Warioba, Salim, Zitto na Slaa washirikiana kufanikisha mazungumzo ya Ikulu

Mkuu Asante sana.Huyu mwandishi Godifrey Dilunga tumeshamjadili sana hapa.Ni mtu ambaye siku zote anaamini Chadema ni mbaya na haina viongozi makini.Alichokiandika ni kujaribu kuleta mgogoro kati ya Mbowe na viongozi wenzake.Si ajabu huyu mwandishi ndiye aliyeleta hii mada kwa jina bandia.Nawashauri wana Chadema puuzeni hii makala na haina jema lolote kwa chama
Very good noted!!na wanaungwa mkono na magamba KIM, FF and co!! Ignore them please!!
 
mi nampongeza zitto zaidi kwa kumlainisha dokta na kumfanya aache kuamini katika maandamano,kwa kuwa yangetuumiza sisi kuliko wao viongozi mwisho wa siku,ila slaa nae nampongeza kwa kukubali kulainika na kupunguza kile kisirani chake toka akose urais!

Mtahangaika sana kwa ID tofauti tofauti
 
hivi inakuwaje kila wakati watu wanapomsifia zito wanatamka suala la yeye kugombea urais? huu ni muda wa kazi, kukijenga chama na pia kuangalia masuala nyeti ya kitaifa sio muda wa kampeni, chama kina taratibu zake za kuwapata wagombea na sio kwa njia ya kupeana sifa kama hizi, wapo vijana wanaofanya kazi kama zito ndani ya chama lakini wapo kimya, tulifikirie hili kidogo ndugu zangu
 
Hivi kuna kuna watu wanampenda mnafiki zitto kabwe makubwa(watakuwa ni ccm na cuf hawa ili chama kife).muwekeni basi agombee urais muone kama hatapata kura hata laki tano.na mmlinganishe na slaa.watu tunajua kutofautisha kati ya kondoo na mbuzi.

kwa sababu muislam na chama chetu si cha waislam au?nini unafiki wa zitto basi kama sio uislam wake?ndugu zangu chadema tuache chuki hizi za kubagua watu kwa misingi ya kidini,ili chama chochote kipate ridhaa ya kuongeza na kura zitoshe ni lazima kipate kura za waislam na wakristo kwa mchanganyiko wake,hapo ndipo ccm wanapowashindia,wao wanao wote nyie na cuf mna kaubaguzi sana nyie!thats why mnakwama,kwa mfano hapo kinachowafanya mumchukie zitto ni uislam wake tu,hayo mengine ni sababu tu kila mtu anajua,issue ni uislam wake
 
The expected stupidity was hiding at the back door; religious marijuana. Stop smoking it is deadly. wewe ni wa kwanza kujifungua nyoka huyu UDINI katika hii thread pole. Zito hana UDINI lakini wapumbavu wachache wanamchafua!!
 
mzee hii sio bible kusema kila anatafsiri yake,kitu kiko wazi kabisa usichoelewa kipi ambacho mimi na mwingine tumekielewa,make it easy man why u wanna complicate kitu easy kama hiki,tatizo hapa ni zitto,ndio mana mmehamaki,angekua yeyote hata mabere marando au shibuda kusingekua na tatizo.

Mkuu hata ufanye nini huwezi kulazimisha kila mtu aelewe kama unavyotaka.Chadema ina utaratibu wake wa kutoa taarifa kama chama.Kamwe mtu kama Dilunga hawezi kuwa msemaji wa chama kwa makala zake za fitina.Tunamjua vizuri na ni miongoni mwa wafuasi wazuri wa magamba wanaotumia vizuri kalamu zao kumaliza upinzani.Tuko macho.
 
wanachadema wenzangu tukubali kijana wetu ni kweli amefanya kazi kunwa,lakini kama alivyosema mwenyekiti wetu kwenye msiba wa regina,kwamba hawa vijana hawakuota kama uyoga bali wamepikwa na wakapikika ndani ya chadema,tujivunie zitto na tuzikubali kazi zake na kumpa credit anapostahili,zitto ni wetu na ataendelea kuwa wetu tu.Akisifiwa zitto ndio imesifiwa chadema.tusijali.
 
kwa sababu muislam na chama chetu si cha waislam au?nini unafiki wa zitto basi kama sio uislam wake?ndugu zangu chadema tuache chuki hizi za kubagua watu kwa misingi ya kidini,ili chama chochote kipate ridhaa ya kuongeza na kura zitoshe ni lazima kipate kura za waislam na wakristo kwa mchanganyiko wake,hapo ndipo ccm wanapowashindia,wao wanao wote nyie na cuf mna kaubaguzi sana nyie!thats why mnakwama,kwa mfano hapo kinachowafanya mumchukie zitto ni uislam wake tu,hayo mengine ni sababu tu kila mtu anajua,issue ni uislam wake

Tumeshajua malengo yenu na hii makala.Ulichoandika hapa juu umejionyesha ulivyo mpumbavu
 
Najua wapo watu hii hawatapenda kuisikia zitto alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili....lakini ndio hali halisi,lazima tuiseme .

Wadau mi nadhani baadhi yetu wakati umefika sasa tubadili mitazamo yetu kuhusu ZITTO KABWE;kiukweli kijana anaonyesha ukomavu wa kisiasa kila kukicha tofauti na vijana wengi ambao wanakimbilia posho tu;zitto kumbe anafanya mambo mengi bila kupiga mayowe wala kuita wapiga picha...hili nalisema kufuatia kugundua kuwa Mh. zitto kabwe kuwa chanzo cha mazungumzo maarufu yanayoendelea ikulu kati ya chadema na Rais kikwete,mambo yako hivi.....

Safari ilianza hivi; baada ya kuona mwenendo wa mijadala na mwelekeo wa baadhi ya viongozi wenzake, hasa katika siku ambazo CHADEMA kilikuwa kinatangaza kwamba kingeitisha maandamano nchi nzima kupinga mchakato wa katiba mpya uliokuwa umewasilishwa na Serikali bungeni, baadhi ya wanaCHADEMA na wengine miongoni mwa umma, walihisi kuwako kwa hatari ya kweli ya vurugu kuibuka nchini, ambayo isingekisaidia chama hicho au kundi jingine lolote, hivyo Zitto alifunga safari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ili kuteta na Dk. Slaa.

Katika mazungumzo yao, vyanzo kadhaa vya habari vimesema, hoja ilikuwa ni umuhimu wa kuchukua njia ya mazungumzo katika suala la mchakato wa katiba mpya, kuliko njia ya maandamano. Lakini Dk. Slaa amekaririwa akiashiria kwamba ilikuwa vigumu zaidi kuanzisha njia ya mazungumzo kwake kuliko njia ya shinikizo kupitia maandamano.

Raia Mwema limeambiwa kwamba kutokana na ugumu huo, Dk. Slaa amekaririwa kumueleza Zitto kuwa wanaweza, katika kufikia kupata muda wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete, kuwatumia wazee wenye utulivu na busara, wasio na misimamo mikali ya kisiasa, wenye kutanguliza mbele maslahi ya nchi na wanaosimamia zaidi nguvu ya hoja, ambao miongoni mwao ni Dk. Salim na Jaji Warioba.

Habari zinasema, tatizo kubwa alilokuwanalo Dk. Slaa katika kuwafikia wazee hao ni kwamba hakuwa na ukaribu wa kiasi hicho nao na Raia Mwema limeelezwa kwamba katika mazingira hayo ndipo Zitto alipoahidi kuwatafuta wahusika na kuwaeleza mtazamo huo na kisha kusikiliza mawazo yao.

"Zitto alikwenda kuwaona Jaji Warioba na Dk. Salim na wakati huo, vikao vya Bunge vilikuwa vikiendelea Dodoma. Kule wale wazee walimsikiliza Zitto na kuona mapendekezo yao yana mantiki na kwa hiyo, Zitto akarudi kumweleza Dk. Slaa na baadaye wakapanga kukutana na Warioba na Salim.
"Walizungumza sana, wakafanya uchambuzi wa kina na njia bora zaidi ya kuweza kufikisha suala hilo kwa Rais Kikwete. Jaji Warioba aliombwa afanye kazi hiyo kuwa kiunganishi na taarifa zinasema baada ya kujiridhisha na hali ya mambo naye aliwasiliana na Ikulu na mchakato ukaanza.

Ndani ya Kamati Kuu CHADEMA

Habari za uhakika zinasema baada ya Dk. Slaa na Zitto kukubaliana na akina Warioba, kibarua kigumu kwao kilikuwa kuwasilisha mawazo yao mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA.
Taarifa hizo zinaelezwa kuwa Zitto hakuwa amehudhuria kikao hicho cha Kamati Kuu na hivyo, mzigo ulibaki kwa Dk. Slaa. Wakati huo, Zitto alikuwa amerejea kutoka India alikokuwa akitibiwa na hivyo hakuweza kushiriki kikao cha Kamati Kuu kwa sababu ya hali yake kiafya kutoimarika.

"Zitto aliitwa na Dk. Slaa kwenye Kamati Kuu amsaidie kueleza suala hilo, tulimwona alikuwa ametoka kuumwa alijitahidi sana kujieleza. Lakini kabla ya hapo, uchokozi wa wazo hilo uliibuliwa na Regia Mtema, ambaye alisema tukamwone Rais Kikwete ili tuzungumze naye....wajumbe karibu wote wakaguna wakimpinga na kumwona msaliti, wengine wakisema eti katumwa.

"Baada ya Zitto kuitwa na Dk. Slaa, ndipo alianza kutoa maelezo na hatimaye wajumbe wakaridhia. Na baadaye Mbowe akaandika barua kwenda kwa Rais kuomba kukutana naye ili kuwasilisha mapendekezo ya chama," kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Warioba ‘messanger' mtiifu

Habari zinasema baada ya Mbowe kuandika barua ya kuomba kukutana na Rais Kikwete, Jaji Warioba ndiye aliyekuwa ‘wakala' wa mawasiliano kati ya pande hizo mbili, yaani CHADEMA na Rais Kikwete.
"Barua ile alipewa Jaji Warioba naye binafsi kwa mkono wake aliifikisha Ikulu moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye baadaye alifanya mazungumzo na Kikwete pamoja na Dk. Salim na kisha kukubali ombi hilo la CHADEMA.
"Warioba akarejea tena kwa viongozi wa CHADEMA kwa ajili ya kutoa majibu kama ‘mjumbe' na akaeleza kuwa Rais hana tatizo kukutana na ujumbe wa CHADEMA kwa sababu hili ni suala la kitaifa, si la kwake pekee," anaeleza mtoa taarifa huyo.

Waziri Mkuu Pinda arudi Dar

Kutokana na kuanza kwa mchakato huo wa ‘kimya kimya' vyanzo vyetu vya habari kutoka bungeni vinaeleza kuwa mjadala wa sheria hiyo ulikuwa ukisogezwa mbele kwa maelezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kutoa nafasi kwa mchakato huo wa CHADEMA, Dk. Salim, Jaji Warioba na Rais Kikwete, ambao mpaka wakati huo haukuwa rasmi, ushike kasi.
Vyanzo vingine vya habari vimesema kuna wakati Waziri Mkuu Pinda alikwenda Dar es Salaam kutoka Dodoma kwa ajili ya mazungumzo kuhusu suala hilo na baada ya mjadala wa sheria hiyo kusogezwa mbele kujadiliwa bungeni kwa mara kadhaa, ilibidi mjadala uruhusiwe.

Milango ya Ikulu yafunguliwa

Baada ya kazi hiyo ya ‘kimya kimya' na baada ya Bunge kujadili, kurekebisha na hatimaye kupitisha muswada huo, ujumbe wa CHADEMA ulikaribishwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo.
Makaribisho hayo yaliwekwa bayana na Ikulu kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano na kuanza rasmi Novemba 27, mwaka jana, na kurejewa tena siku iliyofuata, Novemba 28, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo ya CHADEMA kuhusu sheria hiyo.
"Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa," inaeleza taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa baada ya duru la kwanza la mazungumzo hayo.

Kamati Kuu CCM yatia neno

Hata hivyo, wakati CHADEMA wakiwa wameomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa inaendelea na kikao chake mjini Dodoma, ambako ilimshauri Rais Kikwete kutanua wigo kwa kukutana na wadau wengine, ambao ni pamoja na vyama vingine vya siasa, ambavyo hata hivyo, tayari vimeonana na kuzungumza na Kikwete. Vyama hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.
Kwa upande mwingine, ushauri huo wa Kamati Kuu ya CCM ulizua mjadala mpya katika jamii, wengine wakiupinga na kuukosoa, wengine wakiuunga mkono lakini mwishowe, Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini, aliuzingatia.

Viongozi wanne waibuka vinara

Kama suala hili litafikia hatua nyingine katika hali isiyokuwa na malumbano tofauti na dalili za awali zilivyokuwa zikiashiria, basi, vinara wa kutuliza hali hiyo ni pamoja na Rais Kikwete binafsi ambaye aliridhia kukutana na wawakilishi wa makundi tofauti licha ya muswada kupitishwa na Bunge naye mwenyewe kuutia saini kuwa sheria.
"Angeweza kugoma na kutumia ubabe wa dola kulazimisha mambo, lakini hakufanya hivyo," kinaeleza chanzo chetu cha habari na kuongeza kuwa; "Shukurani za kipekee ziwaendee Dk. Slaa, Zitto, Dk. Salim na Jaji Warioba, wameonyesha upeo mkubwa wa kiuongozi."

Muswada kufanyiwa marekebisho

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa mazungumzo hayo pamoja na ya vyama vingine yamezingatiwa na Rais Jakaya Kikwete na kwa hiyo, katika mkutano ujao wa Bunge unaonza wiki ijayo mjini Dodoma, sheria hiyo ya mchakato wa Katiba mpya nchini itafanyiwa marekebisho.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kurejesha uwezekano wa viongozi wanasiasa, wakiwamo wabunge kuweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Katiba ambao watateuliwa na Rais, kinyume cha ilivyokuwa awali, wanasiasa wakizuiwa kuteuliwa wajumbe.

Marekebisho hayo yatawasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kabla ya mkutano huo kwisha na zipo taarifa nyingine kuwa huenda Rais Jakaya Kikwete akakutana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi au kile alichopaswa kuzungumza nao kikafikishwa kwao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Inatarajiwa kuwa wabunge hao wataelezwa hatua kwa hatua kuhusu kilichojiri kati ya mkutano wa Rais Kikwete na vyama vya upinzani kuhusu muswada walioupitisha ambao hatimaye naye aliutia saini kuwa sheria.

hapo kwenye red,Kwa nini umwone zitto tu ndio anaonekana amefanya kazi ya maana kuliko hao wengine watatu?mimi ninaona ametimiza wajibu wake kama kiongozi wa chama(CDM),wakati mwingine tuwe makini na waandishi waanaogemea upande mmoja.Hoja ya mazungumzo ni nzuri lakini naona mwandishi amevumisha na kutaka kumfanya mtu mmoja ndio kinara wa mazungumzo,hata hivyo haya mazungumzo bado yanaendelea hivyo hatujaona matunda ya maana bado.Huenda sifa hizi baadaye zikigeuka zikawa kitu kingine ikiwa maazimio ya mazungumzo hayo hayatazaa matunda yaliyotegemewa na wengi.Otherwise mwandishi ninaweza kusema unafanya kampeni fulani juu ya zitto kwa baadhi ya maneno uliyotumia ktk makala hii.
 
Nyie wafuasi wa chama cha kususa na kuandamana,ngoja niwaulize,hivi bado hamumtambui rais au sasa mnamtambua?naona mko kimya mno na mbwembwe za kumkataa rais kama zimeisha,hebu tuwekeni wazi leo angalau twende sawa..
 
hapo kwenye red,Kwa nini umwone zitto tu ndio anaonekana amefanya kazi ya maana kuliko hao wengine watatu?mimi ninaona ametimiza wajibu wake kama kiongozi wa chama(CDM),wakati mwingine tuwe makini na waandishi waanaogemea upande mmoja.Hoja ya mazungumzo ni nzuri lakini naona mwandishi amevumisha na kutaka kumfanya mtu mmoja ndio kinara wa mazungumzo,hata hivyo haya mazungumzo bado yanaendelea hivyo hatujaona matunda ya maana bado.Huenda sifa hizi baadaye zikigeuka zikawa kitu kingine ikiwa maazimio ya mazungumzo hayo hayatazaa matunda yaliyotegemewa na wengi.Otherwise mwandishi ninaweza kusema unafanya kampeni fulani juu ya zitto kwa baadhi ya maneno uliyotumia ktk makala hii.

Nina uhakika na wewe unao kwamba angekua kasifiwa slaa hata kama peke yake kusingekua na tatizo uongo?hivi kwanini hatuwi fair?
 
wadau kumbe daktari wa phd baada ya kupewa darasa na zitto ameacha kisirani,sasa anamkubali kikwete kama rais,hivyo nyie hata msipojibu kama mnamkubali ama ala haina nguvu tena;kambi yenu imepata pigo kidogo....jk alisema siku ile bungeni mimi ndio rais wenu msisikilize porojo,yametimia..

mwanahalisi, jana Jumatano 25/1/2012 ukurusa wa pili Aya ya mwisho.

Dr Slaa alinukuliwa akimueleza Rais kikwete ".....nimekuja kukuona Mheshimiwa Rais, maana watu wanasema kuwa mimi nimekukimbia. Nikukimbie kwa nini?" alisema Dr Slaa, huku wajumbe waliokuwepo wakiangua kicheko.

Naye Rais Kikwete, akijibu hoja ya Dr Slaa alisema "..... hawa akina michuzi ( akimnyooshea mpiga picha wa Ikulu, Muhidin Issa Michuzi) wanapenda kutia chumvi".

mara baada ya kauli hiyo ya Dr Slaa na majibu ya Rais Kikwete, mkutano ulianza rasmi.
 
wewe bado unafikiri jamii forum ni mali ya chadema na unadhani kila anaeingia ni chadema!!!ur very wrong mzee,ila habri ndio,watu wote makao makuu marehemu Regia angekuwepo angetusaidia hapa,watu wote cdm makao makuu sio siri wanajua part aliyoplay zitto kufanikisha vile vikao vya ilkulu mabavyo kina mbowe,mnyika,tundu lisa na wengine tunawaona wanavichekelea kwenye makochi ya ikulu,raha mustarehe,watu wamehangaika havikuja hivi hivi tu kazi imefanyika mzee,sema zitto sio mtu wa misifa na kupiga mayowe,ndio maana unaona kimya.

Acha upambe wewe...
 
Wana JF,
Ukifuatilia mtiririko wa hii mada na uchangiaji wake utagundua kuna watu tayari wako kazini kuivuruga Chadema.
Tunajiuliza kama kulikuwa na vikao vya chini chini vya mazungumzo kati ya Chadema na Ikulu kulikuwa na haja gani ya kuandikwa na gazeti kwa mfumo huo? Tena kwa malengo ya kuonyesha mwenyekiti Freeman Mbowe si lolote si chochote kwenye haya mazungumzo? Kweli inaingia akilini mazungumzo makubwa kama haya yangefanywa bila hata Katibu Mkuu Dr Wilbrod Slaa kumjulisha mwenyekiti wake hata kwa simu? Is it possible? Dr Slaa uko huku jamvini tafadhali sana jitokeze uweke wazi kila kitu ili ijulikane kama kuna wanaostahili kupata credit na kuna wasiostahili.

Nilichogundua katika ufuatiliaji wangu ni kwamba kuna watu wanataka kutumia kila hila ili Freeman Mbowe asiwe tena kiongozi wa Chadema.Fine.Lakini tumieni njia za kistaarabu.Ni nani leo hii atakataa maendeleo ya Chama cha CDM ni kutokana na uongozi uliotukuka wa Freeman Mbowe na Wilbrod Slaa? Ni nani atathubutu kusimama kidete na kusema Freeman Mbowe hastahili sifa yoyote kwa haya yanayoendelea? Ninajua fika kwamba lengo kuu la Magamba ni kumuondoa Freeman kwenye uenyekiti na kumpa mtu ambaye itakuwa ni rahisi kum-drive wanavyotaka.Lakini niseme wajumbe wa Chadema wanaofanya uchaguzi wako makini sana na kamwe hawatakubali kupeleka chama kwa mfuasi yeyote wa magamba.

Mleta mada amesahau kwamba ni wiki iliyopita tu alileta mada hapa jamvini ya kumshauri Dr Wilbrod Slaa agombee ubunge wa Arumeru Mashariki ili akachukue nafasi ya uongozi wa upinzani bungeni eti kwa madai kwamba Freeman Mbowe hawezi na imemshinda.Kwa hiyo haya yote tunayojadili hapa ni mwendelezo maalum uliopangwa wa chuki zilezile dhidi ya Freeman Mbowe na Chadema.Ninachoweza kumhakikishia mleta mada kwamba uongozi chini ya Katibu Mkuu Dr Slaa uko makini na utachuja na kutoa ushauri muafaka pale uchaguzi mkuu utakapokaribia.Tukumbuke maneno ya Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye aliposema ‘’ Wanaotumia kalamu kuchafua wengine kwa malengo ya kupata uongozi wakiingia madarakani watatumia bunduki’’.Chadema kuweni macho!!
 
Hakuna mtu aliyetaja dini hapa hoja ni unafiki wake.Naona unamuuza mtu ambaye hauziki.Wewe umeishaona watu tunawachukia wakina Prof.Safari na Arfi na wao ni waislamu?zitto ni mnafiki.na hawezi kupata kura zaidi ya laki tano.wewe msifu tu lakini ukweli ni huo.Bora hata nimsifie silinde na Lema na wenje kuliko huyo mtu wako.utampamba sana lakini umaarufu wake haupo kabisa.Mimi nimsomi sina muda wa kuangalia dini ya mtu uwe buddha,mpagani,mkatoliki,mlokole,mhindu watu tunaangalia matendo tu.zitto hamna kitu.
 
quote_icon.png
By THE WHITE ELEPHANT

Yani mboe wakati mambo yote yakiendelea nasikia alikua amelala usingizi akisubiri posho bungeni,huku dogo akipiga kazi kwa kushirikiana na wazee warioba na salim,na akafanikiwa kumuingiza king DR wa "phd"! dogo agombee tu urais,slaa atakua waziri mkuu,hakuna ubishi hapo,slaa bonge la mtendaji!.
Mtendaji wa Serikali za Mitaa, nakubalina na wewe.
Uzuri ni kwamba kipimio cha utendaji wa viongozi wetu sio FF, The White Ellephant wala mimi bali watanzania wote na pale umma unapopaza sauti kumkubali au kumkataa mtu ndio ujue hicho ni kipimo cha dhati.. sasa dada FF wewe kama umeona Dr ni wa mtendaji wa serikali za mtaa na watanzania walio wengi wanakubali utendaji wake basi wewe una tatizo.. yawezekana ukabila, udini, ukanda nk.
 
Wana JF,
Ukifuatilia mtiririko wa hii mada na uchangiaji wake utagundua kuna watu tayari wako kazini kuivuruga Chadema.
Tunajiuliza kama kulikuwa na vikao vya chini chini vya mazungumzo kati ya Chadema na Ikulu kulikuwa na haja gani ya kuandikwa na gazeti kwa mfumo huo? Tena kwa malengo ya kuonyesha mwenyekiti Freeman Mbowe si lolote si chochote kwenye haya mazungumzo? Kweli inaingia akilini mazungumzo makubwa kama haya yangefanywa bila hata Katibu Mkuu Dr Wilbrod Slaa kumjulisha mwenyekiti wake hata kwa simu? Is it possible? Dr Slaa uko huku jamvini tafadhali sana jitokeze uweke wazi kila kitu ili ijulikane kama kuna wanaostahili kupata credit na kuna wasiostahili.

Nilichogundua katika ufuatiliaji wangu ni kwamba kuna watu wanataka kutumia kila hila ili Freeman Mbowe asiwe tena kiongozi wa Chadema.Fine.Lakini tumieni njia za kistaarabu.Ni nani leo hii atakataa maendeleo ya Chama cha CDM ni kutokana na uongozi uliotukuka wa Freeman Mbowe na Wilbrod Slaa? Ni nani atathubutu kusimama kidete na kusema Freeman Mbowe hastahili sifa yoyote kwa haya yanayoendelea? Ninajua fika kwamba lengo kuu la Magamba ni kumuondoa Freeman kwenye uenyekiti na kumpa mtu ambaye itakuwa ni rahisi kum-drive wanavyotaka.Lakini niseme wajumbe wa Chadema wanaofanya uchaguzi wako makini sana na kamwe hawatakubali kupeleka chama kwa mfuasi yeyote wa magamba.

Mleta mada amesahau kwamba ni wiki iliyopita tu alileta mada hapa jamvini ya kumshauri Dr Wilbrod Slaa agombee ubunge wa Arumeru Mashariki ili akachukue nafasi ya uongozi wa upinzani bungeni eti kwa madai kwamba Freeman Mbowe hawezi na imemshinda.Kwa hiyo haya yote tunayojadili hapa ni mwendelezo maalum uliopangwa wa chuki zilezile dhidi ya Freeman Mbowe na Chadema.Ninachoweza kumhakikishia mleta mada kwamba uongozi chini ya Katibu Mkuu Dr Slaa uko makini na utachuja na kutoa ushauri muafaka pale uchaguzi mkuu utakapokaribia.Tukumbuke maneno ya Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye aliposema ‘’ Wanaotumia kalamu kuchafua wengine kwa malengo ya kupata uongozi wakiingia madarakani watatumia bunduki’’.Chadema kuweni macho!!

ni gazeti la mwanahalisi...siyo mtoa maada

unachosema kina mantiki, hakuna haja ya habari hizi kuwekwa gazetini, cha ajabu mwanahalisi lina bifu na zito, mwanahalisi ni hao wa koo za akina mbowe!
 
Back
Top Bottom