Warioba: Huu ndio ukweli kuhusu Mwananchi Gold

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Raia Mwema: Kuna maneno mengi mitaani kuhusiana na Mwananchi Gold. Umeyasikia?

Warioba: Kwa muda wa miezi kama miwili hivi nimeona kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao uvumi mwingi kunihusu, na baadhi ya mambo yamesemwa, nadhani hata kwenye magazeti yenu, mmeandika.

Raia Mwema mlipata habari huko mkaja kuniuliza, nikaona mliyoandika, na kwenye ThisDay waliandika, nadhani hao ilikuwa ni wiki iliyopita.

Kwa hiyo kuna rumours nyingi zimepita. Lakini ya sasa inayopita ni kwamba mimi nilitumia ujanja, kwa kisingizio cha Mwananchi Gold Company, nikapata milioni tano kutoka Benki Kuu nikazitumia kwa manufaa yangu.

Ngoja niweke wazi kilichotokea ili nyinyi mjue na umma ujue Mwananchi Gold Company ni kitu gani. Imekuwa ikizungumzwa kama ni kitu cha chini chini hivi.



Jaji Warioba
Mwananchi Gold Company ilitokana na uamuzi wa Serikali. Jitihada za Serikali, kwa madhumuni mazuri kabisa kwa ajili ya Taifa. Serikali iliamua kwamba iundwe kampuni ya kusafisha dhahabu katika nchi hii.

Mazungumzo yalifanywa na Serikali na watu wenye teknolojia. Serikali iliachia Benki Kuu na NDC washughulikie jambo hilo. Na sababu zinaeleweka, Benki Kuu ndiye inashughulika na dhahabu na mahali pengi, mambo ya dhahabu yanahusu Benki Kuu, NDC ndiyo chombo cha Serikali kinachoshughulikia madini.

Kwa hiyo, Serikali ikateua vyombo viwili vishughulikie kuunda hiyo kampuni. Vikafanya hivyo na Memorandum of Understanding ambayo ilikuwa kati ya Benki Kuu, NDC na kampuni inaitwa Ma-Ce ya Italia ambayo ndiyo ingetoa teknolojia.

Baada ya kusaini hiyo MoU, ndiyo wakaja hapa (kampuni ya uwakili ya Nyalali, Warioba and Mahalu (Law Associates) kutuomba tuwasaidie kuunda hiyo kampuni.

Kwa hiyo waliajiri Nyalali, Warioba and Mahalu (Law Associates) katika kuunda kampuni hiyo na kufanya matayarisho yote. La kwanza tulilofanya kwa kuwa walikuwa na haraka, wanataka mambo fulani fulani yafanywe mapema, tuliunda trust company kwa kutumia watu wetu hapa.

Mwananchi Gold Company in trust, na kwa kuunda hivyo ikawawezesha kununua..kupata kiwanja, kiwanja hicho kilipatikana Vingunguti pale, ni kiwanja kikubwa na ukubwa wake ni zaidi ya eka 30.

Kwa hiyo tulishughulikia, tuliandika Memorandum na Articles of Association, tukasajili kampuni na kufanya mambo mengine ya kisheria kama kupata vibali vya kufanya biashara ya madini, tukafanya yote pamoja na Environmental Impact Assessment. Tukasaidia katika kulipia kiwanja kile, kwa kuwa walitukuwa wametuteua sisi kuwa wanasheria wao. Benki Kuu ilitoa fedha kwa NDC inunue kile kiwanja kupitia kwetu.

Kwa hiyo mradi wote ulikuwa ni wa Serikali, sasa kwa nini Serikali ilikuwa inataka mradi huo. Kwanza huko nyuma wakati wote ilikuwa ni sera ya Serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo wadogo, na njia mojawapo iliyotumika wakati fulani ilikuwa Benki Kuu inunue dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Katika kufanya hivyo, kukatokea matatizo. Ule mradi haukuendelea. Wakajaribu njia nyingine, wakaingia mambo ya Meremeta, nayo ikawa na matatizo, sasa walipokuwa wakiunda hii (Mwananchi Gold) wakasema watumie utaratibu tofauti.

Kwamba badala ya kuiunda kama shirika la umma, iwe private company ambamo Serikali ina maslahi, na wakaamua pia kwamba mwekezaji wa nje asipate hisa nyingi asije kuwa ndiye anamiliki kampuni.

Sasa katika hilo kama Serikali haitaki kumiliki hisa nyingi, na haitaki mtu wa nje awe na nyingi, ilibidi watafutwe wengine kuingia ili katika kampuni hiyo na wakaamua hao wengine wawe wa hapa ndani.

Ziwe ni kampuni ndogo ndogo za hapa, ziingie mle, hiyo ndiyo iliyoleta kuundwa kwa kampuni ya pili inayoitwa Mwananchi Trust, hii ilikuwa mwavuli wa kampuni ndogo ndogo za hapa. Baada ya kukubaliana kwa hilo, wakakubaliana kuwa mfumo wa hisa uwe Serikali ingechukua asilimia 35, na ziligawanywa Benki Kuu ichukue 20 na NDC 15, mwekezaji wa nje angechukua 20% kwa hiyo jumla inafika 55%. Zilizobaki 45 zilikuwa ndani ya Mwananchi Trust.

Ikaundwa kampuni hiyo ili kwanza kabisa isaidie wachimbaji wadogo wadogo, iweze kuwapa utaratibu wa kuuza dhahabu yao kwa bei halali, pili kupitia hiyo waweze kuwasaidia kupitia teknolojia kwa sababu wanachimba katika mazingira magumu sana, hawana vifaa.

Kupitia mradi huu, Serikali ingeweza kuwasaidia vifaa vinavyofaa kama water pumps na nini…lakini mradi wenyewe ulikuwa mkubwa, na lengo kubwa lilikuwa dhahabu ya nchi hii inayochimbwa hapa iwe inasafishwa hapa, tusiwe tunauza dhahabu ghafi, tuuze bullion.

