Warning: Uzushi kuhusu hayati Chacha Wangwe na Deus Mallya ukome!

Ni Mimi Msiogope

JF-Expert Member
May 28, 2012
352
200
Salaam!
Mnamo Tarehe 5/03/2012 Mahakama ya Rufani Dodoma ilitoa hukumu ya Rufaa kati ya DEUS MALLYA v/s JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (Criminal Appeal no. 52/2010). Hukumu hiyo iliyopinga maamuzi ya Criminal Appeal no.34/2009 iliondoa Hatia na hukumu zote za awali zilizomtia hatiani Ndg.DEUS MALLYA juu ya makosa aliyoshtakiwa nayo na kutiwa nayo hatiani ambayo yalikuwa ni.

(i) Causing Death throug dangerous Driving
(ii) Driving a motorvehicle without a valid driving licence.
Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la Majaji watatu ambao ni.
1.The Honourable Mr. Justice H.R. Nsekela - JA
2.The Honourable Madame Justice N.P. kimaro - JA
3. The Honourable Mr. Justice B.M. Luanda - JA

Kwa muda mrefu sasa tumeshuhudia wanasiasa uchwara wakiendelea kunasibu tatizo la kifo cha Hayati Wangwe (R.I.P) kwa namna wanavyotaka. Pia vijana wepesi wa hoja na masikini wa kufikiri wamekuwa wakitumia msiba ule hadi leo kwa mambo ya hovyo hovyo!..

Ni busara kama mtu akikosa cha kuandika ajisomee vitabu au alale badala ya kuendelea na upotoshaji usiokubalika katika jamii ya kistaarabu.
 
"IT IS ORDERED The proceedings are declared a nulity. Consquently, the Appellant is set free from prison unless he is held for other lawful purposes"

Imenukuliwa sehemu ya hukumu hiyo yenye kurasa 10
 
Salaam!
Mnamo Tarehe 5/03/2012 Mahakama ya Rufani Dodoma ilitoa hukumu ya Rufaa kati ya DEUS MALLYA v/s JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (Criminal Appeal no. 52/2010). Hukumu hiyo iliyopinga maamuzi ya Criminal Appeal no.34/2009 iliondoa Hatia na hukumu zote za awali zilizomtia hatiani Ndg.DEUS MALLYA juu ya makosa aliyoshtakiwa nayo na kutiwa nayo hatiani ambayo yalikuwa ni.
(i) Causing Death throug dangerous Driving
(ii) Driving a motorvehicle without a valid driving licence.
Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la Majaji watatu ambao ni.
1.The Honourable Mr. Justice H.R. Nsekela - JA
2.The Honourable Madame Justice N.P. kimaro - JA
3. The Honourable Mr. Justice B.M. Luanda - JA

Kwa muda mrefu sasa tumeshuhudia wanasiasa uchwara wakiendelea kunasibu tatizo la kifo cha Hayati Wangwe (R.I.P) kwa namna wanavyotaka. Pia vijana wepesi wa hoja na masikini wa kufikiri wamekuwa wakitumia msiba ule hadi leo kwa mambo ya hovyo hovyo!.. Ni busara kama mtu akikosa cha kuandika ajisomee vitabu au alale badala ya kuendelea na upotoshaji usiokubalika katika jamii ya kistaarabu.
Nilifikiri kwa hilo la kuendesha gari bila valid driving license lingemtia hatiani. Hata hivyo Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. Tumeshuhudia wauaji wa Kombe wakisamehewa na rais na kupewa mitaji ya kusukumia maisha. Sitashangaa kama Mallya naye kawezeshwa.
 
Ninawajibika kuendelea kukushangaa unavyozidi kubishana na kivuli.
Kwanza hukuwepo kwenye shauri hilo.. Hujui kilichojiri tofauti ya kusoma kwenye magazeti (Hasa ya Udaku). Kwa kukusaidia Deus Mallya hakuulizwa kuhusu kosa hilo wala hakuletwa shahidi hata mmoja kuthibitisha kosa hilo la kutokuwa na leseni. Mwisho hilo neno 'Wauaji' ni zuri kumtamkia mwenzio.. Ipo siku utatamkiwa wewe tuone utakuwa kwenye hali gani.
 
