Warioba, Salim, Zitto na Slaa washirikiana kufanikisha mazungumzo ya Ikulu

Hivi kuna kuna watu wanampenda mnafiki zitto kabwe makubwa(watakuwa ni ccm na cuf hawa ili chama kife).muwekeni basi agombee urais muone kama hatapata kura hata laki tano.na mmlinganishe na slaa.watu tunajua kutofautisha kati ya kondoo na mbuzi.

zitto kasaliti nini?au ww unaleta ushabik tu,ebu tupe evidenc za usaliti wa zitto na wala usituletee habari za gazeti la udaku la Mwanahalisi.Bravo zitto kwa kas yako.
 
Wana JF,
Ukifuatilia mtiririko wa hii mada na uchangiaji wake utagundua kuna watu tayari wako kazini kuivuruga Chadema.
Tunajiuliza kama kulikuwa na vikao vya chini chini vya mazungumzo kati ya Chadema na Ikulu kulikuwa na haja gani ya kuandikwa na gazeti kwa mfumo huo? Tena kwa malengo ya kuonyesha mwenyekiti Freeman Mbowe si lolote si chochote kwenye haya mazungumzo? Kweli inaingia akilini mazungumzo makubwa kama haya yangefanywa bila hata Katibu Mkuu Dr Wilbrod Slaa kumjulisha mwenyekiti wake hata kwa simu? Is it possible? Dr Slaa uko huku jamvini tafadhali sana jitokeze uweke wazi kila kitu ili ijulikane kama kuna wanaostahili kupata credit na kuna wasiostahili.

Nilichogundua katika ufuatiliaji wangu ni kwamba kuna watu wanataka kutumia kila hila ili Freeman Mbowe asiwe tena kiongozi wa Chadema.Fine.Lakini tumieni njia za kistaarabu.Ni nani leo hii atakataa maendeleo ya Chama cha CDM ni kutokana na uongozi uliotukuka wa Freeman Mbowe na Wilbrod Slaa? Ni nani atathubutu kusimama kidete na kusema Freeman Mbowe hastahili sifa yoyote kwa haya yanayoendelea? Ninajua fika kwamba lengo kuu la Magamba ni kumuondoa Freeman kwenye uenyekiti na kumpa mtu ambaye itakuwa ni rahisi kum-drive wanavyotaka.Lakini niseme wajumbe wa Chadema wanaofanya uchaguzi wako makini sana na kamwe hawatakubali kupeleka chama kwa mfuasi yeyote wa magamba.

Mleta mada amesahau kwamba ni wiki iliyopita tu alileta mada hapa jamvini ya kumshauri Dr Wilbrod Slaa agombee ubunge wa Arumeru Mashariki ili akachukue nafasi ya uongozi wa upinzani bungeni eti kwa madai kwamba Freeman Mbowe hawezi na imemshinda.Kwa hiyo haya yote tunayojadili hapa ni mwendelezo maalum uliopangwa wa chuki zilezile dhidi ya Freeman Mbowe na Chadema.Ninachoweza kumhakikishia mleta mada kwamba uongozi chini ya Katibu Mkuu Dr Slaa uko makini na utachuja na kutoa ushauri muafaka pale uchaguzi mkuu utakapokaribia.Tukumbuke maneno ya Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye aliposema ‘’ Wanaotumia kalamu kuchafua wengine kwa malengo ya kupata uongozi wakiingia madarakani watatumia bunduki’’.Chadema kuweni macho!!

broo kwan Zitto sio kiongoz wa chama mbona haujamtaja hapo kwenye list ya watu waliokifikisha chama hapa?au ww nawe ni mbaguz na Pro-Mbowe?lakin kwa nini hii mada inaonekana tatizo au kwa vile tu katajwa zitto.,nyie ndio munaotaka kumgombanisha mwenyekit mbowe na zitto acheni hizo.
 
ni gazeti la mwanahalisi...siyo mtoa maada

unachosema kina mantiki, hakuna haja ya habari hizi kuwekwa gazetini, cha ajabu mwanahalisi lina bifu na zito, mwanahalisi ni hao wa koo za akina mbowe!

Mkuu wangu sio gazeti la mwanahalisi.Lililoandika ni Raia mwema na imeandikwa na yule mwandishi Dilunga ambaye siku zote anatoa makala za kuichafua Chadema.
 
broo kwan Zitto sio kiongoz wa chama mbona haujamtaja hapo kwenye list ya watu waliokifikisha chama hapa?au ww nawe ni mbaguz na Pro-Mbowe?lakin kwa nini hii mada inaonekana tatizo au kwa vile tu katajwa zitto.,nyie ndio munaotaka kumgombanisha mwenyekit mbowe na zitto acheni hizo.

Mkuu unazidi kujivua nguo na kuonyesha malengo yenu halisi ya hii makala.Mimi nimewataja Freeman Mbowe na Dr Wilbrod Slaa kwani ndio vinara wakuu wa chama na ndio wako front line kuongoza mapambano.Siwezi kumtaja kila kiongozi hapa kwani hata ukurasa hautatosha kuwataja viongozi wote wa chadema na mchango wao katika chama.Ninapowataja vinara hawa wawili ndio utambulisho wa wasaidizi wao wote.Pole sana lakini naamini ujumbe umekufikia.
 
Kim there is a old English adage that sounds "one swallow does not make summer". Hivi just that wazo la kukutana na jk lilianzia kwake that only becomes a greenlight kuwa agombee urais. This leaves much to be desired on your level of thinking and your compatriots. Na kwa nini asiwe aishie kugombea.Nilifikiri kuwa unataka kusema anafaa kuwa rais. Lakini kwa kitu kimoja mtu anaonekana anafaa kushika wadhifa wa ofisi kubwa ya kiutawala nchini basi tutabaki nyuma mithiri ya koti. Tunatakiwa kuainisha sifa wa kiongozi na hasa kiongozi mkuu kama rais. Rai ya Generali Ulimwengu ya jana imesema mengi kuyarudia mimi ni exaggeration. Sisemi Zitto hafai lakini issue moja kuhararisha ndio naquery
 
Jamani nyie wakereketwa wa viongozi wa chama;kina white elephant na wenzake mnatia aibu kiasi cha watanzania kuanza kuhoji uwezo wenu wa kufikiri na elimu zenu juu ya upembuzi wa mambo katika medani za siasa za nchi hii. Yaani kiukweli mnaropoka mambo ambayo hata Zitto mwenyewe anawashangaa! Nahisi nyie ni mapandikizi mnaolenga kuchochea migogoro katika vyama ili watu wafarakane upinzani usambaratike kama ilivyo sasa kwa CUF na NCCR lakini Chadema mtachemsha maana ndiye baba la upinzani Dunia yote inajua hivyo! Mh. Mbowe ni mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mwenyekiti wa vikao vyote vya chama cha chadema, je wataka kutueleza kwamba Zitto alitoroka Dodoma bila boss wake Mbowe kujua alikotokomea wakati issue hiyo ilikuwa ya kiofisi? au je, hukuwahi kusikia kuwa Mh. Mbowe ameshindwa kuhudhuria kesi inayomwandama kule Arusha sababu ya shuguli za kamati ya bunge kutokana na nafasi yake? Au umesahau kuwa Zitto katika chadema ni naibu au msaidizi wa katibu mkuu (Dr. W. Slaa) ambaye ki protokali anatakiwa kuripoti kwake? Kwa ufupi, itifaki ya chadema haiko wazi kama unavyofikiria, ina password yake ndiyomaana kila mamruki anayeiongelea chadema anasema hisia zake tu. Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake brother. Chadema ni chama makini chenye viongozi makini na kinachoendesha shughuli zake kwa makini chini ya Kichwa, Dr Wilbroad Slaa. Hivyo usipende sana kukuza vitu vidogo ambavyo haviisaidii nchi wala hujui chanzo chake. Yaani zito kukutana na Jaji Warioba tayari umeweka katika maajabu nane ya dunia, sasa ukiambiwa kule ulaya mbwa anatumwa sokoni na kurudi akiwa na alichotumwa hiyo si utaitisha kikao na waandishi wa habari?! Mh. Zitto alishawambia hatagombea urais msimu ujao akiwa Hospitalini India wakati akijibu tuhuma dhidi yake juu ya mgogoro wa Mh. D. Kafulila na James Mbatia wa Nccr, na sababu alizitoa za kikatiba (ya Chadema) na kisheria. Anawaheshimu na kuwatii viongozi wenzake ndani ya chama, wa juu na chini yake. sasa ya nini kumchonganisha na wakubwa zake wa kazi. Maana hata ukilazimisha Zitto avae kiatu cha Dr Slaa bado kitakuwa oversize! Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Nakushauri fuatilia mambo yanayoelimisha watu kama vile katiba ya nchi, utasaidia wengi nawe mwenyewe*
 
Igekuwa wengi wanamkubali si tungemuona Ikulu saa hizi? yeye tunapigana vikumbo hapahapa JF. mitaani huko hapawezi.
Ikulu kaja mwizi wa kura amebakia kuvuta uso tuu simanzi imemshika hawezi hata kusimama akitoa hotuba shurti aninamie meza dhuluma itamtafuna sana anakimbia kimvuli chake
 
broo kwan Zitto sio kiongoz wa chama mbona haujamtaja hapo kwenye list ya watu waliokifikisha chama hapa?au ww nawe ni mbaguz na Pro-Mbowe?lakin kwa nini hii mada inaonekana tatizo au kwa vile tu katajwa zitto.,nyie ndio munaotaka kumgombanisha mwenyekit mbowe na zitto acheni hizo.

Sikuzote kiongozi anayefaa ni yule anayesema tume, tuta,tuli, lakini yule anyesema nime,nina,nita,huyu hafai niwakutupwa katikati ya bahari
 
Najua wapo watu hii hawatapenda kuisikia zitto alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili....lakini ndio hali halisi,lazima tuiseme .

Wadau mi nadhani baadhi yetu wakati umefika sasa tubadili mitazamo yetu kuhusu ZITTO KABWE;kiukweli kijana anaonyesha ukomavu wa kisiasa kila kukicha tofauti na vijana wengi ambao wanakimbilia posho tu; Zitto kumbe anafanya mambo mengi bila kupiga mayowe wala kuita wapiga picha...hili nalisema kufuatia kugundua kuwa Mh. zitto kabwe kuwa chanzo cha mazungumzo maarufu yanayoendelea ikulu kati ya chadema na Rais kikwete,mambo yako hivi.....

Safari ilianza hivi; baada ya kuona mwenendo wa mijadala na mwelekeo wa baadhi ya viongozi wenzake, hasa katika siku ambazo CHADEMA kilikuwa kinatangaza kwamba kingeitisha maandamano nchi nzima kupinga mchakato wa katiba mpya uliokuwa umewasilishwa na Serikali bungeni, baadhi ya wanaCHADEMA na wengine miongoni mwa umma, walihisi kuwako kwa hatari ya kweli ya vurugu kuibuka nchini, ambayo isingekisaidia chama hicho au kundi jingine lolote, hivyo Zitto alifunga safari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ili kuteta na Dk. Slaa.


Katika mazungumzo yao, vyanzo kadhaa vya habari vimesema, hoja ilikuwa ni umuhimu wa kuchukua njia ya mazungumzo katika suala la mchakato wa katiba mpya, kuliko njia ya maandamano. Lakini Dk. Slaa amekaririwa akiashiria kwamba ilikuwa vigumu zaidi kuanzisha njia ya mazungumzo kwake kuliko njia ya shinikizo kupitia maandamano.

Raia Mwema limeambiwa kwamba kutokana na ugumu huo, Dk. Slaa amekaririwa kumueleza Zitto kuwa wanaweza, katika kufikia kupata muda wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete, kuwatumia wazee wenye utulivu na busara, wasio na misimamo mikali ya kisiasa, wenye kutanguliza mbele maslahi ya nchi na wanaosimamia zaidi nguvu ya hoja, ambao miongoni mwao ni Dk. Salim na Jaji Warioba.

Habari zinasema, tatizo kubwa alilokuwanalo Dk. Slaa katika kuwafikia wazee hao ni kwamba hakuwa na ukaribu wa kiasi hicho nao na Raia Mwema limeelezwa kwamba katika mazingira hayo ndipo Zitto alipoahidi kuwatafuta wahusika na kuwaeleza mtazamo huo na kisha kusikiliza mawazo yao.

“Zitto alikwenda kuwaona Jaji Warioba na Dk. Salim na wakati huo, vikao vya Bunge vilikuwa vikiendelea Dodoma. Kule wale wazee walimsikiliza Zitto na kuona mapendekezo yao yana mantiki na kwa hiyo, Zitto akarudi kumweleza Dk. Slaa na baadaye wakapanga kukutana na Warioba na Salim.
“Walizungumza sana, wakafanya uchambuzi wa kina na njia bora zaidi ya kuweza kufikisha suala hilo kwa Rais Kikwete. Jaji Warioba aliombwa afanye kazi hiyo kuwa kiunganishi na taarifa zinasema baada ya kujiridhisha na hali ya mambo naye aliwasiliana na Ikulu na mchakato ukaanza.

Ndani ya Kamati Kuu CHADEMA

Habari za uhakika zinasema baada ya Dk. Slaa na Zitto kukubaliana na akina Warioba, kibarua kigumu kwao kilikuwa kuwasilisha mawazo yao mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA.
Taarifa hizo zinaelezwa kuwa Zitto hakuwa amehudhuria kikao hicho cha Kamati Kuu na hivyo, mzigo ulibaki kwa Dk. Slaa. Wakati huo, Zitto alikuwa amerejea kutoka India alikokuwa akitibiwa na hivyo hakuweza kushiriki kikao cha Kamati Kuu kwa sababu ya hali yake kiafya kutoimarika.

“Zitto aliitwa na Dk. Slaa kwenye Kamati Kuu amsaidie kueleza suala hilo, tulimwona alikuwa ametoka kuumwa alijitahidi sana kujieleza. Lakini kabla ya hapo, uchokozi wa wazo hilo uliibuliwa na Regia Mtema, ambaye alisema tukamwone Rais Kikwete ili tuzungumze naye....wajumbe karibu wote wakaguna wakimpinga na kumwona msaliti, wengine wakisema eti katumwa.

“Baada ya Zitto kuitwa na Dk. Slaa, ndipo alianza kutoa maelezo na hatimaye wajumbe wakaridhia. Na baadaye Mbowe akaandika barua kwenda kwa Rais kuomba kukutana naye ili kuwasilisha mapendekezo ya chama,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Warioba ‘messanger’ mtiifu

Habari zinasema baada ya Mbowe kuandika barua ya kuomba kukutana na Rais Kikwete, Jaji Warioba ndiye aliyekuwa ‘wakala’ wa mawasiliano kati ya pande hizo mbili, yaani CHADEMA na Rais Kikwete.
“Barua ile alipewa Jaji Warioba naye binafsi kwa mkono wake aliifikisha Ikulu moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye baadaye alifanya mazungumzo na Kikwete pamoja na Dk. Salim na kisha kukubali ombi hilo la CHADEMA.
“Warioba akarejea tena kwa viongozi wa CHADEMA kwa ajili ya kutoa majibu kama ‘mjumbe’ na akaeleza kuwa Rais hana tatizo kukutana na ujumbe wa CHADEMA kwa sababu hili ni suala la kitaifa, si la kwake pekee,” anaeleza mtoa taarifa huyo.

Waziri Mkuu Pinda arudi Dar

Kutokana na kuanza kwa mchakato huo wa ‘kimya kimya’ vyanzo vyetu vya habari kutoka bungeni vinaeleza kuwa mjadala wa sheria hiyo ulikuwa ukisogezwa mbele kwa maelezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kutoa nafasi kwa mchakato huo wa CHADEMA, Dk. Salim, Jaji Warioba na Rais Kikwete, ambao mpaka wakati huo haukuwa rasmi, ushike kasi.
Vyanzo vingine vya habari vimesema kuna wakati Waziri Mkuu Pinda alikwenda Dar es Salaam kutoka Dodoma kwa ajili ya mazungumzo kuhusu suala hilo na baada ya mjadala wa sheria hiyo kusogezwa mbele kujadiliwa bungeni kwa mara kadhaa, ilibidi mjadala uruhusiwe.

Milango ya Ikulu yafunguliwa

Baada ya kazi hiyo ya ‘kimya kimya’ na baada ya Bunge kujadili, kurekebisha na hatimaye kupitisha muswada huo, ujumbe wa CHADEMA ulikaribishwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo.
Makaribisho hayo yaliwekwa bayana na Ikulu kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano na kuanza rasmi Novemba 27, mwaka jana, na kurejewa tena siku iliyofuata, Novemba 28, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo ya CHADEMA kuhusu sheria hiyo.
“Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa,” inaeleza taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa baada ya duru la kwanza la mazungumzo hayo.

Kamati Kuu CCM yatia neno

Hata hivyo, wakati CHADEMA wakiwa wameomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa inaendelea na kikao chake mjini Dodoma, ambako ilimshauri Rais Kikwete kutanua wigo kwa kukutana na wadau wengine, ambao ni pamoja na vyama vingine vya siasa, ambavyo hata hivyo, tayari vimeonana na kuzungumza na Kikwete. Vyama hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.
Kwa upande mwingine, ushauri huo wa Kamati Kuu ya CCM ulizua mjadala mpya katika jamii, wengine wakiupinga na kuukosoa, wengine wakiuunga mkono lakini mwishowe, Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini, aliuzingatia.

Viongozi wanne waibuka vinara

Kama suala hili litafikia hatua nyingine katika hali isiyokuwa na malumbano tofauti na dalili za awali zilivyokuwa zikiashiria, basi, vinara wa kutuliza hali hiyo ni pamoja na Rais Kikwete binafsi ambaye aliridhia kukutana na wawakilishi wa makundi tofauti licha ya muswada kupitishwa na Bunge naye mwenyewe kuutia saini kuwa sheria.
“Angeweza kugoma na kutumia ubabe wa dola kulazimisha mambo, lakini hakufanya hivyo,” kinaeleza chanzo chetu cha habari na kuongeza kuwa; “Shukurani za kipekee ziwaendee Dk. Slaa, Zitto, Dk. Salim na Jaji Warioba, wameonyesha upeo mkubwa wa kiuongozi.”

Muswada kufanyiwa marekebisho

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa mazungumzo hayo pamoja na ya vyama vingine yamezingatiwa na Rais Jakaya Kikwete na kwa hiyo, katika mkutano ujao wa Bunge unaonza wiki ijayo mjini Dodoma, sheria hiyo ya mchakato wa Katiba mpya nchini itafanyiwa marekebisho.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kurejesha uwezekano wa viongozi wanasiasa, wakiwamo wabunge kuweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Katiba ambao watateuliwa na Rais, kinyume cha ilivyokuwa awali, wanasiasa wakizuiwa kuteuliwa wajumbe.

Marekebisho hayo yatawasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kabla ya mkutano huo kwisha na zipo taarifa nyingine kuwa huenda Rais Jakaya Kikwete akakutana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi au kile alichopaswa kuzungumza nao kikafikishwa kwao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Inatarajiwa kuwa wabunge hao wataelezwa hatua kwa hatua kuhusu kilichojiri kati ya mkutano wa Rais Kikwete na vyama vya upinzani kuhusu muswada walioupitisha ambao hatimaye naye aliutia saini kuwa sheria.

DUH! MDAU UME COPY RAIA MWEMA LOTE?!!! hata hivyo habari uliyoleta ni kweli
 
Sungura alipokosa zabibu alisema...
mwizi ni Mwizi,Magogoni kajaa mwizi wa kura aibu shupa hawezi kitu tena,maisha kwa kila mtu yamenda komba bado anawaza ajitoe vipi na aibu ,serikali kaifirisi amebaki anarubaruba
 
Mimi sio magwanda lakini mkubali msikubali hakuna aliyeipandisha chati magwanda kama Zitto, kabla ya Zitto ilikuwa si lolote si chochote, na akiondoka mmekwisha!

Hapo Faiza umedanganya ni kweli kuwa Zitto ni kijana mchapa kazi na mbunifu lakini si kweli kwamba akiondoka itakwisha hata kidogo!!! Wapo wengi sana tu wenye nguvu kuliko yeye Mathalani DR Slaa!
 
Ikulu kaja mwizi wa kura amebakia kuvuta uso tuu simanzi imemshika hawezi hata kusimama akitoa hotuba shurti aninamie meza dhuluma itamtafuna sana anakimbia kimvuli chake
@Froida: Magamba yanampango ya kumwekea TISS wa kumshikilia wakati akihutubia aache kuanguka anguka ovyo majukwaani kwa kuona soo!!
 
mwizi ni Mwizi,Magogoni kajaa mwizi wa kura aibu shupa hawezi kitu tena,maisha kwa kila mtu yamenda komba bado anawaza ajitoe vipi na aibu ,serikali kaifirisi amebaki anarubaruba
Kweli mwana kaishiwa sera!! ana kazi ya kutetea majambazi menzie yasimuumbue ameachana na"maisha bora kwa kila mtz" labda hongo ya wanyama kule Doha watampa ulinzi tutakapochoka naye!!
 
@Froida: Magamba yanampango ya kumwekea TISS wa kumshikilia wakati akihutubia aache kuanguka anguka ovyo majukwaani kwa kuona soo!!

Si ndiyo hapo mtu nafsi inamsuta anasukumwa na upepo halafu mtu anataka kutugeuza sisi madondocha kusifu wezi , anatuleteea za kuleta wakati watu tumeshaanza kula majongoo na pumba kama mlo wa siku kwa ajili ya ukata
 
CCM inaogopa Zitto akipata uongozi, Slaa na Mbowe, hawana kitu, washafikia kikomo chao cha kufikiri na ndio maana wamebaki na siasa maji taka. Zitto ana kichwa lakini akichukuwa uongozi wa chadema, itabidi isambaratike kwani Wachagga hawatomkubali kabisa tena. Na hapo ndio tutaona CCK ikitutumka.

na unategemea watu wenye akili wasome haya uliyoyaandika, halafu wakuheshimu au hata kuheshimu chochote unachoandika?

Mnahangaika bure na cheap talk....Zitto alisema mwenyewe kwamba, marehemu Regia ndio aliyeleta wazo la mazungumzo na kikwete, sasa hapa mnaongea nini.

Too Cheap.
 
najua wapo watu hii hawatapenda kuisikia zitto alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili....lakini ndio hali halisi,lazima tuiseme .

Wadau mi nadhani baadhi yetu wakati umefika sasa tubadili mitazamo yetu kuhusu zitto kabwe;kiukweli kijana anaonyesha ukomavu wa kisiasa kila kukicha tofauti na vijana wengi ambao wanakimbilia posho tu; zitto kumbe anafanya mambo mengi bila kupiga mayowe wala kuita wapiga picha...hili nalisema kufuatia kugundua kuwa mh. Zitto kabwe kuwa chanzo cha mazungumzo maarufu yanayoendelea ikulu kati ya chadema na rais kikwete,mambo yako hivi.....

Safari ilianza hivi; baada ya kuona mwenendo wa mijadala na mwelekeo wa baadhi ya viongozi wenzake, hasa katika siku ambazo chadema kilikuwa kinatangaza kwamba kingeitisha maandamano nchi nzima kupinga mchakato wa katiba mpya uliokuwa umewasilishwa na serikali bungeni, baadhi ya wanachadema na wengine miongoni mwa umma, walihisi kuwako kwa hatari ya kweli ya vurugu kuibuka nchini, ambayo isingekisaidia chama hicho au kundi jingine lolote, hivyo zitto alifunga safari kutoka dodoma kwenda dar es salaam ili kuteta na dk. Slaa.


Katika mazungumzo yao, vyanzo kadhaa vya habari vimesema, hoja ilikuwa ni umuhimu wa kuchukua njia ya mazungumzo katika suala la mchakato wa katiba mpya, kuliko njia ya maandamano. Lakini dk. Slaa amekaririwa akiashiria kwamba ilikuwa vigumu zaidi kuanzisha njia ya mazungumzo kwake kuliko njia ya shinikizo kupitia maandamano.

Raia mwema limeambiwa kwamba kutokana na ugumu huo, dk. Slaa amekaririwa kumueleza zitto kuwa wanaweza, katika kufikia kupata muda wa kukutana na rais jakaya kikwete, kuwatumia wazee wenye utulivu na busara, wasio na misimamo mikali ya kisiasa, wenye kutanguliza mbele maslahi ya nchi na wanaosimamia zaidi nguvu ya hoja, ambao miongoni mwao ni dk. Salim na jaji warioba.

Habari zinasema, tatizo kubwa alilokuwanalo dk. Slaa katika kuwafikia wazee hao ni kwamba hakuwa na ukaribu wa kiasi hicho nao na raia mwema limeelezwa kwamba katika mazingira hayo ndipo zitto alipoahidi kuwatafuta wahusika na kuwaeleza mtazamo huo na kisha kusikiliza mawazo yao.

“zitto alikwenda kuwaona jaji warioba na dk. Salim na wakati huo, vikao vya bunge vilikuwa vikiendelea dodoma. Kule wale wazee walimsikiliza zitto na kuona mapendekezo yao yana mantiki na kwa hiyo, zitto akarudi kumweleza dk. Slaa na baadaye wakapanga kukutana na warioba na salim.
“walizungumza sana, wakafanya uchambuzi wa kina na njia bora zaidi ya kuweza kufikisha suala hilo kwa rais kikwete. Jaji warioba aliombwa afanye kazi hiyo kuwa kiunganishi na taarifa zinasema baada ya kujiridhisha na hali ya mambo naye aliwasiliana na ikulu na mchakato ukaanza.

ndani ya kamati kuu chadema

habari za uhakika zinasema baada ya dk. Slaa na zitto kukubaliana na akina warioba, kibarua kigumu kwao kilikuwa kuwasilisha mawazo yao mbele ya kamati kuu ya chadema.
Taarifa hizo zinaelezwa kuwa zitto hakuwa amehudhuria kikao hicho cha kamati kuu na hivyo, mzigo ulibaki kwa dk. Slaa. Wakati huo, zitto alikuwa amerejea kutoka india alikokuwa akitibiwa na hivyo hakuweza kushiriki kikao cha kamati kuu kwa sababu ya hali yake kiafya kutoimarika.

“zitto aliitwa na dk. Slaa kwenye kamati kuu amsaidie kueleza suala hilo, tulimwona alikuwa ametoka kuumwa alijitahidi sana kujieleza. Lakini kabla ya hapo, uchokozi wa wazo hilo uliibuliwa na regia mtema, ambaye alisema tukamwone rais kikwete ili tuzungumze naye....wajumbe karibu wote wakaguna wakimpinga na kumwona msaliti, wengine wakisema eti katumwa.

“baada ya zitto kuitwa na dk. Slaa, ndipo alianza kutoa maelezo na hatimaye wajumbe wakaridhia. Na baadaye mbowe akaandika barua kwenda kwa rais kuomba kukutana naye ili kuwasilisha mapendekezo ya chama,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.

warioba ‘messanger’ mtiifu

habari zinasema baada ya mbowe kuandika barua ya kuomba kukutana na rais kikwete, jaji warioba ndiye aliyekuwa ‘wakala’ wa mawasiliano kati ya pande hizo mbili, yaani chadema na rais kikwete.
“barua ile alipewa jaji warioba naye binafsi kwa mkono wake aliifikisha ikulu moja kwa moja kwa rais jakaya kikwete, ambaye baadaye alifanya mazungumzo na kikwete pamoja na dk. Salim na kisha kukubali ombi hilo la chadema.
“warioba akarejea tena kwa viongozi wa chadema kwa ajili ya kutoa majibu kama ‘mjumbe’ na akaeleza kuwa rais hana tatizo kukutana na ujumbe wa chadema kwa sababu hili ni suala la kitaifa, si la kwake pekee,” anaeleza mtoa taarifa huyo.

waziri mkuu pinda arudi dar

kutokana na kuanza kwa mchakato huo wa ‘kimya kimya’ vyanzo vyetu vya habari kutoka bungeni vinaeleza kuwa mjadala wa sheria hiyo ulikuwa ukisogezwa mbele kwa maelezo ya waziri mkuu, mizengo pinda, ili kutoa nafasi kwa mchakato huo wa chadema, dk. Salim, jaji warioba na rais kikwete, ambao mpaka wakati huo haukuwa rasmi, ushike kasi.
Vyanzo vingine vya habari vimesema kuna wakati waziri mkuu pinda alikwenda dar es salaam kutoka dodoma kwa ajili ya mazungumzo kuhusu suala hilo na baada ya mjadala wa sheria hiyo kusogezwa mbele kujadiliwa bungeni kwa mara kadhaa, ilibidi mjadala uruhusiwe.

milango ya ikulu yafunguliwa

baada ya kazi hiyo ya ‘kimya kimya’ na baada ya bunge kujadili, kurekebisha na hatimaye kupitisha muswada huo, ujumbe wa chadema ulikaribishwa ikulu na rais jakaya kikwete kwa ajili ya mazungumzo.
Makaribisho hayo yaliwekwa bayana na ikulu kupitia kurugenzi ya mawasiliano na kuanza rasmi novemba 27, mwaka jana, na kurejewa tena siku iliyofuata, novemba 28, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuipa nafasi serikali iweze kutafakari mapendekezo ya chadema kuhusu sheria hiyo.
“katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa katiba mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa,” inaeleza taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ikulu iliyotolewa baada ya duru la kwanza la mazungumzo hayo.

kamati kuu ccm yatia neno

hata hivyo, wakati chadema wakiwa wameomba kukutana na rais jakaya kikwete kwa ajili ya mazungumzo, kamati kuu ya chama cha mapinduzi (ccm) ilikuwa inaendelea na kikao chake mjini dodoma, ambako ilimshauri rais kikwete kutanua wigo kwa kukutana na wadau wengine, ambao ni pamoja na vyama vingine vya siasa, ambavyo hata hivyo, tayari vimeonana na kuzungumza na kikwete. Vyama hivyo ni chama cha wananchi (cuf) na nccr-mageuzi.
Kwa upande mwingine, ushauri huo wa kamati kuu ya ccm ulizua mjadala mpya katika jamii, wengine wakiupinga na kuukosoa, wengine wakiuunga mkono lakini mwishowe, rais kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini, aliuzingatia.

viongozi wanne waibuka vinara

kama suala hili litafikia hatua nyingine katika hali isiyokuwa na malumbano tofauti na dalili za awali zilivyokuwa zikiashiria, basi, vinara wa kutuliza hali hiyo ni pamoja na rais kikwete binafsi ambaye aliridhia kukutana na wawakilishi wa makundi tofauti licha ya muswada kupitishwa na bunge naye mwenyewe kuutia saini kuwa sheria.
“angeweza kugoma na kutumia ubabe wa dola kulazimisha mambo, lakini hakufanya hivyo,” kinaeleza chanzo chetu cha habari na kuongeza kuwa; “shukurani za kipekee ziwaendee dk. Slaa, zitto, dk. Salim na jaji warioba, wameonyesha upeo mkubwa wa kiuongozi.”

muswada kufanyiwa marekebisho

taarifa zaidi zinabainisha kuwa mazungumzo hayo pamoja na ya vyama vingine yamezingatiwa na rais jakaya kikwete na kwa hiyo, katika mkutano ujao wa bunge unaonza wiki ijayo mjini dodoma, sheria hiyo ya mchakato wa katiba mpya nchini itafanyiwa marekebisho.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kurejesha uwezekano wa viongozi wanasiasa, wakiwamo wabunge kuweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa tume ya katiba ambao watateuliwa na rais, kinyume cha ilivyokuwa awali, wanasiasa wakizuiwa kuteuliwa wajumbe.

Marekebisho hayo yatawasilishwa na waziri wa katiba na sheria, celina kombani kabla ya mkutano huo kwisha na zipo taarifa nyingine kuwa huenda rais jakaya kikwete akakutana na wabunge wa chama cha mapinduzi au kile alichopaswa kuzungumza nao kikafikishwa kwao na waziri mkuu, mizengo pinda. Inatarajiwa kuwa wabunge hao wataelezwa hatua kwa hatua kuhusu kilichojiri kati ya mkutano wa rais kikwete na vyama vya upinzani kuhusu muswada walioupitisha ambao hatimaye naye aliutia saini kuwa sheria.


so what??
 
Kama ccm inaogopa Zito kuwa kiongozi ilikuwaje hao ccm kutumia nguvu kubwa kumwingiza kuwa kiongozi wa kamati ya mashirika ya umma.Na inakuwaje wabunge wa CCM humtumia mara kwa mara kufanikisha mambo ambayo wao wakithubutu itaonekana wanapingana na maamuzi ya chama chao.

Rejea hoja zake bungeni kuhusu suala la Jairo na pia sakata la mafuta, kwa mtu makini alijua kabisa nini kilichokua kimepangwa kati ya zito na wabunge wa ccm.Angalia support kubwa wanayompa zito,angalia wanavyomshangilia Shibuda bungeni

JK alipenda sana kukutana na CHADEMA ili maandamano yasitokee baada ya kugundua kuwa wananchi wengi walikuwa wakiunga mkono uamuzi wa wabunge wa CHADEMA. JK hakuwa na uwezo wala namna ya kuwafikia viongozi wa CHADEMA, akamtumia Zito kuweza kulifanikisha hilo. CHADEMA walikubali wazo lililoletwa kama ni wazo la Zito (wakati lilikuwa ni wazo la JK), kwa vile nao waliona kuwa ni njia nyingine ambayo ingeweza kufanikisha dhamira ya CHADEMA bila ya misuguano.
 
Kwa ufupi sana, ni dhahiri kuwa Mh. Zitto Zuberi kafanya kazi kubwa mno katika huu mchakato wote. Yatosha tu kuamini hivyo!!
 
Mijadala yote ya kukutana na JK, haina maana yoyote zaidi ya kutumikia AMANI na UTULIVU. Na sababu ni ndigo kabisa. Aliyetukosea wananchi ni JK ambaye alipitisha sheria bila ridhaa yetu, sasa tunapokwenda kumwona na kumwomba yeye alotukosea ndio itifaki au?... Ilikuwa na maana tu pale kumwona JK kabla hajaweka saini muswada lakini baada ya hapo sisi tunajidanganya wenyewe.
- Kifupi, Siasa za Bongo nimechoka nazo...Navua gloves!
 
Back
Top Bottom