Ukisafisha hapa na Benki Kuu inapata nafasi ya kuinunua na kuiweka, kwa sababu hazina ya dhahabu ni fedha. Kama inapelekwa nje inasafishwa kule nje Benki Kuu haiipati. Na ingewezesha…kwa sababu sasa hivi hatujui kiasi gani cha dhahabu kinachopelekwa nje, kama Serikali ingefika mahali kama nchi nyingine zinavyofanya kwamba dhahabu yote inayochimbwa hapa inasafishwa hapa basi hakuna mtu ambaye angeweza kusafirisha dhahabu ghafi, tungeweza kujua tunatoa dhahabu kiasi gani.

Huu ulikuwa mradi mzuri, kwamba katika sera ile kwamba tusiwe tunapeleka mali ghafi tu, tupeleke processed na kwa kuwa dhahabu ni bidhaa muhimu, tungekuwa tumepiga maendeleo sana.

Basi mipango yote ilifanywa, hii wanayosema fedha tuhuma inakwenda kwamba zimetumiwa vibaya. Sisi hapa tulipewa dola za Marekani milioni 1.875 kama shirika kwa shughuli hizo.

Kati ya hizo, dola milioni 1.8 zilikuwa ni kununua kiwanja, bei ya kiwanja ilikuwa miliojni 1.5, VAT 300,000. Dola 60,000 ilikuwa ya kulipia stamp duty na dola 15,000 ilikuwa ndiyo malipo yetu kwa kazi zote hizo ambazo tulikuwa tumezifanya.

Kwenye nyaraka mtaona fedha tulizopata, tulipata mwanzo dola milioni 1.5 kwa barua kutoka BoT tukapokea ile hundi sisi tuka-deposit, baadaye wakatupa dola 375,000 nazo tukazi-deposit. Kisha kuna malipo yanakuwa reflected kwenye bank statement na pia kwenye voucher zetu, tukawalipa Nyanza Road Works kwa kiwanja kile milioni 1.5.

Kisha 60,000 zile wakasema stamp duty ilikuwa imepungua tukawapa Mwananchi 45,000 za kulipia stamp duty kwa hiyo sisi tukabakiwa na 30,000. Dola 30,000 tukatoa 15,000 kwa ajili ya malipo yetu, zilizobaki tukazirejesha Mwananchi.

Kwa hiyo fedha zote ambazo tulipewa zipo-accountable. Hakuna kitu tulichokula. Kuna nyingine ambazo fedha zilitoka na katika hizo nyaraka mtaona kuna makubaliano, kwamba Benki Kuu imeingia makubaliano na NDC ndiyo imetoa hizo fedha imewapa NDC, NDC wanunue kiwanja, NDC ndiyo wameleta hapa tufanye hiyo kazi. Kwa hiyo ninavyosema ilikuwa ni ya Serikali wakati wote.

Lakini pia kuna fedha zilitumika za kununulia mitambo. Walivyokubaliana wenyewe ilikuwa Tanzania kwa maana ya Benki Kuu na NDC watoe dola milioni 15,000 kwa mradi mzima na walikuwa wameweka vipindi vya kuja kutoa, lakini baadaye tulivyokuja kukaa maana ilikuwa mradi wote ufanywe…wanataka mtambo wa kusafisha kilo 200 za dhahabu kwa siku. Kwa siku za kazi 300 hiyo ni sawa na tani 60, ambazo ndizo Tanzania inazalisha .

Ndivyo walivyokuwa wameamua wakati ule, lakini baadaye tulivyokuja kufanya tathmini mpya, watu wakasema dhahabu inayotolewa Tanzania ni zaidi ya tani 60, kwa hiyo ikaja kwamba tuanze na mradi huu mdogo tuelekeze juhudi kwa wachimbaji wadogo wadogo kwanza baadaye ule mradi mkubwa zaidi uwe unasafisha kilo 300 kwa siku. Kwa siku za kazi 300, tungezalisha tani 90 za dhahabu iliyosafishwa.

Sasa ile ya mitambo ililipwa moja kwa moja na Benki Kuu kwa yule supplier, kwa hiyo hili la kuanza kukwepa kwamba huu ulikuwa ni mradi wa watu fulani halipo. Ni mradi wa Serikali na mimi naamini bado ni mradi mzuri. Ni kitu kizuri sana kama Tanzania ingekuwa na refinery hapa na dhahabu yote na madini mengine yanayochimbwa hapa yangesafishwa hapa hapa.

Kwa sababu ndiyo sera yetu, sasa mradi ulizunduliwa, tulifanya kazi zote kufika Desemba 2005 mradi ukazinduliwa. Tukaanza kufanya kazi, tukaanzisha na kituo cha kununua dhahabu Geita, tukawa tunanunua kwa kiwango kidogo.

Tathmini iliyokuwa imefanywa huko nyuma ilionyesha wachimbaji wadogo wadogo walikuwa wanauza dhahabu yao kwa punguzo la asilimia 85. Na tuliona kwa punguzo la aina hiyo kiwanda kingeweza kufanya kazi, lakini tulipoingia wale ambao wamezoea kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo wadogo wakapandisha, wakawa wanawapa wachimbaji wadogo punguzo la asilimia 97, wakawa wanabakiwa na asilimia 3.

Hata hiyo asilimia 3 tungeweza kufanya kazi, lakini Serikali mwaka 2006 kwa kufuatana na Sheria ya EPZ sisi tusingelipa royalty (mrahaba) kwa sababu kama tunasafisaha dhahabu ile dhahabu tunayopata ni raw material, lakini Serikali ikasema lazima tulipe royalty.

Kwa hiyo kama tunanunua kwa 97% kisha unalipa royalty ya 3% ni kwamba utapata hasara na sababu waliyotoa, sheria ya EPZ inatusamehe kwa sababu tupo kwenye EPZ lakini sheria ya madini inasema anayeuza dhahabu analipa royalty, sasa ile royalty siyo sisi wanasema tunalipa kwa niaba ya huyu mchimbaji mdogo kwamba yeye ndiye anayepaswa kuilipa.

