Warioba, Lusinde `wafagilia` wazee kuenguliwa CC, Nec

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, ameunga mkono uamuzi uliofikiwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuunda Baraza la Ushauri.

Baraza hilo litawajumuisha marais wastaafu, hivyo kuhitimisha ukomo wa kuwa wajumbe wa kudumu wa Nec na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho.
Jaji Warioba alitoa wito huo wakati akiizungumza katika mahojiano na NIPASHE Jumapili mapema wiki hii.
Alisema uamuzi huo ni mzuri kwani umefika wakati wazee kujenga utamaduni wa kukaa pembeni wanapoona wamezeeka na

kuwaachia vijana washike nafasi za uongozi ndani ya chama na serikali.
Alisema wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere, kulikuwa na utaratibu wa watu kuachiana madaraka, lakini hivi sasa umetoweka.
Jaji Wariona alisema kuna watu wenye hulka ya kung’anga’nia madarakani na kuwafanya vijana kukosa nafasi za uongozi.
Alisema baada ya Nec kutoa maamuzi hayo inashangaza kuona kwamba baadhi ya watu wanatafsiri vibaya uamuzi huo, kana kwamba

viongozi hao wastaafu wa kitaifa wameondolewa kwa nguvu kutoshiriki vikao hivyo.
Jaji Warioba alisema wanachama wa CCM lazima watambue kuwa ni dhana potofu kufikiri kuwa chama kikiongozwa na idadi kubwa ya vijana kitakwenda mrama.
“Hapana, bali kitaendelea kuimarika na wala hakitatetereka kama wanavyodhani baadhi ya watu,” alisisitiza.

Kwa upande wake, mmoja wa waasisi wa CCM, Balozi Job Lusinde, amesema baraza la ushauri lililoundwa na CCM litawafanya wazee kuwa wawazi na huru katika kujadili mambo nyeti, kuliko walivyokuwa ndani ya Nec na CC.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili nyumbani kwake, Uzunguni mjini Dodoma mapema wiki hii,Balozi Lusinde alisema baraza hilo litasaidia kurejesha maadili ndani ya CCM.

Balozi Lusinde alisema uamuzi huo ni mzuri na kwamba ulistahili kupitishwa miaka kadhaa iliyopita.
“Ni kweli kuwa na wale wazee muda wote, umri umeshakwenda lakini bado akili zao zinafanya kazi sasa kuwaalika wanakuwa wajumbe kamili, kukaa kikaoni saa zote hata kama mijadala haihitaji busara zao…nadhani tumechelewa kidogo kulianzisha baraza hilo,”alisema.

Balozi Lusinde alisema kuwa mambo yanayoitikisa CCM yanaweza kusuluhishwa kwenye baraza hilo badala ya kupelekwa Nec ama CC.
Alisema kuwa baraza hilo linaweza kumuita mtu yoyote likijua kuwa mambo ya nchi hayaendi sawa jambo ambalo wasiweza kufanya katika vikao hivyo vya CCM.

Kuhusu idadi ya wajumbe, Balozi Lusinde alisema wajumbe waliopendekezwa katika baraza hilo wanatosha.
Nec katika kikao chake kilichofanyika Februari 12, mwaka huu mjini Dodoma, kilifanya marekebisho ya katiba yaliyosababisha kuwaondoa rasmi wajumbe waliowahi kuwa marais, wakaundiwa baraza la ushauri.
Viongozi walioondolewa ni Marais wastaafu wa awamu ya pili na tatu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Wengine ni aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti (Bara), John Malecela, marais wastaafu Zanzibar, Dk.Salmin Amour na Abeid Aman Karume.
Mara baada ya kupitishwa kwa uamuzi huo, baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa na maoni tofauti huku wengine wakidai kuwa uamuzi huo utakiathiri chama hicho.

Hata hivyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Jumatano wiki hii akizungumza na waandishi wa habari uamuzi ulioridhiwa na Nec alisema si mpango au mkakati wa kuwaengua makusudi wazee hao kwenye vikao hivyo. Nnauye alisema uamuzi huo ulitokana na baadhi ya wazee wenyewe wastaafu wakiongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi kuomba wapumzike.
Habari hii imeandikwa na Thobias Mwanakatwe, Dar es Salaam na Sharon Sauwa, Dodoma.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
Back
Top Bottom