Warombo,Wamachame,Wakibosho si wachagga

Ukisema 'wa old moshi' na 'wa moshi ya zamani' kitu ni kile kile ila lugha tu!
Ila sikubaliani na mtoa mada,ninachofahamu ni kwamba wote ni wachaga ila wanatofauti chache za kimatamshi na kimsamiati.
Hivyo kuna lahaja anuwai za Kichaga!
Mimi napinga kabila kuitwa wa old moshi, haiwezekani kwani Wakoloni wamekuja mwishoni mwa karne ya 18 na tayari kulikuwa watu wanakaa pale. Kiingereza kilikuja na ukoloni, kwa hiyo wape jina lolote wale watu lakini sikubali uwaite eti wa Old Moshi. Nakataa
 
:A S 465: huu utafitu wako mheshimiwa Makupa uko biased kwanini unawafavour wa kv!? kirua vunjo na wamarangu unakotoka wewe kuna lipi haswa la kujivunia mtu ajitambulishapo yeye ni mchaga kutoka kirua vunjo!?
:juggle:
 
Dah..kweli wachagga wako juu sana...threads za kuwajadili hazikauki JF...big up sana wachagga woteeeee. tusisahau jadi...mwezi wa kumi na mbili ndio huu twende vijijini tukawaonyeshe walio waliobaki vijijini tulikuwa tunafanya nini mjini kwa miezi yote kumi na 12. kama mwaka ulikuendea vibaya usijali nenda tuu ukapate baraka kwa wazee urudi mjini.
 
:A S 465: huu utafitu wako mheshimiwa Makupa uko biased kwanini unawafavour wa kv!? kirua vunjo na wamarangu unakotoka wewe kuna lipi haswa la kujivunia mtu ajitambulishapo yeye ni mchaga kutoka kirua vunjo!?
:juggle:
KV ndio eneo lenyes wasomi wa ngazi ya PHD kwa wingi kuliko eneo lolote Mkoani Kilimanjaro,Marungu kwa sasa is more or less mjini
 
Mi nadhani tukiwaondoa hao Watani zetu, wengine wote (Warombo, Wavunjo, Waold Moshi, Wauru, Wamachame, Wanarumu, Wasiha na Wakibosho) ni WACHAGGA. Kinachotutofautisha ni DIALECTS!
Kila jamii moja ilipokuwa inatenganishwa na nyingine na labda msitu mnene, mto mkubwa, bonde, mlima n.k, hapo huzaliwa dialect mpya ambayo si tofauti sana na Lugha Mama.
Hata desturi na mila zinafanana sana. Tofauti ni ndogo kati ya sehemu na sehemu zinazotenganishwa na mto, misitu au milima
Ina maana msitu inazalisha lugha tofauti mbona haya yatakuwa ni maajabu ya karne
 
Ndio nilisema hivyo nikiwa kama mrombo nachukia wachagga(vunjo) huwa wanajifanya kuwa ndio wasomi wa mkoa wa kilimanjaro

Nadhani hapo unamaanisha Wamarangu, kama unamaanisha hivyo mimi sidhani kama wanajifanya ila ndio ukweli wenyewe kwamba hawa waliwahi kwenda shule, na ndio maana Lord chief alikuwa ni Marlialle, na ni huyu aliktaa kupigana vita ya majimaji maana alipinga kwamba risasi haiwezi kugeuka maji kamwe. Sifa kuu ya warombo ni kuendesha mabar hapa mjini na vijana wa kirombo upande wa jikoni ndio wenyewe ukitaka supu ya ulimi , supu ya mkia, supu ya kichwa hapo kwa Warombo umefika.
Nenda Muhimbili kuna idadi kubwa ya Madaktari Wachaga lakini asilia kubwa ni Wamarangu.
 
kila siku JF haikosekani thread inayohusu wachaga!!!

Mkuu Rejao hii ndio thread ya kwanza inawahusu wachagga halisi hizo thread nyingine zilizokuwepo zilikuwa zinachanganya makabila tofauti yaani warombo,wapare,wkibosho ,wamachame you name it
 
Kutokana na utafiti wangu niliofanya mkoani kilimanjaro nimegundua ya kwamba mkoa wa kilimanjaro una makabila tofauti si chini ya saba kama ifuatavyo:wapare,wagweno,warombo,wamachame,wakibosho,wasiha,wachagga(vunjo),na wakahe.Kilichonisaidia kwenye tafiti yangu na kugundua kuwa watu wa vunjo ndio wachagga ni kwamba wanaongea lugha moja na tamaduni yao ni tofauti kabisa na hayo makabila mengine,na ikumbukwe ya kwamba jamii inaweza kujitambulisha ya kuwa wao ni kabila moja pale tu ambapo jamii husika wanaongea lugha moja na tamaduni yao ni moja.
Nawasilisha