Pamoja na hoja zetu zote kwamba kuna sheria inaturuhusu kwamba hii tusilipe kodi, ya pili mkiacha hivi hao wanaonunua huko (madalali) hamjaona royalty yoyote wanakuja kulipa kwa Serikali afadhali sisi mnaiona, hao wanaonunua huko hamuioni kwa hiyo nchi inapata hasara.

Kwa hiyo kwa kuwa huu ni mradi wa Serikali mngeweza kufuata ile sheria ya EPZ lakini kwa kuwa tumelazimika kulipa royalty, tukaanza kupata matatizo ya kibiashara. Lakini hiyo haikutukatisha tamaa, Serikali kupitia NDC ina mradi wa kuchimba dhahabu, inaitwa Matinje Gold Company iko Igunga, Tabora.

Tukafanya makubaliano na Matinje kwamba dhahabu watakayoipata badala ya kuiuza kama mali ghafi wanaileta kiwandani wanatuuzia sisi, tunaisafisha kisha ndiyo inauzwa na bado nadhani wanatuuzia ilikuwa ni njia ya kujaribu kuhakikisha dhahabu tunayochimba hapa nchini tunaisafisha.

Tumesomesha watu, tumepeleka vijana watatu Zimbabwe. Zimbabwe kuna refinery nzuri sana wakawafundishwa. Kwa wahandisi kemikali watatu tungefanya kazi. Hii kazi ingefanywa na Watanzania maana tuliamua mapema kufundisha vijana wetu.

Sasa sijui kwa sababu ya kelele za kisiasa, Serikali inajaribu kuruka mradi huu… na ni mradi wake na madhumuni yake ni mazuri sana. Wanaanza kutafuta mchawi, huu ni mradi wa Serikali wao ndio waliuanzisha wakashirikisha wengine.

Na mimi kama Mtanzania nafikiri ni vizuri sana kuanzisha mradi huu na ingekuwa ni busara kufanya kila kitu kuimarisha mradi huu. Sasa Serikali imeamrisha Benki Kuu ijitoe, na benki kuu kujitoa maana yake ni kuua mradi kwa sababu fedha nyingi zilizotumika, kweli wanahisa walitoa fedha zao ambazo zilitumika kutengeneza majengo pale, kuweka mfumo wa ulinzi, hata wengine tulioingia tulilipa, lakini Benki Kuu sasa hivi wanasema dola milioni tano.

Kwa kuwa walikuwa wametoa fedha, tuliweka security. Kwa hiyo Title ya kiwanja hiki iko Benki Kuu na kwa valuation iliyofanywa mwaka jana thamani yake kiwanja na majengo hayo ni dola milioni 5.18, mitambo iliyopo pale thamani yake ni zaidi ya dola 600,000.

Fedha nyingine ziko benki, hesabu iliyopo sasa hivi ni kati ya dola milioni 6 na 7 , hakuna ambacho kimepotea kwa sababu mali hiyo ukiorodhesha ina-appreciate…hakuna kilichopotea.

Hiyo hati iko Benki Kuu, lakini kuna rumors hapa fedha zimeibwa. Wale waliokuwa wakurugenzi kipindi chote tangu walipoanza kufanya kazi hadi sasa hawalipwi hata senti, hawapati posho ya vikao. Wanafanya kazi kwa commitment tu kwa sababu waliona ni mradi muhimu, kila kilichopo tukitumie kuimarisha mradi huu.

Sitaki kueleza mangine zaidi. nataka kuzungumzia hizi tuhuma za wizi wa fedha. Kiwanja kiko pale na ni kikubwa sana, sasa hivi kama kuna mtu anataka kuuza kiwanja akikata vidogo na kuuza ni fedha nyingi, mashine zilizopo pale ni teknolojia ya juu, kuna kinu pale ambacho kinaweza kuyeyusha dhahabu yote ya nchi hii.

Kinu kile ndiyo ni kidogo kwa sasa, lakini ni kukipanua. Maana unaweza kusikia kinu ukadhani ni kitu complicated, hapana, hili ni suala la kutumia kemikali. Unakuwa na mtungi, unatia kemikali, unatia dhahabu inasafishwa, kama kuna madini mengine yamechanganyika kama shaba na fedha inayachambua na kuyatenga.

Mimi nashangaa kwamba tunao msingi hapa lakini kwa sababu ambazo hazieleweki tunapigwa vita. Ni kama tunahubiri, tunasema ni lazima tuchukue hatua ya kuchakata mazao yetu, kisha unaweka msingi wa kufanya hivyo anakuja mtu mwingine anaubomoa.

Naunga mkono kabisa hatua ya Serikali ya kuwa na kiwanda, Zimbabwe wanacho, sisi ukiacha Afrika Kusini nadhani tungekuwa wa tatu kuwa na kinu hapa na kama tungefanikiwa tungeweza kusafisha dhahabu yote ya Tanzania na tungeongeza uwezo hata kusafisha ya kutoka Kongo (Jamhuri ya kidemokrasia-DRC).

Lakini sasa dhahabu yetu yote inakwenda Ulaya kusafishwa na inapokwenda kule hapa hata wakitoa royalty, ujue dhahabu ile unapoondoa takataka zote na kuitia kwenye baa (mche) wewe unaona ni dhahabu mle kuna madini mengine. Kwa kawaida kuna shaba, fedha na palladium wakati mwingine hata platinum.

Sasa wale wanaokwenda kusafisha kule nje, yale madini sisi hayahesabiwi kama yametoka hapa Tanzania, wanachukua. Sisi tulitaka madini yetu yote tuyapate lakini wanaharibu mradi huu kwa mambo ya kisiasa tu kisha wanaanza kutafuta wachawi….wachawi ni wao.

Raia Mwema: Mradi mzima unaonekana mzuri, kwa nini Serikali inachezea kitu kizuri kwa nchi na wananchi?

Warioba: Ninavyoona katika hili wakati wanafuatia mambo fulani fulani na hasa ya Benki Kuu, wabunge waliwahi kuzungumzia hii na ikatamkwa hata Mwananchi, nadhani Dk. (Wilbroad) Slaa au Hamad Rashid wakazungumza kwenye Bunge.

