivaliwe... Mbwa nae ana haki ya kuvalishwa nguo iliyoko available. Hao vijana wala wasijifiche,,,, sheria inayokataza mbwa wasivalishwe nguo ni ya kifungu gani? Hiyo t-shirt ni nguo kama nyingine na upatikanaji wake ni rahisi maana zinagawiwa bure!!! Labda hawa watu walikuwa on the way kwenda kumnunulia mbwa wao nguo, walivyokutana na mgao huo wakawa wameserve hela yao.....

Police wanawatafuta kwa kuvunja sheria gani??....
 
Tena naomba wanaotetea haki za wanyama wawashtaki hao waliokuwa wanamfukuza mbwa huyo maana hana kosa na anavyoonekana amepigwa.....
 
images




MsaniiBushokeakitumbuizauwanjawaSaharajijiniMwanza.jpg
 
T-SHIRT ZA BURE! Mtu si anahaki yakuitumia zawadi aliyopewa vyovyote apendavyo? Mnamtafuta kwa kosa gani kama kwa hiari yake ameamua kugawa zawadi yake kwa kiumbe akipendacho?
 
Where is freedom of expression? Kama mtu anasema "mimi na nyumba yangu wote CCM, hata mbwa wetu CCM" ashindwe kuji express?
This is how I looked at this issue Kiranga........yaani hapa tunaswing kwenye frequency moja.
 
Wale wanadekia hizo fulana nao wawafanyeje!! Fulana ina matumizi zaidi ya moja!!
 
Wengine wanazitumia kudekia nyumba na kufutia miguu waingiapo na kutoka ******, wengine wanazivaa kama nguo za kutokea wengine wanabebea Magunia, wengine wamezigeuza unifom za gereji. Kwa mtaji huu watakama wengi mbona? Hivi nini maana ya kumpa mtu hilo vazi? Hiyo T-shirt ishakuwa mali yake ana haki ya kuifanyia chochote jamani. Hiyo T-Shirt haina popote ilipoandikwa "vigezo na masharti kuzingatiwa" Ukishapokea hiyo T-shirt una haki ya kuifanyia chochote upendacho.
 
Hawa CCM vipi tena???

Cha ajabu hapa ni nini??T-shirt yenye picha ya Kikwete ina umuhimu gani kwa Mtanzania?? Kama yule mbwa anelikuwa amevishwa BENDERA ya Taifa hata mimi ningelaani kitendo hicho. Lakini kulalamikia T-shirt yenye picha ya Kikwete naona ni uzuzu wa CCM.
T-shirt ya Kikwete ina thamani gani kwa Mtanzania anayeshindia mlo mmoja kwa siku na hajui kesho atakula nini????Hii ni kuonyesha kuwa watu wameshachoswa na longolongo za CCM. Huo ni uhuru wa kutoa mawazo yao kwa njia kama hiyo. Mimi nawapa Big-up.
 
Hata mimi ningependa kujua watatumia sheria gani kuwashtaki hao vijana. Na hata kama hiyo sheria ipo kosa ni mbwa kuvalishwa t-shirt, au hiyo tshirt kuwa na picha ya jk? tafsiri nyingine ni kwamba vijana kikwete angewaona angewapa zawadi kwa kuwa wabunifu kama mdau alivyosema hapo juu, maana mbwa atapita na kufika sehemu nyingi sana ambazo kampeni haziwzi fika,,,si unajua tena nyumba za watu barabara hakuna! ...ughaibuni huko kuna maduka maalumu ya viwalo vya madogidogi alafu!
 
Watafutiwe wanasheria, hakuna haja ya kujificha.
Huyo Dogo wa Shule ana akili sana, Huenda darasani anakalia matofali, sasa unampa Tshirt itamsaidia nini katika elimu yake.
 
hata mimi nakubaliana na kiranga its freedom of expression!dog and the dog owner are pure chi chi m te te te te teh
 
Kwani shida iko wapi kumvika mbwa gauni au nguo ya aina yoyote? Check hizi picha za mbwa na tishet ya Obama. Kama obama anvaliwa na mbwa who is Kikwete?

080708-obamadog-vmed-9a.grid-4x2.jpg dog.jpg

Problem ni kwamba hawa polisi wetu hawajui sheria na ndio wanapenda kunyanyasa wananchi. Mfano ya polisi kupiga watu walio kwisha kukubali arrest. That is wrong and things need to change! POLISI ACHENI KUNYANYASA WATANZANIA KWA UJINGA WENU. We are free people as long atuvunji sheria.
 
Back
Top Bottom