Warning Alarm: Hili ni Onyo kwa CCM Msiposikia msiseme hatukuwashauri!!

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,325
92,480
Ndugu Members wa JF kuna kitu nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu, lakini nadhani sasa kutoka ndani ya nafsi yangu napaswa kuwashauri CCM hili walifanyie kazi haraka kwa maslahi ya Taifa otherwise hapa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ni kitu kisichoepukika bali ni kama timer bomb tu.

Kama wengi mlivyopata taarifa kwamba Mkuu wa Wilaya ya Serengeti amefariki mchana huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, sasa kinachonisukuma mimi kuleta thread hii hapa ni kitendo cha vijana wengi kwenye mitandao mbalimbali kuonesha kufurahiswa na kifo cha DC huyu kwa maelezo tu eti ni Gamba limepunguwa!!

Sasa basi nachukuwa fursa hii kuiomba CCM ichukuwe hatua hata za Dharura maana naona kuchukiwa huku kwa CCM ni kwa kiwango cha juu ambapo sijawahi kushuhudia watu hasa vijana kuichukia CCM kwa viwango hivi, na kama mtakumbuka Watanzania kwenye misiba huwa tunaweka itikadi kando, lakini sivyo ilivyo hivi sasa.

Huu ni mfano tu ukipita kwenye kurasa mbalimbali za kisiasa za vijana hasa huko uso kitabu, na kulwe karibu wote ni verified user.

[h=6]Gulam Mhedu
[/h] [h=6]Breaking News : Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,Kapteni Mstaafu James Yamungu amefariki dunia mchana huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Bugando Mwanza.
[/h]
y-2LR9eyI1L.gif
· · · about an hour ago via mobile

[h=6]Deogratias Masyenene
[/h][h=6]Tayari wameanza kufa mmoja mmoja...Gamba la Wilaya ya Serengeti limeaga dunia kwa presha ya UAMUZI WA MAHAKAMA TABORA!
[/h]Like · · Follow Post · 30 minutes ago
 
vita vya wenyewe kwa wenyewe vitasababishwa na nani?ni vyema kukaa pembeni na kutafakari sababu za kuchukiwa kiasi hiki.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Ni jukumu la kila mtanzania kujilinda. Msidhani watawala wetu wanafanya maamuzi to our best interests. Kiwango hiki cha hasira (chuki?) ni dalili mbaya kwa Taifa letu. Utanzania mbele kwanza.
 
Sasa basi nachukuwa fursa hii kuiomba CCM ichukuwe hatua hata za Dharura maana naona kuchukiwa huku kwa CCM ni kwa kiwango cha juu ambapo sijawahi kushuhudia watu hasa vijana kuichukia CCM kwa viwango hivi, na kama mtakumbuka Watanzania kwenye misiba huwa tunaweka itikadi kando, lakini sivyo ilivyo hivi sasa.

Hata mimi kwenye msiba huwa napatwa na huzuni sana na hasa kama aliyefariki namfahamu kama huyu mwenye hili Kaburi hapa chini

View attachment 62602

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Nawachukia CCM nadhani they are like a devil!!Potelea mbali.wapukutike tu,
 
Matola Ushauri huu unaotoa hapa ungekuwa na maana sana kama ccm na serikali yake wangekuwa sikivu. Lakini kwakuwa hawa wachuuzi wa maisha ya watanzania hawasikii wala hawaoni huu ushauri hawataufikiria zaidi ya kukuona si lolote si chochote.
Fedha wamejaza kwenye mabenki huko nchi za ng'ambo kikiwaka tu wanaruka wao na familia zao, kazi itabaki kwenu makapuku kuchinjana wakati wao wakiwashuhudia kwenye runinga na mitandao ya kijamii.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimetimiza wajibu wangu tu, kwa sababu natembelea mitandao mingi kila siku, na takwimu zisizo rasmi lakini ambazo haziwezi kutiliwa shaka na yeyote ni kwamba katika watumiaji wa Internet 10 basi 7 ni Anti CCM na wawili ndio CCM na 1 ndio anakuwa neutral hii si dalili nzuri hata chembe.

Inavyoonekana CCM inaungwa mkono na watumiaji Internet wale tu ambao wao na wazazi wao bado wananufaika na mfumo wa ufisadi au ni viwavi walioajiliwa na Nape kushinda mitandaoni kuharibu mijadala. haya maneno na ukweli huu utaendelea kusimama na mtashangaa watu wa Category ya Zomba nao kutangaza kuhama CCM baada ya maslahi yao kukoma, there will be no more System at work.
 
Mkuu pongezi.

- umetoa angalizo wapi tunakoenda na hatari iliyombele yetu.

watanzania wa aina yako ni wengi, bali kuna kundi la WAPUMBAVU wachache wanaopepelusha matumain ya kuishi pamoja kama ndugu wa taifa moja. Ni uchochezi, matusi, udin nk.

Sijui tunaelekea wapi? Mungu atulinde.
 
Back
Top Bottom