Warioba: Wanaotaka Tanganyika wasipuuzwe!

Mimi siitaki Tanganyika!

Mimi naitaka sana Tanganyika ndiko nilokozaliwa ndoto zangu hazijafutika hasa wimbo nilioumba

"Vijana wa Africa Kazeni mwendo wenu kuufikia ustarabu. Tazameni mbele yenu nyuma kuna giza tupu"

Kutoka 1964 tumetazamishwa nyuma yetu mbele yetu kumebaki giza tupu. Sababu tuliingizwa kwenye muungano wenye maslahi yasiyotuhusu, wala nyenzo za kuurekebisha hazipo.
 
Mimi siitaki Tanganyika!
Mkuu.
Kwa nini huitaki Tanganyika?
Tanganyika imekufanya nini? Tanganyika imekukosea nini?
Jee Tanzania itakuwepo?Itabakia kuwa Tanzania wakati wa Shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki litakapofikiwa au nayo pia utakuwa huitaki tena?
 
Amesahihisha kauli yake hapa.
28th February 2011
Warioba ashauri njia kuelekea Shirikisho Afrika Mashariki.

Jaji Joseph Warioba amesema kuwa wakati wote ameunga mkono mfumo wa serikali mbili katika muundo wa Muungano na kwamba anatambu mafaniko makubwa ayaliyofikiwa katika Muungano huo.

Jaji Warioba alitoa ufafanuzi huo juzi kwa NIPASHE kufuatia habari iliyomnukuu ikisema kuwa anataka wenye maoni ya kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika mawazo yao yaheshimiwe.

Akizungumza katika mjadala uliowashirikisha wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam waliokutaka kujifunza muundo wa Muungano wa Tanzania katika kufanikisha Shirikisho la Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki, Jaji Warioba alizitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuiga mfano wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuhakikisha Shirikisho la Afrika Masharikli linalopendekezwa kuanzishwa linafanya kazi vizuri.

Jaji Warioba alisema nchi wanachama wa EAC zinapaswa kuwa tayari kuacha mamlaka za nchi zao kama zinataka kufikia kwenye Shirikisho.

Alisema kama nchi hizo hazitakuwa tayari kufanya hivyo zitakuwa zinajigawa kisiasa badala ya kuwa na umoja na kuwaunganisha wananchi wa ukanda huo.

"Ninachokisema ni kwamba vyovyote tutakavyofanya katika nchi zetu, lazima tukumbuke mchakato wa kuelekea katika Shirikisho la Afrika Mashariki," alisema.

Warioba aliwaambia washiriki wa mjadala huo kuwa mafanikio ya Muungano wa Tanzania umekuwa imara ingawa kuna matatizo madogo madogo.

Aliongeza kuwa wananchi wa Tanzania walianza kuwa kitu kimoja tangu mwaka 1960 ingawa wakati fulani kulikuwa na pasi za kusafiria kutoka upande mmoja wa Muungano kwenda mwingine.

Hata hivyo, alisema kuna kazi kubwa ya kufanya katika kufikia haki za raia na za kisiasa, kwa mfano ili mtu aweze kupiga kura Zanzibar kumchagua Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani, anatakiwa kuwa amekaa visiwani hapo kwa muda usiopungua miaka mitatu mfululizo.

"Kwa Mtanzania bara hawezi kupiga kura visiwani kadhalika Mzanzibari ambaye ameishi bara anakosa nafasi hiyo kuwachagua viongozi wao," alisema.

Alisema kwa upande wa Tanzania Bara Watanzania wote wana haki zote za kuchagua na kuchaguliwa bila kujali wanatoka sehemu gani ya Jamhuri. Mzanzibari anaweza kupiga kura na kuomba kuchagauliwa katika Bunge ka Muungano na serikali za mitaa.

Jaji Warioba alisema maoni ya kutaka kuanzishwa kwa serikali ya Bara (Tanganyika) inaweza kuleta madhara kama yale yale ya Zanzibar ya kuvunja haki za wananchi katika kuchagua na kuchaguliwa, hali ambayo ni kurududi nyuma dhidi ya mafanikio yaliofikiwa na itadhoofisha Muungano.

Alisema kuanza kwa mfumo huo kutakuwa na Wabara ambao haki zao za kisiasa na kijamii zimezuiwa Zanzibar na kutakuwa na Wanzanzibari ambao haki hizo zikezuiwa kwa pande zote, yaani Visiwani na Bara.

Tofauti na tulivyoripoti juzi, kwamba Warioba anaunga mkono maoni ya kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika, msimamo wake ni wa kuunga mkono mfumo wa sasa wa serikali mbili ambao umeimarisha Muungano

CHANZO: NIPASHE
 
Mimi naitaka na kuitamani sana Tanganyika. Japo nime zaliwa Mtanzania mimi nimefundishwa darasani kwamba waasisi wetu wali gombea uhuru wa Tanganyika na si Tanzania. Utanzania hauja wahi kuuwa Utanganyika wetu.

Mimi binafsi naji tambulisha kama Mtanzania wala si Mtangayika. Ila tuwe wakweli wenzetu wa Zanzibar wamekunywa na kulewa Uzanzibar. Iweje upande mmoja wajione ni Watanzania na wengine wajione ni Wazanzibar? Kama tumeshindwa kuwa nchi moja basi bora tuwe nchi mbili ndani ya mwamvuli wa serikali moja.

Mkuu.
Utanzania ni sawa na uzungu au uafrika.
Haizuii mtu kuwa Mtanzania pia Mtanganyika au Mtanzania na pia Mzanzibari.


Tunaijua EU..Europeans lakini kila mzungu ana utaifa wake pia mfaransa, mjerumani, mwingereza, mgiriki, mspaniola nk.
  • Europeans plural
  • A native or inhabitant of Europe
  • A national of a state belonging to the European Union
  • Tanzanians ni watanganyika na wazanzibari.
  • Mkuu wewe unaona utata wowote hapa? Nafikiri huu ugumu tunaouweka hapa ni kwa makusudi tu.
  • Vipi Utanzania unakuondoshea utanganyika? au kivipi utanzania unamuondoshea Mzanzibari uzanzibari wake?
Vipi Tanzania au Utanzania unaua nchi z/iliyokuwepo kabla? Muungano wenyewe haukuwa wa kila jambo. Ulikuwa muungano wa mambo kumi na moja tu.

Kinachofanywa na CCM ni mazingaombwe tu, kiini macho.

Jee EAC itaziua, itazifuta nchi wanachama wake? Uafrika Mashariki utaua Utanzania, ukenya, urwanda, uburundi ,uuganda?

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...iano-ya-muungano-wa-tanzania-na-zanzibar.html
 
Ndio maana unaona wao wanajiita Wazanzibar wawapo nje ya nchi ni kwa sababu ya kuwapa huo uhuru.
The best way to do, ni kutoa kabisa huo uraisi wa huko Zanzibar ( ingawa sio rahisi) na kuweka majimbo.
Hapo kutakuwa na Utanzania wa ukweli, lasivyo ni sawa na kujilisha na upepo tu
Mkuu,
Hili kosa kubwa sana tulishafanya huko nyuma kuificha Tanganyika ndani ya Muungano. Unaikumbuka story ya East Timor na Indonesia?
Jaji Mkuu, Chande alipata mvi kwa haraka katika kushughulikia suala hilo la East timor na Indonesia.

Wala tusijaribu kufanya kosa hili tena. Mwalimu lilimshinda hilo ingawaje ukitizama mwelekeo inaonekana alikuwa na nia hiyo.

kwa kifupi, Mwalimu ndiye aliyetuachia huu mkorogo wa Muungano kutokana na ujanja wake.
 
Kwa kuwa Tunakwenda katika East-Africa Community, hii ikifanikiwa kutakuwa hatuna haja ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa sababu tutakuwa na Federation kubwa Zaidi na yenye tija, Zanzibar tunaweza kuwaacha Wakaenda kivyao, wakitaka kujiunga kwenye EAC wakaribishwe!!, kwa sababu ninajua hawawezi kukaa nje ya EAC, nchi yao ni ndogo, na itakuwa haina tija kuwa nje ya EAC,watageukana wao kwa wao muda si mrefu kwa sababu ya ubaguzi mbaya wa baadhi miongoni mwao. then wakitaka kujiunga na EAC ndo watafahamu kwa uzuri, muungano ni mbaya ukiwa ndani, ukiwa nje Muungano ni lulu, wenye akili wanajua hili ndo, maana kuna UNITED STATES OF AMERICA, EUROPIAN UNION, etc.
Mkuu.
maneno uliyayasema hapa ni mazuri kabisa lakini unapotolea mfano wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jinsi unavyoendeshwa na hii mifano ya USA na EU huoni "umetapika" baada ya kula chakula ukipendacho?

Hebu pitia tena hoja yako.

EU na Muungano wa TZ!!!????
EU imefuta nchi wanachama wake? EU imeua utaifa wa mfaransa? Mjerumani? mgiriki?

Muungano wetu ungeendeshwa kwa namna ya EU kila nchi ingependa kujiunga nasi.
Nilichowafahamu mimi wazanzibari wanataka Muungano wa haki na usawa na sio ubabe.
 
Natoa wito wa kuanzishwa /Kufufuliwa kwa Taifa Jipya la TANGANYIKA kama lifuatalo halitafanyika:-

Mahakama kuu ya Tanzania itangaze kwa umma wa Tanzania kwamba mbadiliko ya Katiba ya Zanzibar yaliounda serikali ya Umoja wa Kitaifa ni Kinyume cha Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania na yalimaanisha kuundwa kwa Taifa jipya la Zanzibar.

Naomba hili lisingoje mabadiliko ya Katiba,Mahakama ndio chombo cha kutafsiri sheria,itangaze na kubatilisha mabadiliko hayo.
 
Mahakama inaweza kutangaza tu au hadi mtu/ watu walalamike na kufungua kesi isikilizwe na then hukumu inatolewa? Mie niko tayari kujiunga na watu watakaodai Tanganyika yetu
 
Nyerere (far left) with some leaders of the frontline states
President Samora Machel of Mozambique (left), Nyerere and President Kenneth Kaunda of Zambia (right)
Celebrating Independence Day in 1961
1962, Nyerere receiving his honorary second degree from the University of Edinburgh
Tanzania's first President Julius Nyerere with Bernhard Grzimek
Mwalimu Julius K.Nyerere, President of Tanzania, at Taj Mahal, Agra 1971
Nyerere addressing on the opening of Mlimani Campus at the University Collage of Dar-es-Salaam
Nyerere congrats after Kagera war victory 1979
Nyerere congrats in Iringa, after Kagera war victory 1979
Nyerere congrats after Kagera war victory 1979
Nyerere with his generals on Amini of Uganda invasion to Tanzania, November 1978
1978 Nyerere and Samora in Dar-es-Salaam Airport
Nyerere with Samora with both their wives in Dar-es-Salaam airport
Mwalimu with Southern Africa liberation leadera 1975
Mwalimu Nyerere, Dr. Kaunda, Dr. Obote and Kawawa in State House in Dar-es-Salaam
Page 5 of 8 pages « First < 3 4 5 6 7 > Last »

Random Images Nyerere with elders on independence ceremonies 1961
Ismaili Leaders Of Arusha With Former President Julius Nyerere
J.K.Nyerere with President Charles de Gaulle on his right in Paris 1965
Julius K. Nyerere with Pope John Paul II in Dar-es-Salaam
The Rallies along the street of Dar-es-Salaam lead by president against the revolt made in 1964
 
kwa mambo yaendavyo, sina shaka vizazi vijavyo vitadai tanganyika yao! Mwl. Nyerere tutamkumbuka daima!
 
umetukumbusha mbali.Tanganyika hapo kwa sasa.kama muungano wavunjika ni TANZANIA itabaki ZANZBAR kivyaoo
 
Mzeemwanakijiji wewe endelea kula kuku wako kwa mrija ,wenye kuishi hapa Tanganyika ndio wenywe uchungu wa Tanganyika yao ,sipingi kutoipenda kwako Tanganyika na heshimu sana na kwa maana hiyo ndio umeikimbia Tanganyika kwakuwa huipendi na huitaki kuwepo kwake sasa waache wenye kuitaka waipiganie irudishe hadhi yake

Kwani kuwa Marekani kuna maana ya moja kwa moja kuwa kuna raha!!! Una maanisha nini "kuku kwa mrija mkuu?"
Tukubaliane kila mtu ana choice ya kuishi kokote katika dunua hii, ari-muradi utimize masharti ya nchi husika...

Tuongee hoja....
Mimi naona kudai Tanganyika kumekwisha pitwa na wakati, maana tumekwisha ingiliana sana kiasi cha kuwa wamoja!! Let us re-define huu muungano kwenye katiba mpya kwa uwazi, ushikishwaji na umoja!
 
Tukishindwa kuboresha Muungano na kujenga Tanzania Imara, tukafikia ama kuuvunja Muungano au kuiacha Zanzibar kuwa nchni ndani ya Tanzania badala ya Kata au wilaya; hamna haja ya kwenda EAC maana hatutakuweza tutashindwa tu! tutakuwa ndani ya EAC na ubinafsi na Ubaguzi kama unaofanywa na Wazibari sasa, Members wengine wa EAC hawatatuelewa na tutakuwa na EAC yenye vurugu na malalamishi ya kila siku kitu kitakacho perekea kuvunjika kwa hiyo EAC nashauri kabla ya kwenda EAC tumalize na kuweka sawa swala la Tanzania.

Siupendi ubaguzi siku zote lakini Wazanzibari wamejibagua sana na kuinyonya sana Bara
 
Tukishindwa kuboresha Muungano na kujenga Tanzania Imara, tukafikia ama kuuvunja Muungano au kuiacha Zanzibar kuwa nchni ndani ya Tanzania badala ya Kata au wilaya; hamna haja ya kwenda EAC maana hatutakuweza tutashindwa tu! tutakuwa ndani ya EAC na ubinafsi na Ubaguzi kama unaofanywa na Wazibari sasa, Members wengine wa EAC hawatatuelewa na tutakuwa na EAC yenye vurugu na malalamishi ya kila siku kitu kitakacho perekea kuvunjika kwa hiyo EAC nashauri kabla ya kwenda EAC tumalize na kuweka sawa swala la Tanzania.

Siupendi ubaguzi siku zote lakini Wazanzibari wamejibagua sana na kuinyonya sana Bara
Mkuu hayo maandishi mekundu unamaanisha nini?
Kuboresha muungano ni kitu gani?
Tanzania imara ikoje? Hebu ifafanue unakusudia nini?

Sasa hivi Tanzania imo EAC na mambo mengi ya EAC si katika mambo ya Muungano hapo unawaelezaje wale members wengine wa EAC wanapohoji serikali ya Muungano wa Tanzania imepata wapi mamlaka ya kuiwakilisha Zanzibar katika mambo ambayo si ya Muungano.

Haya ya ubaguzi nafikiri ni makelele zaidi. Sisi pia tunapiga kelele hizi kuwa wakenya wako hivi, wako vile au ubaguzi maana yake nini?

Kama Muungano utasimamiwa na kuendeshwa kwa haki na usawa kelele za ubaguzi zitapotea zenyewe.

Natumai umeshakisoma kijarida "Shirikisho ndani ya shirikisho."
 
Ndugu wanaJf najua kunabaadhi naweza washangaza kwa kuzungumzia Tanganyika wakati kuna Tanzania ijulikanao kimataifa, lakini naomba muwe makini ktk kulielewa hili licha yakuwa ni mawazo binafsi bt naamin yana maana!
Ndugu wanaJF nadhan kwa wale wenye umri km wangu, ambao hatuku bahatika ishi ktk uongoz wa Mwl. Nyerere tukiwa na akili zetu timamu na uelewa km huu tulionao bt tumepata kusikia maisha waliyoishi watanganyika wenzetu ktk awamu ya kwanza either kwa kusoma vitabu au kwa kusimuliwa, kifupi maisha yalikuwa mazuri, matamu na yenye kutia tumaini, wananchi walijawa na moyo wa uzalendo, walijituma nakujitolea kwa moyo mmoja kwa maendeleo ya taifa, watu wote walikuwa sawa, heshima ilitawala,rushwa na uhujumu uchumi vilikomeshwa, madaraja ktk jamii yalikomeshwa, maadui wa taifa (ujinga, maradhi na umasikini) yalitanabaishwa na serikali ikaweka malengo juu ya kutatua matatizo hayo, kifupi nchi ilikwenda, tanganyika ikafahamika kimataifa, ikajenga marafiki ktk sehemu kubwa duniani. Kwa mambo aliyoifanyia Tanzania Mwl. Nyerere kamwe atakumbukwa na vizazi vyote vya watanzania kwa maisha yote.
Ndugu wanaJF mambo kwa sasa yapo tofauti sana, ufisadi umekithiri, uzalendo umepungua, uwajibikaji wa viongoz umekua mdogo, maendeleo yamezorota, matabaka kati ya mwenye kipato na wasionacho Limekua kubwa, huduma kwa wananchi zimedhohofu, hali ya maisha ni tata kias mipango haikawi sawa!
Ktk hali ndugu wanajf nadhan nina kila sababu ya kuitaman tanga!
 
Back
Top Bottom