Warning Alarm: Hili ni Onyo kwa CCM Msiposikia msiseme hatukuwashauri!!

NCHI yetu kwa sasa imekosa watu wenye hekima serikalini na chama Tawala.chuki hizi za vijana zina sababu yake.sehemu kubwa ni kutotimiza matarajio ya vijana.kuna viongozi wamejilimbikizia mali kupindukia vijana wanaona na wengine wanasikia! kuna viongozi hawafanyikazi zaidi ya kuzurura,vijana wanaona. kuna viongozi wamehodhi kila fursa nzuri kwaajili yao na watoto wao vijana wanaona! kuna viongozi wanajiona ni miungu watu,vijana wanawaona kwa kujisikia kwao! kuna viongozi wanachezea maisha ya wenzao vijana wanawaona,MWISHO WA YOTE NDIO HIZI CHUKI ZA WAZIWAZI!!!
Kwakuwa hatuna watu wenye hekima, walioko kwenye system watapuuza kwakusema hao ni wajinga wachache wa kwenye mitandao.wanasahau hata wasiongia kenye mitandao huonesha hasira zao kwenye mikokoteni, magari kwa kusema iko siku, yote yana mwisho etc.
 
sanga malua hata Gaddafi alisema hawezi kusumbuliwa na Panya, lakini matokeo yake ni yeye ndio alikwenda kujificha kwenye mtaro kama panya, na kuwaachia Hekalu panya wakigonga champagne.
 
Ndugu Members wa JF kuna kitu nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu, lakini nadhani sasa kutoka ndani ya nafsi yangu napaswa kuwashauri CCM hili walifanyie kazi haraka kwa maslahi ya Taifa otherwise hapa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ni kitu kisichoepukika bali ni kama timer bomb tu.

Kama wengi mlivyopata taarifa kwamba Mkuu wa Wilaya ya Serengeti amefariki mchana huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, sasa kinachonisukuma mimi kuleta thread hii hapa ni kitendo cha vijana wengi kwenye mitandao mbalimbali kuonesha kufurahiswa na kifo cha DC huyu kwa maelezo tu eti ni Gamba limepunguwa!!

Sasa basi nachukuwa fursa hii kuiomba CCM ichukuwe hatua hata za Dharura maana naona kuchukiwa huku kwa CCM ni kwa kiwango cha juu ambapo sijawahi kushuhudia watu hasa vijana kuichukia CCM kwa viwango hivi, na kama mtakumbuka Watanzania kwenye misiba huwa tunaweka itikadi kando, lakini sivyo ilivyo hivi sasa.

Huu ni mfano tu ukipita kwenye kurasa mbalimbali za kisiasa za vijana hasa huko uso kitabu, na kulwe karibu wote ni verified user.

Gulam Mhedu


Breaking News : Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,Kapteni Mstaafu James Yamungu amefariki dunia mchana huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Bugando Mwanza.


y-2LR9eyI1L.gif
· · · about an hour ago via mobile


unaona mbali sana ndugu ila wenye akili fupi hawatakuelewa chuki inapozidi binaadamu hufanya chochote anachofikiria.ila nisiwe mnafiki mimi ni mmojawapo wa wanaofurahia vifo vya viongozi wa hovyo,mfano meles zenawi iweje leo asifiwe ingali watu wengi sana wapo jela kwa ajili yake.narudi kwenye mada,hii chuki na huku kutokujali kwa viongozi wetu kutapelekea wananchi kuchoka na wakichoka tu ni machafuko.jana madale wananchi walikuwa wanakabiliana moja kwa moja na polisi kitu ambacho sio kawaida kwa tanzania ila watu wanachukulia kawaida tu big up sana.
 