"IT IS ORDERED The proceedings are declared a nulity. Consquently, the Appellant is set free from prison unless he is held for other lawful purposes"

Imenukuliwa sehemu ya hukumu hiyo yenye kurasa 10

Ahsante mkuu kwa taarifa. Hata mimi nilikuwa sina habari kwamba Deus Mallya alikata rufani na kushinda na sasa hivi is a FREEMAN.

Tunajua wanaopenda kutumia uzushi huu .... Si umeona sms eti "alizotumiwa" Nchemba?
 
Ninawajibika kuendelea kukushangaa unavyozidi kubishana na kivuli.
Kwanza hukuwepo kwenye shauri hilo.. Hujui kilichojiri tofauti ya kusoma kwenye magazeti (Hasa ya Udaku). Kwa kukusaidia Deus Mallya hakuulizwa kuhusu kosa hilo wala hakuletwa shahidi hata mmoja kuthibitisha kosa hilo la kutokuwa na leseni. Mwisho hilo neno 'Wauaji' ni zuri kumtamkia mwenzio.. Ipo siku utatamkiwa wewe tuone utakuwa kwenye hali gani.
Kwa hiyo hapa unachotaka kutuambia ni kwamba polisi au waendesha mashtaka walizembea na hawakutoa ushahidi kwamba mshtakiwa hakuwa na leseni? Kama ni hivyo basi, Gagnija anayo point. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Salaam!
Mnamo Tarehe 5/03/2012 Mahakama ya Rufani Dodoma ilitoa hukumu ya Rufaa kati ya DEUS MALLYA v/s JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (Criminal Appeal no. 52/2010). Hukumu hiyo iliyopinga maamuzi ya Criminal Appeal no.34/2009 iliondoa Hatia na hukumu zote za awali zilizomtia hatiani Ndg.DEUS MALLYA juu ya makosa aliyoshtakiwa nayo na kutiwa nayo hatiani ambayo yalikuwa ni.
(i) Causing Death throug dangerous Driving
(ii) Driving a motorvehicle without a valid driving licence.
Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la Majaji watatu ambao ni.
1.The Honourable Mr. Justice H.R. Nsekela - JA
2.The Honourable Madame Justice N.P. kimaro - JA
3. The Honourable Mr. Justice B.M. Luanda - JA

Kwa muda mrefu sasa tumeshuhudia wanasiasa uchwara wakiendelea kunasibu tatizo la kifo cha Hayati Wangwe (R.I.P) kwa namna wanavyotaka. Pia vijana wepesi wa hoja na masikini wa kufikiri wamekuwa wakitumia msiba ule hadi leo kwa mambo ya hovyo hovyo!.. Ni busara kama mtu akikosa cha kuandika ajisomee vitabu au alale badala ya kuendelea na upotoshaji usiokubalika katika jamii ya kistaarabu.
wanataka kuleta ishu ya kwamba majaji hawakuwa fair walipotoa hukumu ilhali upande wa pili wanasema majaji wanauwezo na uzoefu wa kutosha ilimradi tu kupinga hoja ya lissu......hawa jamaa ni kizunguzungu sana.....
 
Ahsante mkuu kwa taarifa. Hata mimi nilikuwa sina habari kwamba Deus Mallya alikata rufani na kushinda na sasa hivi is a FREEMAN.

Tunajua wanaopenda kutumia uzushi huu .... Si umeona sms eti "alizotumiwa" Nchemba?

Nimeusoma ule uchafu!
Ni wazi kuwa aliyeandika awe mwanamke au mwanaume Ubongo wake haujai kwenye kikombe cha kahawa.
 