Waziri (Zakia) Meghji (aliyekuwa Waziri wa Fedha Zakia) nadhani ilikuwa 2006 au 2007, tukadhania imekwisha. Lakini sasa kwa ajili ya kusemwa hivyo ndiyo hiyo mnavyosema ya ufisadi.

Kwamba kwa kuwa imesemwa hata kama ni kitu kizuri kwa kuwa imesemwa, basi baada ya kusemwa hivyo kutokana na matatizo ya Benki Kuu ndiyo Serikali ikasema basi Benki Kuu maana nadhani ilikuwa hii Meremeta na nini….wajiondoe.

Badala ya kuchunguza waone huu ni mradi ambao ni wao waliouanzisha kwa nia nzuri na kwa manufaa ya nchi wamekimbilia wanataka kuua tu. Kwa kweli itakuwa set back kubwa sana kama Serikali inakusudia kuua mradi.

Mradi ambao wameuanza wao wenyewe, baadaye wakaja kutuomba sisi tuwasaidie sasa wanaanza kuukana.

Raia Mwema: Inaelezwa kuwa Benki Kuu haipaswi kujitumbukiza au kufanya biashara, hili lina nafasi gani hapo?

Warioba: Ndiyo! Tazama, Benki Kuu kwa mambo ya dhahabu dunia nzima huwa yanakuwa chini ya Benki Kuu, nendeni Zimbabwe si mbali sana, refinery ya Zimbabwe ni owned na Benki Kuu kwa sababu dhahabu ni fedha.

Mnaona katika dunia currency ziki lega lega hivi watu wanakimbilia dhahabu, Benki Kuu inaruhusiwa kabisa kuingia kwenye biashara ya dhahabu hata hapa nchini.

Raia Mwema: Kama hali itakuwa hivi sasa, wakazuia Benki Kuu isiendelee katika mradi huu mnafikiria kufanya nini?

Warioba: Wamekwisha kuilazimisha ijitoe. Benki Kuu imetoa taarifa hiyo kwenye bodi ya Mwananchi kwamba wanatakiwa wajitoe, bodi yao imeamua hivyo na wamejitoa. NDC haijatoka, kwa hiyo nafikiri bado ni mradi mzuri kwa Serikali.

Kwa hiyo tunasema kwa kuwa Benki Kuu inajitoa na ikijitoa itaondoa fedha zake na kuchukua fedha zake ni kuua mradi, tunasema Serikali isiue mradi, afadhali tutafute mwekezaji mwingine aje atoe hizo fedha za Benki Kuu iliyojitoa.

Tunajua ni mradi unaohitaji fedha nyingi na wasipoangalia sasa anaweza kuja kuuchukua mtu wa nje, na akichukua mtu wa nje yale manufaa yanapungua. Zimbabwe wameweza kwa nini sisi tusiweze?

Actually, Gavana wa BoT aliwahi kuulizwa kwenye Kamati ya Bunge ya Mashirika la Umma, akaeleza kuhusu kinachowafanya wanajitoa ni sababu za kibiashara, kwa sababu inaonekana hakuna faida.

Kwamba kama tunanunua dhahabu kwa punguzo la asilimia 97 kisha mrahaba ni asilimia 3 hakutakuwa na faida. Sisi tulikwisha kuona hiyo wakati tunaanza kuzungumza. Lakini tukasema tangu awali mradi wa kusafisha dhahabu ungeanzishwa lakini pangekuwapo pia na School of Jewellery (kitengo cha utengenezaji samani).

Faida kubwa kwenye dhahabu ni kwenye vito, ukitengeneza pete, bangili. Zimbabwe wanafanya hivyo kwa hiyo, sisi dhahabu yetu inachukuliwa na nchi nyingine wanatengeneza bangili na kutuletea, tungeweza kufanya hayo na kupanua ajira zaidi.

Lakini ni mradi gani unaoanza mwaka wa kwanza tu mkapata faida? Mbona wanakuja kuwasamehe wawekezaji miaka mitano kodi kwa sababu wanapata hasara. Kwa nini huu mradi wa nyumbani wenye manufaa kwa Taifa unapigwa vita?

Raia Mwema: Mchakato wa kutafuta mbia umefikia wapi?

Warioba: Kwa sasa hivi tunatafuta mbia wa nje au wa ndani. Tukimpata wa ndani itakuwa vizuri, lakini hata wa nje, tukimpata tunataka achukue hisa za Benki Kuu, pili, atupatie mkopo tulipe hilo deni la benki na kwa hiyo amana yetu tutaihamisha kwa huyo atakayetoa fedha. Tunayo rasimali za kutosha bado.

Hatuwezi kukopa wenyewe bila kuwa na hati, Benki Kuu wamejitoa na wanaendelea kushikilia hati. Kuna maoni kwamba wataifilisi kampuni, wakiifilisi itakuwa ni kwa manufaa ya nani? Huu ni mradi wa nani?

Raia Mwema: Wamesema mtafilisiwa lini? Mmepewa muda maalumu kabla ya kufilisiwa?

Warioba: Hapana.

Raia Mwema: Mwekezaji wa Italia hana uwezo wa kuongeza fedha akanunua hisa za BoT.

Warioba: Kule tulifanya makusudi kuchukua kampuni ndogo isiyo na fedha lakini yenye teknolojia nzuri. Kwa hiyo tunatafuta mwekezaji.

Raia Mwema: Nani anayepiga vita mradi? Ni Serikali au mtu mmoja mmoja ndani ya Serikali?

Warioba: Sijui. Ukiona yanayoandikwa magazetini na ukiuliza habari zinatoka wapi wanasema kwa watu wanaoaminika close to the investigation ambayo maana yake ni Serikali. Mimi nilitarajia Serikali ingezungumzia mradi huu wenye nia njema.

Raia Mwema: Kujitoa kwa BoT kisheria kuna kasoro gani? Wanaweza kuchukuliwa hatua?

Warioba: Hapana naye ni mbia. Anaweza kujitoa lakini najua wamejitoa kwa shinikizo la Serikali, lakini ambalo linanistaajabisha ni Serikali hiyo hiyo ndiyo waliyoipa mandate BoT kuanzisha mradi huu.
 
Hii ni aibu kubwa kwa serikali inayozunguka dunia nzima ikiomba misaada wakati inayo rasilimali kubwa ndani, ila kwa makusudi inaamua kuiua tu. Inawezekana Serikali imeamua kuiondoa BoT ili Kampuni ikose nguvu na kufa kutokana na shinikizo la wawekezaji katika sekta ya madini zaidi ya shinikizo la wanahabari.

Kama Mwananchi ingefanikiwa, ni dhahiri kuwa dhahabu na madini mengine yaliyomo kwenye zao hilo ingebaki ndani ya nchi, na hivyo wawekezaji wangekosa ile bakshishi wanayoipata kila waipelekapo nje kuisafisha. Hilo kwao ni upungufu wa mapato. Maana katika mkataba wao na Serikali yetu, hakuna zao jingine zaidi ya dhahabu linalohesabiwa. Hivyo hizo Platnum, Silver na mengineyo ni halali yao kwa sasa.

TUNALIWA HIVI HIVI. SIJUI TUTAAMKA LINI JAMANI?
 
Inaelekea zengwe hili lilisukwa tangu lilipoanzishwa kwa sababu kama ni ushauri wa kisheria serikali ingeweza kuupata kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali. Na Warioba na wenzake waliombwa kusaidia kuanzisha kampuni kisheria, ilikuwa, ilipotokea nafasi ya kuanzisha kampuni ndogondogo kwa ajili ya kuwa na hisa kwenye kampuni mama, wao tena wajitose huko na kushina nafasi mbili-washauri wa kisheria na wamiliki wa kampuni.
Inaelekea kuna mambo mengi yamejificha ambayo hayaelezwi kinagaubaga
 
Mwanasheria mkuu ndiye aliyeiingiza nchi kwenye mikataba ya hasara kubwa sana asingeweza kuunga mkono kuanzishwa kwa kampuni ambayo itakuwa ya manufaa kwa taifa.
 
Hii ni aibu kubwa kwa serikali inayozunguka dunia nzima ikiomba misaada wakati inayo rasilimali kubwa ndani, ila kwa makusudi inaamua kuiua tu. Inawezekana Serikali imeamua kuiondoa BoT ili Kampuni ikose nguvu na kufa kutokana na shinikizo la wawekezaji katika sekta ya madini zaidi ya shinikizo la wanahabari.

Kama Mwananchi ingefanikiwa, ni dhahiri kuwa dhahabu na madini mengine yaliyomo kwenye zao hilo ingebaki ndani ya nchi, na hivyo wawekezaji wangekosa ile bakshishi wanayoipata kila waipelekapo nje kuisafisha. Hilo kwao ni upungufu wa mapato. Maana katika mkataba wao na Serikali yetu, hakuna zao jingine zaidi ya dhahabu linalohesabiwa. Hivyo hizo Platnum, Silver na mengineyo ni halali yao kwa sasa.

TUNALIWA HIVI HIVI. SIJUI TUTAAMKA LINI JAMANI?
bot ilijitoa au ilitolewa na serikali kwa sababu si jukumu la bot kujiingiza kwenye biashara ya kusafisha dhahabu, tunapoongelea bank za nchi zingine kujiingiza kwenye biashara ya dhahabu ni kwenye kununua na kuhifadhi reserve ya taifa katika dhahabu ili kujilinda kiuchumi kutokana na flactuation exchange rates katika forex currency. na hilo warioba analijua au anafaa kulielewa hili. mtaaji wa mitaji kwa serekali ni treasury. na watoaji wa mikopo ni commercial banks na sio bot.
 
Inaelekea zengwe hili lilisukwa tangu lilipoanzishwa kwa sababu kama ni ushauri wa kisheria serikali ingeweza kuupata kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali. Na Warioba na wenzake waliombwa kusaidia kuanzisha kampuni kisheria, ilikuwa, ilipotokea nafasi ya kuanzisha kampuni ndogondogo kwa ajili ya kuwa na hisa kwenye kampuni mama, wao tena wajitose huko na kushina nafasi mbili-washauri wa kisheria na wamiliki wa kampuni.
Inaelekea kuna mambo mengi yamejificha ambayo hayaelezwi kinagaubaga

Ndugu yangu Mpita Njia, Mwananchi Gold si taasisi ya serikali. Ni kampuni iliyoanzishwa kama kampuni binafsi ambayo inamilikiwa kwa asilimia 35 na serikali. Katika mantiki hiyo, Mwanasheria Mkuu hana wajibu wowote wa kuianzisha ama kuipa ushauri wowote wa kisheria.

Warioba amesema wazi kuwa kampuni yake ilipewa kazi ya kuitengenezea Memorandum na kuisajili Brela pamoja na kuisimamia (as consultants). Sijaona mahali aliposema anamiliki Kampuni hiyo. Labda kama kuna sehemu ambayo sijaielewa vizuri (naomba unisaidie).
 
Mwanasheria mkuu ndiye aliyeiingiza nchi kwenye mikataba ya hasara kubwa sana asingeweza kuunga mkono kuanzishwa kwa kampuni ambayo itakuwa ya manufaa kwa taifa.

Jasusi,

Hiyo kampuni ya akina Warioba faida yake kwa wananchi ilikuwa ni ipi zaidi ya kuliingizia taifa hasara kubwa? Je ni wachimbaji wadogo wadogo wangapi wamefaidika?

Kweli mshauri wa kisheria unageuka shareholder na unageuka mwenyekiti wa board?

Huko nyuma mzee warioba alikuwa anasema hii ilikuwa kampuni ya serikali na CCM. Kwenye hii makala haongelei kabisa CCM.