NCHI yetu kwa sasa imekosa watu wenye hekima serikalini na chama Tawala.chuki hizi za vijana zina sababu yake.sehemu kubwa ni kutotimiza matarajio ya vijana.kuna viongozi wamejilimbikizia mali kupindukia vijana wanaona na wengine wanasikia! kuna viongozi hawafanyikazi zaidi ya kuzurura,vijana wanaona. kuna viongozi wamehodhi kila fursa nzuri kwaajili yao na watoto wao vijana wanaona! kuna viongozi wanajiona ni miungu watu,vijana wanawaona kwa kujisikia kwao! kuna viongozi wanachezea maisha ya wenzao vijana wanawaona,MWISHO WA YOTE NDIO HIZI CHUKI ZA WAZIWAZI!!!
Kwakuwa hatuna watu wenye hekima, walioko kwenye system watapuuza kwakusema hao ni wajinga wachache wa kwenye mitandao.wanasahau hata wasiongia kenye mitandao huonesha hasira zao kwenye mikokoteni, magari kwa kusema iko siku, yote yana mwisho etc.
wanajiona wamesimama wakati kimsingi wameshaanguka lakini naongezea tu mwisho utafika tu na utakua mbaya sana.have word like then have original like.
 
kama alikuwa hausiki na uchakachuaji wa kura za watu then RIP Mku wa Wilaya
Wakuu wa Wilaya wote kuharibu na kuchakachuwa kura ndio kazi yao kuu waliyopewa na CCM huko Mawilayani maana hawana kazi nyingine yoyote.
Kazi zote za maendeleo ya wilaya zote ni jukumu la Halmashauri za Wilaya husika.
 
mimi natamani magamba yote yangeanguka na kufa siku moja. Nampongeza jamaa anayesema kuwa jambazi likifa je utalia? Yangefuata mengine yote kabla ya mwisho wa mwaka huu.
 
Hakuna kitu kama CCM ambacho ni hai hapa Tanzania ila kuna genge la wajanja wakichanganyika na wajuaji ana wajinga wameshikana mikono kwa nguvu wanaogopa wakiachiana tu wote watazama. Hawa ndiyo wanajiita CCM. Hamuwezi mkawa viongozi wa kamati moja halafu hamuongei, mtafanya kazi kweli??? Kushangilia kifo ni uchuro aliyekufa ni individual na sisi tatizo letu ni mfumo wa hili genge linalojiita CCM ambalo limebeba mpaka watu wema ambao hawana ushujaa tu wa kusema basi naachana na wahuni hawa
 
Tupingane lakini tusipigane. Tunataka CCM iwe chama cha upinzani kwa angalau miaka kumi ili wajirudi. Wana CCM ni Watanzania wenzetu, ni ndugu zetu. Hatutaki wafe, tunataka wasing'anganie madaraka mno. Uchu wao wa madaraka unatuchosha, lakini akifa mmoja wao bado ni amekufa Mtanzania mwezetu, binadamu mwenzetu. Lazima tusikitike na tumwombe Mungu amwonee HURUMA
.......[/QUOTE]

Watanzania tuache longolongo.Ninachojuwa Mageuzi duniani kote huanza kwa kudaiwa kwa hoja na kukaa mezani au kutekeleza demokrasia, ikishindikana hatua ya pili yanafuata maandamano na migomo, ikishindikana inafuata hatua ya tatu ambayo ni uadui na vita.

Na katika hatua mbili za kwanza kinachopingwa ni mitazamo, mawazo, sera na tabia za mtu/watu, na kinachotakiwa kutekelezwa ni mitazamo, mawazo, sera na tabia za watu na si watu.

Lakini katika hatua ya tatu kinachopingwa ni mtu/watu, na kinachotakiwa kuteketezwa ni mtu/ watu.

Mfano mzuri angalia Libya na Misri wakati Misri wameishia katika hatua ya pili, Walibya wameenda mpaka ya tatu na mtu waliyemuona kuwa ndio adui ameuwawa.

kwa nini walibya wasingemuacha Gadafi waseme kuwa tunachochukia ni siasa zake na yeye kuwa madarakani na si kuwa tunamchukia yeye?

Ni kwa kuwa walishakuwa maadui na sio siasa tena. hata katika vita ikiwa mazungumzo yameshindikana kinachofuata ni kuuana.

Mleta hoja ameitahadharisha CCM kuwa wakiona hivi (mtu anakufa watu wanashangilia) wajue kuwa tunakaribia kizingiti cha hatua ya tatu. and thats reality
.
 
Back
Top Bottom