Kwa hiyo hapa unachotaka kutuambia ni kwamba polisi au waendesha mashtaka walizembea na hawakutoa ushahidi kwamba mshtakiwa hakuwa na leseni? Kama ni hivyo basi, Gagnija anayo point. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.

Skia bro (Am nt sure kama ni ME au KE).
Polisi baada ya kugundua kuwa waliropoka bure kwenye vyombo vya habari na kuandika hati ya mashtaka kuwa Deus Mallya hakuwa na Leseni ilhali alikuwa nayo (Hawakumuuliza) Wakaamua kukaa kimya hadi ilipokuja kuamuliwa mahakamani.. Hata hivyo walifungua kesi hiyo maksudi wakijua kosa likiwa moja tu (1st count) hukumu itakuwa ni Faini na si kumpeleka Jela (Pengine kama ilivyolengwa)

Toka huko nyuma ya pazia uliko!
 
wanataka kuleta ishu ya kwamba majaji hawakuwa fair walipotoa hukumu ilhali upande wa pili wanasema majaji wanauwezo na uzoefu wa kutosha ilimradi tu kupinga hoja ya lissu......hawa jamaa ni kizunguzungu sana.....

Kuna watu wameamua kuwa Wapotoshaji tu!
Wanabishana na mahakama na majaji wa mahakama ya Rufani.
 
nashukuru kwa taarifa maana mwigullu kashaanza kutumia jina la wangwe kujipa umaarufu

Naona ana bidii kweli kweli!... Nimeanza kufutilia alama zake za ufaulu kwenye uchumu anaodai alisoma manake msomi yeyote (hata kama alisoma sanaa) hawezi kutunga mashairi ya taarabu vile!..

Shame!.
 
Kwa hiyo hapa unachotaka kutuambia ni kwamba polisi au waendesha mashtaka walizembea na hawakutoa ushahidi kwamba mshtakiwa hakuwa na leseni? Kama ni hivyo basi, Gagnija anayo point. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.

...

Umeona ee?

Mie naunganisha nukta zaidi, kama cdm wangekuwa na influence namna kwenye mahakama zetu na mapolisi wetu, Lema

asingevuliwa ubunge!

Ni serikali pekee yenye uwezo huo.!!!

.
 
Maamuzi ya mahakama si kila wakati yanaweza kupindishwa kwa nguvu za mtu! Ushahidi ukiwa clear majaji watatu si wajinga wala wa kuyumbishwa kama unavyodhani.. Hata hivyo sikulazimishi kutoka huko nyuma ya pazia.. Baki huko huko ili baadaye umshukuru atakayekutoa huko kwa vibao na bakora za makalioni.
 
Unachosema ni kitu cha Busara sana, afadhali mtu asishiriki kutoa maoni yoyote kama hana la maana la kusema, lakini kujenga tuhuma sizo na msingi wowote inakuwa uchochezi na mzizi wa kuwatenganisha watanzania. ukiwa mshabiki wa CDM au CCM nyote ni watanzania na tuna haki sawasawa.

Mtu huwezi kuongoza nchi kwa uongo.
 
Maamuzi ya mahakama si kila wakati yanaweza kupindishwa kwa nguvu za mtu! Ushahidi ukiwa clear majaji watatu si wajinga wala wa kuyumbishwa kama unavyodhani.. Hata hivyo sikulazimishi kutoka huko nyuma ya pazia.. Baki huko huko ili baadaye umshukuru atakayekutoa huko kwa vibao na bakora za makalioni.

Mh,

..

Kumbe weye gamba! hilo povo la kufikiria mtu atandikwe viboko makalioni ni dalili ya pili kuwa umekasirika sana kiasi

ambacho ungeniona live ungeweza kuning'oa kucha na meno kwa tupa!!

Sasa ukisema ushahidi ukiwa clear, watu wanawezaje kuhusisha kifo kile na cdm!?

Nyambaff!!

.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom