Warioba na Tambwe kama Bagenda kama Cheyo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Yale mambo ya zomeazomea yaliyowakumba makada wa CCM na UDP,Prince Bagenda na John Momose Cheyo pale katika Ukumbi wa Nkrumah-UDSM,jana yaliwakumba Makada wawili wa CCM:Jaji Joseph Sinde Warioba na Tambwe Hiza pale katika Ukumbi wa Karimjee-Dar es Salaam.Walitaka kuubeba Muswada mbovu kuliko yote Tanzania uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni uhusuo mabadiliko ya Katiba.Zomeazomea zote hizo zinahusu makongamano ya kujadili Katiba mpya ya Tanzania hasa 'Muswada wa Marekebisho ya Katiba' badala ya 'Muswada wa Baraza la Katiba' unaotakiwa.Poleni sana mliozomewa na tunawaahidi kuwa tutaendelea kuwazomea pindi mtakapoendelea kuongea pumba zenu.CCM mnaelekea mahali ambapo hamtakuwa na mtu wa kumhutubia zaidi ya 'Press Conference'.
 
wajifunze kusoma alama za nyakati na wao

Alama za nyakati kwa Warioba-sawa. Tambwe Hisa je? ni alama za nyakati au ni ana tatizo kwenye ufahamu wake kutokana na umri alionao?
 
Kwa Warioba naweza kusema ilikuwa bahati mbaya sana. Huyu mzee bado anaheshimika sana mbele ya jamii. Lakini kwa Tambwe Hiza: Huyu hamnamo, ni wa hivyo hivyo hana uwezo wa kufikiri zaidi ya hapo. Mtamuua bure. Upeo wa kuelewa ni mdogo pia ni mvivu wa kufikiri.

Yeye na makamba tofauti yao ni umri tu, na Tambwe hiza akifikisha umri wa Makamba sijui itakuwaje, pigeni picha!!
 
Kwa Warioba naweza kusema ilikuwa bahati mbaya sana. Huyu mzee bado anaheshimika sana mbele ya jamii. Lakini kwa Tambwe Hiza: Huyu hamnamo, ni wa hivyo hivyo hana uwezo wa kufikiri zaidi ya hapo. Mtamuua bure. Upeo wa kuelewa ni mdogo pia ni mvivu wa kufikiri.

Yeye na makamba tofauti yao ni umri tu, na Tambwe hiza akifikisha umri wa Makamba sijui itakuwaje, pigeni picha!!
Ila tusisahau na zile Bil 50 zetu walizochukua pale BOT na mwanvuli wa mwananchi gold.
Nikisema ccm imeshindwa kudeliver for 50yrs now katika kila nyanja ikiwemo elimu sidhani kama huyu mzee atabaki salama.
In short anaheshima mbele yako si kwa jamii. au unaongelea jamii ipi? Be specific.
 
Unajua tunaweza kuwalaumu tuu haya jamaa lakini inawezekana ni laana au wamelogwa hawa!
Mbona ni wenzetu na wanajua shida na matatizo ya katiba iliyopo!
 
Kuna vitu vya msingi ambavyo ninaweza kuvianisha hapa chini amabavyo mtu yeyote inabid avitazame kwa umakini kable hajatoa mwazo yake kuhusu hili suala la katiba!
1.Watanzania wako radhi kumdhalilisha yeyote ambaye itaonekana hataki kuwapa katiba itayowarudishia haki zao
2.Muda wa kuwateka watu kiakili unafikia ukingoni,ukipata nafasi ya kuchangia,sema kile kitakachosaidia.
3.Uchama ndani suala la katiba ni wa kuogopwa
4.Lengo la katiba sio kukiua chama cha mapinduzi,bali kurudisha mamlaka kwa umma
5.Kama hatukuamini sasa,kamwe watanzania hawatakuamini kua utaleta katiba yenye tija kwao.
6.Pamoja na kua wenye uelewa wapo wachache,lakini kwa sasa wamekata shauri kua wanashinda katika hili.
7.Ukiwa na damu ya kidhalimu,jichunge sana mdomo wako usiponze kichwa chako.
8..........................................
9........................................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom