Warombo,Wamachame,Wakibosho si wachagga

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
4,916
2,453
Kutokana na utafiti wangu niliofanya mkoani kilimanjaro nimegundua ya kwamba mkoa wa kilimanjaro una makabila tofauti si chini ya saba kama ifuatavyo:wapare,wagweno,warombo,wamachame,wakibosho,wasiha,wachagga(vunjo),na wakahe.Kilichonisaidia kwenye tafiti yangu na kugundua kuwa watu wa vunjo ndio wachagga ni kwamba wanaongea lugha moja na tamaduni yao ni tofauti kabisa na hayo makabila mengine,na ikumbukwe ya kwamba jamii inaweza kujitambulisha ya kuwa wao ni kabila moja pale tu ambapo jamii husika wanaongea lugha moja na tamaduni yao ni moja.
Nawasilisha
 
Unaonaje hii ... Kilimanjaro hakuna wachagga, wako kwa majina uliyoyatoa ... hata hao uliowaita wachagga ni wa Vunjo! ... Cha msingi wote ni Watanzania!
 
Wachaga maanake ni muunganiko wa makabila zaidi ya manne yenye lugha tofauti zenye ufanano wa karibu na yanayopatikana katika mkoa mmoja wa kasikazini.
 
kuna wanarumu pia ambao mmachame haambulii hata neno moja kuna wengine kiruuuuuu ni tusi wengine ni mshangao kuhusu wagweno ni wapare sema wanabana pua
 
Kwa mtazamo wako Makupa si hao tu bali kuna wa-Uru na wa-Old Moshi. Ni vizuri utambue kuwa si Wachaga tu Makabila yote ya vikabila vidogo vidogo ndani yake (clans) ambavyo huwa kuna tofauti hata za baadhi ya maneno.
Ukitoka hapo Makupa, utakuta hakuna Wakristo basi, bali WaRc, Walutheri, Waanglikana, Wasabato, nk
 
Mi nadhani tukiwaondoa hao Watani zetu, wengine wote (Warombo, Wavunjo, Waold Moshi, Wauru, Wamachame, Wanarumu, Wasiha na Wakibosho) ni WACHAGGA. Kinachotutofautisha ni DIALECTS!
Kila jamii moja ilipokuwa inatenganishwa na nyingine na labda msitu mnene, mto mkubwa, bonde, mlima n.k, hapo huzaliwa dialect mpya ambayo si tofauti sana na Lugha Mama.
Hata desturi na mila zinafanana sana. Tofauti ni ndogo kati ya sehemu na sehemu zinazotenganishwa na mto, misitu au milima
 
wakahe unawajua? Kakabila flan kadogo sana,ndo nitokako mie,sifa yao kubwa ni uchawi,though cjawah kushuhudia bali naambiwa,wanaishi tambarare sana na sikule miliman!
 
Ndg Nyagi,
Wakahe na Wauru naona ni kitu moja tu.
Yale yalikuwa maeneo ya Wauru ya kulima. Wenyewe wanaita "nuka"; nahisi maana yake ni "porini".
 
Pamoja na kautafiti mwitu ulichofanya,bado kuna mambo mengi huelewi,endelea kujifunza kutoka kwa wadau kama alivyokueleza Nkundaruwa Dialects ndiyo point,kuwa na dialects tofauti hakufanyi kabila kuwa tofauti.Juu ya wakahe kutokana na simulizi za watu,wa-kahe ni kundi dogo lililotokana na watu waliokimbia kwao kutokana na kutengwa au kukimbia kwao kwa sababu mbalimbali wakaenda kuishi(kujificha)tambarare,ndio maana koo zao ni mchanganyiko utakuta koo za asili ya kibosho,old moshi,uru nk kutegemea alikimbia kutoka wapi.
 
Si kweli hatuwezi kuwa na kabila lenye jina la Kiingereza 'Wa Old Moshi". No this is awkward na ni namna ya kuwadharau hao watu wanaotoka hapo. Labda mukiniambia wa Moshi ya Zamani nitakubali lakini hata munichune ngozi Old Moshi si kabila
 
Mi nadhani tukiwaondoa hao Watani zetu, wengine wote (Warombo, Wavunjo, Waold Moshi, Wauru, Wamachame, Wanarumu, Wasiha na Wakibosho) ni WACHAGGA. Kinachotutofautisha ni DIALECTS!
Kila jamii moja ilipokuwa inatenganishwa na nyingine na labda msitu mnene, mto mkubwa, bonde, mlima n.k, hapo huzaliwa dialect mpya ambayo si tofauti sana na Lugha Mama.
Hata desturi na mila zinafanana sana. Tofauti ni ndogo kati ya sehemu na sehemu zinazotenganishwa na mto, misitu au milima

Uko sawa mkuu.

Dialects=Lahaja.
 
Wote hao wanatambulika na jamii zingine nje ya kilimanjaro kama wachagga sasa machame, kibosho, marangu au rombo ni udambu udambu (mbwe mbwe tu).
Ndio maana nyerere alionya ubaguzi na dhambi zake
 
Mimi napinga kabila kuitwa wa old moshi, haiwezekani kwani Wakoloni wamekuja mwishoni mwa karne ya 18 na tayari kulikuwa watu wanakaa pale. Kiingereza kilikuja na ukoloni, kwa hiyo wape jina lolote wale watu lakini sikubali uwaite eti wa Old Moshi. Nakataa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom