Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Na B. OLE,
Baada ya kufuatilia kwa makini maoni na ya tume ya katiba inayoongozwa na Jaji Warioba kuhusu mchakato wa katiba mpya inayotegemewa ifikapo hapo mwaka 2014 ,nimepatwa na wasi wasi juu ya ukweli na lengo la wenzetu kuhusu lengo na hatma ya mchakato huu.
Inaonekana kwamba haya maoni yanayotolewa hasa kwa upande wa Zanzibar na kupitia na vianzio mbali mbali ni geresha tu ya kuudanganya ulimwengu kwamba Tanzania ni Nchi ya demokrasia jambo ambalo sio kweli.
Tanganyika haiko tayari kufuata matakwa ya Wazanzibar kwa kile wanacholilia cha kuwa na Zanzibar huru yenye Dola kamili. Hii imedhihirisha pale Warioba na timu yake walipotembelea na kutaka kupata maoni ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Wajumbe takribani wote ukiwacha wale akina minal-dhalimina walitaka kuona kwamba Zanzibar inajitegemea wenyewe kama dola huru lenye mamlaka kamili ndani na nje ya Nchi hoja ambayo Warioba na timu yake walikuwa wanaipinga wazi wazi ndani ya Baraza la Wawakilishi.
Jaji Warioba yeye na Tume yake ilitumia sana muda kuwakatisha Wajumbe hasa pale waliupokuwa wakilizungumzia suala la kuwa na Mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar na zaidi walipokuwa wakidai Utaifa wa Mzanzibar,na kusema apewe maelezo kuhusu wale wajumbe wanaodai Muungano wa mkataba maana yake nini?
Inashangaza kuona kwamba mtu kama Jaji Warioba kuwa haelewi kuhusu Muungano wa mkataba kama ule wa EU na mengine sio kweli,suala hapa ni kwamba Tanganyika wana ajenda yao kuhusu Zanzibar. Hawako tayari kuona Zanzibar inajikomboa kisiasa wa kiuchumi.
Ilikuwa inaonekana wazi wazi kwamba kauli ya Muungano wa mkataba inawakera akina Warioba na tume yake huku akitishia kuvunjika kwa Muungano,kutokana na madai yanayotolewa na Wajumbe hao.
Mimi nimuulize Jaji warioba kwa heshima na taadhima hivi Muungano ni Msaafu kwamba ukiupinga utakuwa huna salama kwa Mola wetu? Hakuna haja ya kuwatisha Wazanzibar kwa hilo. Zanzibar ilikuwepo tokea enzi na enzi na wala ilikuwa haitegemei Muungano.
Lazima nyinyi kama tume mueleze kile ambacho Wazanzibar wanataka kwani hapa kila mtu anaangalia maslahi yake kama Taifa, ikiwa munahisi kwamba Wazanzibar wanachodai ni kero kwenu, kwa nini tusivunje huu Muungano kwa faida za pande zote mbili?
Nahisi Jaji Warioba ni vyema kuziba ukuta kuliko kujenga ukuta, huko munakotaka kutupeleka sisi kama Wazanzibar tunasema kwa kinywa kipana kwamba hilo haliwezekani,Jamhuri ya watu Wazanzibar kwanza.