Nina wasiwasi hizo pesa wamekula tu. Mbona hatumsikii huyo mwekezaji wa Italia akilalamika? Ni mwekezaji gani huyo serikali itajitoa na yeye asipige kelele au kuishitaki serikali mahakamani?

Nashindwa kuelewa kwanini mpaka leo Warioba abahangaika na mtu kama Mahalu?

Tatizo la Tanzania ya leo ni watu kufikiri fisadi ni yule asiye ndugu au anayetoka mbali. Mafisadi tuko nao mpaka vyumbani mwetu.

Serikali iliamua kununua kiwanja chake yenyewe kwa dola 1.5 milioni? Na ikajilipa VAT?

Management ya huo mradi ukiondoa akina Warioba ilikuwa akina nani? Hata ingelikuwa kweli, huo mradi ungelikufa tu maana viongozi walichaguana kwa kujuana kuliko uwezo.
 
Kweli mshauri wa kisheria unageuka shareholder na unageuka mwenyekiti wa board?

- Only in Tanzania, Warioba alipaswa kusema hivi huu ndio upande wa habari yangu, sasa nitoe nafasi na za wengine kuhusu Mwananchi Gold, kwa yale yanamuhusu angeomba radhi kwa wananchi kwa kujishirikisha na hili shrika la kifisadi.
 
...inawezekana ana point,lakini saga ya mwananchi gold inachanganya akili maana kila mtu anasema lake na ufisadi unaongelewa,sijui ukweli ni upi lakini all in all kusafisha dhahabu ndani ya nchi ni faida kubwa kwa Taifa....kwanini isiwepo sheria ya kusafisha dhahabu yote ndani kabla haijasafirishwa,can you imagine Tax wanayolipa wachimba dhahabu ikipelekwa nje ni kodi ya matope ambayo ukweli hatupati kitu,wasafishe ili dhahabu inapoondoka inalipiwa Tax ya kitukamili uone billions zitakazobaki ndani ya nchi....South Africa hawafanyi upuuzi huo chimba na usafishe na uki export unalipa tax based on gold bar sio michanga
 
...inawezekana ana point,lakini saga ya mwananchi gold inachanganya akili maana kila mtu anasema lake na ufisadi unaongelewa,sijui ukweli ni upi lakini all in all kusafisha dhahabu ndani ya nchi ni faida kubwa kwa Taifa....kwanini isiwepo sheria ya kusafisha dhahabu yote ndani kabla haijasafirishwa,can you imagine Tax wanayolipa wachimba dhahabu ikipelekwa nje ni kodi ya matope ambayo ukweli hatupati kitu,wasafishe ili dhahabu inapoondoka inalipiwa Tax ya kitukamili uone billions zitakazobaki ndani ya nchi....South Africa hawafanyi upuuzi huo chimba na usafishe na uki export unalipa tax based on gold bar sio michanga

Koba,

Ni kweli kuna faida malighafi ku process hapo hapo nchini kwetu, lakini hiyo kazi inatakiwa ifanywe na watu wenye uwezo na sio hao wanasiasa ambao wengi wao walishindwa kusimamia mashirika ya umma mpaka yakafa.

Warioba ana uwezo gani wa kusimamia shirika kubwa kama hilo ili lilete faida kwa wananchi?

Matokeo yake ndio maana pesa zimeliwa na hakuna dhahabu ya maana waliyonunua au kusafisha.

Wananunua ardhi kwa bei ya kutisha na eti kujenga kiwanda Dar wakati dhahabu inachimbwa kanda ya ziwa, hapo kweli kuna uchumi?
 
Ndugu yangu Mpita Njia, Mwananchi Gold si taasisi ya serikali. Ni kampuni iliyoanzishwa kama kampuni binafsi ambayo inamilikiwa kwa asilimia 35 na serikali. Katika mantiki hiyo, Mwanasheria Mkuu hana wajibu wowote wa kuianzisha ama kuipa ushauri wowote wa kisheria.

Warioba amesema wazi kuwa kampuni yake ilipewa kazi ya kuitengenezea Memorandum na kuisajili Brela pamoja na kuisimamia (as consultants). Sijaona mahali aliposema anamiliki Kampuni hiyo. Labda kama kuna sehemu ambayo sijaielewa vizuri (naomba unisaidie).

Mkuu heshima mbele naona mtu mzima anataka kutumia janja ya mengi kutaka public symphasy

Balozi wa Tanzania Italy wakati huo Profesa costa Mahalu
Shareholder wa kuandaa kampuni Warioba, Nyalali and Mahalu
Kampuni ya kuleta technologia inatoka Italy
Mwenye kesi ya kuhujumu uchumi Mahalu
Mtu mzima bora tafuta kingine huyo Mahalu keshakuingiza mkenge
 
Again mnarudi tena na habari ambazo wenyewe mnashindwa kufahamu tumetoka wapi na tunakwenda wapi..

Kifupi inaonyesha wazi kwamba akili za watu wengi humu bado ni UJAMAA na kuwa shughuli zote za biashara ni lazima ziendeshwe na serikali.. Jamani karibuni Canada mje muone jinsi serikali inavyoweza kushirikiana na wananchi wake kuunda mashirika huru na wakaya Incorporate kuendesha biashara...

Sio lazima kila kitu kile Kibepari kama America au Kujamaa kama China na Urusi..
Mwanzo wa kila kitu ni mgumu lakini malengo ya mradi mzima ndiyo yanayotazamwa hapa..Haya maswala ya wachimbaji wadogo wananufaika vipi au watanufaika vipi ni kazi ya kufikiria tu..

Badala ya dhahabu yetu kununuliwa na walanguzi tunakuwa na chombo ambacho kinanunua na kuhifadhi dhahabu hiyo mbali na ufisadi unaotumika leo hii..

Ukisoma kwa makini maelezo ya Warioba tunapoteza fedha nyingi sana kwa Umaskini jeuri..Yaani ukitazama kila alichokisema Warioba ni ushindi mtupu kinachotakiwa ni kurekebisha tu baadhi ya mambo fulani ndani ya kampuni hiyo badala ya kuiuza kwa wageni.