Mkuu rudia tena utafiti wako kuhusu makabila ya Kilimanjaro umesahau kuwa kuna sizable population ya kabila la Maasai na ....pia pande za Himo kule kunatoroshwa sukari daily kuna Wakamba wa kutosha uelekeo wa Nyumba ya Mungu
 
Nadhani hapo unamaanisha Wamarangu, kama unamaanisha hivyo mimi sidhani kama wanajifanya ila ndio ukweli wenyewe kwamba hawa waliwahi kwenda shule, na ndio maana Lord chief alikuwa ni Marlialle, na ni huyu aliktaa kupigana vita ya majimaji maana alipinga kwamba risasi haiwezi kugeuka maji kamwe. Sifa kuu ya warombo ni kuendesha mabar hapa mjini na vijana wa kirombo upande wa jikoni ndio wenyewe ukitaka supu ya ulimi , supu ya mkia, supu ya kichwa hapo kwa Warombo umefika.
Nenda Muhimbili kuna idadi kubwa ya Madaktari Wachaga lakini asilia kubwa ni Wamarangu.
Wamarangu wapi hao wamesoma? au unamaanisha wakina Marealle kama huyu wa Kili marathon! kama ni huyo basi umekosea maana ana vyeti vya ku-forge! Shule hana...
 
Mi nadhani tukiwaondoa hao Watani zetu, wengine wote (Warombo, Wavunjo, Waold Moshi, Wauru, Wamachame, Wanarumu, Wasiha na Wakibosho) ni WACHAGGA. Kinachotutofautisha ni DIALECTS!
Kila jamii moja ilipokuwa inatenganishwa na nyingine na labda msitu mnene, mto mkubwa, bonde, mlima n.k, hapo huzaliwa dialect mpya ambayo si tofauti sana na Lugha Mama.
Hata desturi na mila zinafanana sana. Tofauti ni ndogo kati ya sehemu na sehemu zinazotenganishwa na mto, misitu au milima

hiyo ndo fact. Nyngne ni longolongo na porojo.
 
Mkuu Rejao hii ndio thread ya kwanza inawahusu wachagga halisi hizo thread nyingine zilizokuwepo zilikuwa zinachanganya makabila tofauti yaani warombo,wapare,wkibosho ,wamachame you name it
Kwa criteria yako ya lugha uliyotumia naona upo wrong sana! Ungeniambia labda mtu wa kwanza kuishi kwenye ardhi ya uchagani aliishi Vunjo na wengine wote ni wahamiaji, ningekuelewa kidogo. Mimi nimeishi uchagani kwa zaidi ya miaka 30. Sehemu ya Vunjo ndio wametofautiana sana,,,,,mkirua hataki kuitwa mkilema, mkilema hataki kuitwa mmarangu licha ya kwamba wote hawa ni waanjo! sasa sijui unaposema wote hawa lao moja unamaanisha nini!!
 
Wamarangu wapi hao wamesoma? au unamaanisha wakina Marealle kama huyu wa Kili marathon! kama ni huyo basi umekosea maana ana vyeti vya ku-forge! Shule hana...
Ninavyofahamu mimi Wamarangu ndio wasomi zaidi kutoka uchagani, hili liko wazi. kuhusu Marlealle hata kama hana shule lakini ana pesa na hili ndio la umuhimu na hii ndio shule namba moja kuliko zote.
 
Stuxnet yuko sahihi,hili jina old Moshi halifananii kuwa asili,inawezekana sana limekuja baada ya idea ya mjerumani kutaka kuweka mji wa Moshi kuwa eneo hilo,But wazee huwaita 'wa-mochi' na sio wa-old moshi.Natumaini wapo humu jamvini watakuja kujitetea kuwa wao ni kina nani?
 
Kwa criteria yako ya lugha uliyotumia naona upo wrong sana! Ungeniambia labda mtu wa kwanza kuishi kwenye ardhi ya uchagani aliishi Vunjo na wengine wote ni wahamiaji, ningekuelewa kidogo. Mimi nimeishi uchagani kwa zaidi ya miaka 30. Sehemu ya Vunjo ndio wametofautiana sana,,,,,mkirua hataki kuitwa mkilema, mkilema hataki kuitwa mmarangu licha ya kwamba wote hawa ni waanjo! sasa sijui unaposema wote hawa lao moja unamaanisha nini!!
Hapo kwenye RED si kweli, na unafahamu mwenyewe unachoongea hapa ni uwongo mtupu, na usishangae nimejuwaje kama umedanganya, nina Latest software ya kuwagunduwa watu waongo kama wewe.
 
Ninavyofahamu mimi Wamarangu ndio wasomi zaidi kutoka uchagani, hili liko wazi. kuhusu Marlealle hata kama hana shule lakini ana pesa na hili ndio la umuhimu na hii ndio shule namba moja kuliko zote.
taja hao wasomi wako wa Marangu kwa majina tukusaidie wanatoka wapi mmoja baada ya mwingine....maana unaweza ukawa unachanganya wachagga wa sehemu nyingine kwa kuwaita Wamarangu
 
Back
Top Bottom