Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
- So far tumesikia one side ya WArioba peke yake on this ishu, sasa tunasubiri upande mwingine najua soon atatokea wa kumjibu, lakini tumeshamsikia ila maneno yake sio final katika hii ishu ya Mwananchi Gold.
Mkuu FMES, heshima kwako.
Ni kweli kuwa tumemsikia Warioba pekee akielezea kuhusu uundwaji wa Mwananchi Gold (amefanya hivyo hadharani). Angefanya hivyo kwenye vikao vya siri na/au kwa kuomba asiandikwe ingekuwa tofauti. Ukweli unabaki kuwa yeye ndie anaejua zaidi kuhusu uanzishwaji wa Mwananchi Gold kuliko si ajabu mtu mwingine yeyote. Ninayo kila sababu ya kuamini kuwa alichokisema ni ukweli mtupu (kwa kuzingatia utu uzima wake, heshima yake, na nafasi yake katika Mwananchi Gold). Mpaka hapo atakapojitokeza mtu anaeweza kutuhakikishia kuwa anaijua zaidi Mwananchi Gold zaidi yake (na hivyo kupinga kauli ya Warioba), sina shaka na wala sidhani kama ni jambo sahihi kudhani kuna wowote katika kauli zake hizo. Naamini si rahisi mtu mwingine kuja na kupinga maneno ya Warioba kuhusiana na Mwananchi Gold.
Mkuu, Taifa hili lina watu na viongozi wengi wenye uoga wa kuthubutu (labda hii inaweza kuwa sababu ya kushindwa kwetu katika kila jambo). Serikali ilijitahidi kupingana na ukweli huu kwa kuthubutu kufanya jambo la maana sana kuanzisha mradi huu. Inaelekea uoga huo huo wa kuthubutu ndio ulioifanya serikali kurudi nyuma na kuanza kuukwepa (ikidhani ni mradi mbaya). Nadhani ni vyema mTanzania yeyote mwenye mapenzi mema na nchi hii hasa mwenye kutaka maendeleo ya kudumu na kuzuia ubadhilifu unaofanywa/unaoweza kufanywa katika kuhujumu madini yetu akaangalia upya suala la Mwananchi Gold. Si lazima iwe ni kampuni ya Warioba (kama mwekezaji tu), ila mtu yeyote mwenye uwezo, na nia ya kuikomboa nchi hii. Ni vyema tukapenda uwekezaji wa ndani kuliko wa watu wa nje. Maana wao wana kwao, nako kunahitaji kujengwa vile vile. Hivyo miradi kama hii ni vyema ikawa ya waTanzania pekee. Ni miradi nyeti kwa ustawi wa Taifa letu.