Warioba: Wanaotaka Tanganyika wasipuuzwe!

196458_1944171122871_1200297381_32399105_7054030_n.jpg
Enzi hizi zilikuwa za uzalendo wa kweli!
pencil.png
 
siitamani... tulikula yanga, tulikana wadogo zetu kwenye foleni za sukari na ilichukua miaka minne ulaya kuleta mtumba wa datsun... wa hilo siitamani

Ila nakumbuka mema na uadilifu wa Mwalimu

MIMI NAITAMANI TANZANIA IJAYO BILA CCM WALA VIONGOZI WA SASA WA CCM MADARAKANI
 
JIdu, nimependa hiyo picha! Kwa kweli Tanganyika yetu ilipendeza. Mwalimu nyerere atakumbukwa Daima kwa Upendo wake wa dhati kwa nchi pia kwa mazuri yote aliyotutendea!
 
Gagurito,

Ikiwa sasa hivi watu wanasema maisha magumu wangekuwepo wakati wa nyerere wangesema hii ni pepo.

Wakati wa nyerere tulikuwa "motoni", hata sukari unapewa kaya moja kilo moja kwa wiki au mpaka mwezi, hiyo ni mjini, vijijini walishasahau sukari ni nini?

Halafu wewe "unatamani"??!!

Tuulize tuliokuwepo, usisikie vitabu vya kumpamba. Uongo mtupu.
 
Mkubwa Maji mshindo kamwe sikubaliani na wewe, Tanganyika ya mwalimu ilipendeza, Umasikini ulikithiri kutokana na ukoloni bt wananchi hawakukata tamaa, walijituma wakijua ipo siku tumaini lao litatimia, viongozi na wananchi walíshi ktk usawa, wote wakipambana na adui wale wale, madaraja ya watu hayakuwepo kamwe, ufisadi ulikomeshwa na ilikuwa km kosa la uhaini, mashirika ya umma yalianzishwa na yalifanya kazi kwa ufanisi, mashule yalijengwa, vijana wakapata elimu iliyojaa usawa kwa wote, si kwa wakubwa wala wadogo, wahindi, waarabu na wamatumbi. Kifupi NCHI ILIPENDEZA NA WOTE WALIKUWA NA FURAHA ILIYOJAWA MATUMAINI YA MAFANIKIO.
Kwa sasa hali si shwari, NCHI IPO HOVYO, mambo hayaendi, matabaka yamezidi, na Gap kati ya aliyenacho na asienacho ni kubwa sana, imagine Mbunge apate 12,000,000/= kwa mwezi (hapo bila posho) then wajiriwa wa kima cha chini, mfano mwl. wa primary alipwe 104,000/=, VIONGOZI WAMEJAA VIBURI, WAMEKOSA USTAARABU NA NDIO WEZI WAKUBWA WA FEDHA ZA UMMA, WANAWANYONYA WANANCHI KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA WANANCHI PASIPO TIMIZA AHADI WALIZO WAAHIDI HAPO AWALI, Wananchi hawana furaha, wamekosa tumaini, gharama za maisha zimepanda, PASIPO KUWAPO DALILI ZA KUTATUA SHIDA ZAO, Serikali imelala, haina macho, mikataba mibovu isiyo na masirah kwa taifa imekithiri, nchi imegawanya ktk misingi ya ki'udini, ukabila na sasa ktk dhana ya uchochezi, Viongozi waandamizi wamekosa suluhu, wamebaki wakiishia kulalamika. Usalama wa Raia umepungua na kujawa hofu kutokana na milipuko ya hapa na pale.
Kwa haya binafsi naamini na natamani sana Tanganyika ya mwalimu nyerere, ile Tanganyika iliyotupa uhuru, ikatukusanya pamoja, tukawa na amani, tukifanya kazi kwa bidii. Mungu Ampumzishe Mwl. Nyerere, Baba wa Taifa hili, Tanzania na Watanzania TUTAKUKUMBUKA DAIMA!
 
Gagarito, hayo umeyasoma hujayaishi. Sisi tumeyaishi na washahili hunena "siri ya mtungi aijuwae kata".
 
Gagurito,

Ikiwa sasa hivi watu wanasema maisha magumu wangekuwepo wakati wa nyerere wangesema hii ni pepo.

Wakati wa nyerere tulikuwa "motoni", hata sukari unapewa kaya moja kilo moja kwa wiki au mpaka mwezi, hiyo ni mjini, vijijini walishasahau sukari ni nini?

Halafu wewe "unatamani"??!!

Tuulize tuliokuwepo, usisikie vitabu vya kumpamba. Uongo mtupu.
Hiyo ni baada ya vita ya kagera! but from independence to 1979 things were better in terms of literacy level,classless society,we were standing up for any nation that was oppressed.They needed us and we were there,they admired us a lot! not because we were rich,strong but because that was our character.

But anyways!..mi nakumbuka mkate wa siha! national milling corporation! that was the best bread ever made by humans!!!
 
tusidanganyane... kulikuwa na mazuri na mabaya pia

cha maana tutazame tanzania ijayo, kwa ajili yetu na wajukuu zetu... na iwe bora kuliko zote... hakuna mgao wa sukari, umeme wala ufisadi
 
Gagarito, hayo umeyasoma hujayaishi. Sisi tumeyaishi na washahili hunena "siri ya mtungi aijuwae kata".
MI nimeyaishi!!...
Katika soko la dunia tulikuwa tunabaniwa sana na mataifa ya kibepari compared to kenya,zaire etc. ukijumlisha na sisi kutopenda uonevu,tuliwasupport ndugu zetu sauzi,palestina,sahrawi,biafra etc.
Tulishauri umoja wa mataifa kumpa china kura ya veto kwa sababu ina population kubwa.
Kwa sasa hivi nchi kama cuba nanicaragua zinabaniwa sana access to grants,trade na projects nyinginezo za kimataifa..simply because wameamua kuishi kijamaa,kindugu!..is that a sin?....
South america ni bara lenye maliasili nyingi mno!! na wameliwa saana lakini sasa hivi wananchi wanatake over!..wamewachagua lula,chaves,morales....na wanaanza kufaidi ardhi waliyopewa na mungu pamoja,hospitali,shule,ardhi,chakula...etc
Kama hupendi hizo,basi tumekwisha...
 
Kwa upande wake, mwanasheria maarufu, Mabere Marando, akizungumza na NIPASHE baada ya kumalizika mjadala huo alipingana na mawazo ya Warioba kuhusu Serikali ya Tanganyika kwa maelezo kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndicho kinachokwamisha mpango wa kuwepo kwa serikali hiyo.

Alisema Warioba ni mwanachama wa CCM kwa kipindi kirefu lakini anashangaa kuona anatoa mawazo nje ya chama badala ya kuyatoa ndani ili yafanyiwe kazi.


Nakubaliana na wewe Marando! Warioba anzia chamani kwako kwanza ndipo uje uhubiri hayo huku nje na hapo tutakapokuona kuwa wewe ni mwenye usawa na mzalendo wa kweli............. by the way mimi ni mmoja wa wale wanaoihitaji Tanganyika kama mbingu!!!!
 
Back
Top Bottom