Haya haya yametokea NBC, ATC, IPTL, TRC, Tanesco na kwingineko ambako siku zote tulitanguliza kulaumu shirika na kufikiria kuuza miradi hiyo wakati tukifahamu wakosa ni viongozi waendeshaji.. Wasifunguliwe mashtaka au kufukuzwa kazi tunachagua kuua shirika zima kwa makosa ya binadamu..

Binafsi nalitazama swala zima la Mwananchi Gold nje ya Warioba mwenyewe na kosa kubwa linalotumika hapa ni kumtazama Warioba kama mbia jambo ambalo halikatakiwi kiuchumi, as a fact ni risk yake na wana hisa wote waliowekesha ktk mradi kama ule, lakini inapofikia serikali kuweka mkono wake kuzuia badala ya kuwawezesha wananchi hapo ndipo naposhindwa kuelewa..

Tatizo la wengi hapa mnatazama Benki kuu zote duniani zinafanya kazi vipi bila kufahamu kwamba sio kila nchi ina produce dhahabu kwa kiwango tunachozungumzia..Hata mimi mwanzo nilifikiria kuwa benki kuu inafanya mchezo lakini baada ya kusoma maelezo haya nimepata mwanga zaidi na kuunga mkono BoT kuwezesha mradi kama huu kwani BoT imekuwa ikifanya kazi nyingi za ajabu ajabu ambazo sijawahi kusikia duniani.. Leo ktk kitu kama hiki ambacho ni wazi kabisa mshindi nani niweke mashaka?..I mean guys BoT inakopesha watu fedha (sijui benki kuu gani inayohifadhi cash money) inatoa mikopo kama vile ni benki ya mtaani na hamsemi kitu, wamechota weee na wanaendelea kuchota sijasikia mtu akisema kitu leo kwa Mwananchi imekuwa Ufisadi!..

South Afrika Zimbabwe na nchi nyingi zinazoongoza duniani kwa kutoa dhahabu, benki kuu zao zimejihusisha sana na ununuzi wa dhahabu hizo ikiwa ni pamoja na usafishaji wake...Na kama nchi haina dhahabu basi benki kuu hujishughulisha zaidi ktk ununuzi toka nje..Leo sisi tumejaliwa kuwa nayo nyumbani tunaanza kuuma meno kwa gubu na kimeo..

Bila shaka hatuwezi kufaidika wote, wapo watakaokuwa wa kwanza na pengine ktk nafasi nzuri zaidi yetu ktk miradi kama hii lakini muhimu zaidi ni kutazama nini faida ya mradi mzima kwa wananchi na Taifa. Nafikiri Warioba kajieleza vizuri sana pamoja na kwamba kidogo nimeshikwa na Utata aliposema wananunua dhahabu kwa asilimia 97... hii sijui kama ni kutoka bei gani?..

Kwani asilimia 97 ya mchanga wa dhahabu haina maana baada ya kusafishwa bei na thamani ya dhahabu iliyopatikana itakuwa sawa na asilimia ile ya mchanga..Kidogo nimepata taabu kuelewa hapo lakini given the case mradi huu ni muhimu sana hasa kutokana na scandals za Barricks na mashirika mengi ya madini nchini ambayo kwa mtu anayefikiria mbali ataelewa kabisa wana mkono ndani.. Kuwepo kwa Mwananchi Gold refinery ni tishio la pato la mashirika haya huko mbeleni na pia inaweza kabisa kuwazuia wao kujipanua ktk maeleno ambayo tayari wamekwisha yapigia mahesabu..

Mtanisamehe wakuu, lakini kwa jinsi nilivyoona Utawala wa Kikwete ulivyojiingiza ktk madini, nina wasiwasi mkubwa kuwa hili ni deal against wananchi yaani Watanzania na Warioba ni bangusilo tu ktk kuliangusha shirika zima la Mwananchi Gold...

Kama alivyosema yeye Warioba ni mwajiriwa, na hii ni mali ya serikali basi kwa nini wasimwondoe Warioba na watu wengine wote wanaokisiwa wafikishwe mahakamani kujibu mashtaka lakini mradi huu uendelee kufanya kazi. Mbona tumewafikisha hao viongozi wa BoT na hatukufikia hatua ya kufunga BoT kwa sababu tunahisi kuna Ufisadi BoT..

Ningewashuari kina Idd Simba na shirika lao linalouza hisa za mashirika kupitia DSE wachukue mradi huu na kuuza kwa wananchi nina hakika kabisa kwamba fedha zinazotakiwa zitapatikana kirahisi sana pengine hao walanguzi wenyewe watachukua hisa...

What I care most is - MADE IN Tanzania, sijali kama hiyo ni mali ya Somaiya, warioba au serikali....
 
Mkandara,
Hapa umesema kile hasa nilitaka kukisema na hata kuweka bayana zaidi. Labda tu niongeze kwa kukumbuka kila alichokisema wakati ule Warioba na wakati huo nikimjibu Mtanzania. Kama sikosei alisema kuwa MRADI huu ni kusafisha madini yote ya Tanzania. Yaani dhahabu, alimasi, Tanzanite, nk. Labda kwa hilo ndilo linaleta utata. Ila nafikiri kwa madini kama dhahabu, fedha na platinium, BoT inaweza na inatakiwa kabisa kujihusisha.

Kama walifikia hadi kupeleka watu nje kwenda kusoma, nafikiri walikuwa na malengo mazuri. Ingelitakiwa tu kusomesha wengine kadhaa na kupata akina JOHHNY DENG wetu hapa hapa Tanzania na hizi BLING BLING ziwe zinatengenezwa hapa Tanzania. Nafikiri Mikufu, saa, vito nk bado milele na milele itakuwa biashara safi sana. Siku hizi unaweza hata kuwa na soko ndani ya EBAY. Wenye pesa zao kama wakiwa na uhakika wa bidhaa, basi watanunua tu. Nafikiri kwa hali ya Tanzania, tunahitaji viongozi wasio ogopa kuleta mawazo mapya ili mradi tu nchi itafaidika.

Huu mradi naona alianzisha Mkapa, alivyokuja Muungwana, wakamuambia huyo ni mchawi na sasa unauliwa. Kuna haja kweli ya kuuangalia kama MRADI na si WARIOBA. Tuanze kuupigia kelele ili huu mradi urudi hata kama kwa asilimia nyingi uwe wa Watanzania na serikali ibaki na hisa kidogo kupitia NDC. Hayo madini muhimu kwa Bank na yaende BoT, mengineyo kampuni iuze popote itakapotaka. Na kama wakitengeneza VITO, basi wapunguziwe kodi fulani kwa kuleta ajira nchini.

Tujifunze kujenga vyetu na si kukimbilia tu hizo 10% au nasikia kwa Tanzania 90%.
 
Koba,

Ni kweli kuna faida malighafi ku process hapo hapo nchini kwetu, lakini hiyo kazi inatakiwa ifanywe na watu wenye uwezo na sio hao wanasiasa ambao wengi wao walishindwa kusimamia mashirika ya umma mpaka yakafa.

Warioba ana uwezo gani wa kusimamia shirika kubwa kama hilo ili lilete faida kwa wananchi?

Matokeo yake ndio maana pesa zimeliwa na hakuna dhahabu ya maana waliyonunua au kusafisha.

Wananunua ardhi kwa bei ya kutisha na eti kujenga kiwanda Dar wakati dhahabu inachimbwa kanda ya ziwa, hapo kweli kuna uchumi?
Mtanzania,
Warioba ni wakili. Ukisoma tena maneno yake hakusema kuwa yeye alikuwa tayari kufanya kazi ya kusafisha dhahabu au anao utaalamu huo. Alichofanya ni kusaidia kufanikisha kuunda kampuni ambayo ingeshughulika kusafisha dhahabu nchini na kuisaidia nchi kupata kipato zaidi kutokana na dhahabu inayosafishwa hapo hapo nchini badala ya kupelekwa ghafi katika nchi za nje. Hakuna pesa iliyoliwa kama ninavyoelewa na mradi huo ni salvageable hata kama BOT wamejiondoa.Unapouliza Warioba ana uwezo gani wa kusimamia shirika kubwa kama hilo ili kuleta faida kwa wananchi na mimi nakuuliza ni nani aliye na uwezo huo? Kuna vigezo gani? Kama Warioba aliwahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania kweli hana uwezo wa kusimamia kashirika angalau hata kamoja tu ka kusafisha dhahabu? Come on!
 
- So far tumesikia one side ya WArioba peke yake on this ishu, sasa tunasubiri upande mwingine najua soon atatokea wa kumjibu, lakini tumeshamsikia ila maneno yake sio final katika hii ishu ya Mwananchi Gold.
 
- So far tumesikia one side ya WArioba peke yake on this ishu, sasa tunasubiri upande mwingine najua soon atatokea wa kumjibu, lakini tumeshamsikia ila maneno yake sio final katika hii ishu ya Mwananchi Gold.
Sawa FMES,
Afadhali yeye katoa upande wake siyo akina Mkapa wanaominyia tu wakidhani the issue is going away. Nothing is going away and the truth will always triumph.
 
Sawa FMES,
Afadhali yeye katoa upande wake siyo akina Mkapa wanaominyia tu wakidhani the issue is going away. Nothing is going away and the truth will always triumph.

- Hapa tupo pamoja sana, strong point.
 
Excellent piece of information! Na walioanzisha hii kampuni walikuwa na vision, bank ingekuwa na unafuu mkubwa wa kuprotect/backingup currency. But sure we need another side of the story and some simple questions:
1. For a government which owns Land buying land at USD 1.5 million and paying itself VAT USD 300,000. It doesn't tick to me.

2. BOT have reasons to backup this project; all banks in the world (especially Central Banks) are backedup by gold reserves; how can this fourth term government of CCM lack such a vision to persuade BOT to withdraw itself from the shareholding?

3. Free Processing Zone and its incentives: Hii hainiingii akilini kwa nini serikali yenyewe iliyounda hii, halafu yenyewe inajipinga kwenye hili na maslahi yake?

4. In my conclusion I find that there is a big MAFIA playing around with this country economy, I don't see the sincerity of this sitting president on this; Warioba in his side of the story makes this project a boost for Tanzania Economy; how can people in the sitting government don't focus on these advantages? Or otherwise we are cowards
 
Mtanzania,
Warioba ni wakili. Ukisoma tena maneno yake hakusema kuwa yeye alikuwa tayari kufanya kazi ya kusafisha dhahabu au anao utaalamu huo. Alichofanya ni kusaidia kufanikisha kuunda kampuni ambayo ingeshughulika kusafisha dhahabu nchini na kuisaidia nchi kupata kipato zaidi kutokana na dhahabu inayosafishwa hapo hapo nchini badala ya kupelekwa ghafi katika nchi za nje. Hakuna pesa iliyoliwa kama ninavyoelewa na mradi huo ni salvageable hata kama BOT wamejiondoa.Unapouliza Warioba ana uwezo gani wa kusimamia shirika kubwa kama hilo ili kuleta faida kwa wananchi na mimi nakuuliza ni nani aliye na uwezo huo? Kuna vigezo gani? Kama Warioba aliwahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania kweli hana uwezo wa kusimamia kashirika angalau hata kamoja tu ka kusafisha dhahabu? Come on!

Jasusi,

Kuwa waziri mkuu na kuwa mwenyekiti wa board wa kampuni kubwa kama hiyo ni vitu tofauti. Ndio maana mashirika yetu yote yamekufa shauri ya kutumia watu kama hao.

Nikiona hata anavyojitetea, inaonyesha wazi Warioba hakuwa na hana uwezo wa kusimamia kampuni kama hiyo. Ukitaka kampuni kama hiyo ipate faida lazima uwe na watendaji wanaoelewa biashara sio hao wanasiasa wanaofikiri solution ni kutumbukiza more money.

Hiyo kampuni ilikuwa doomed for failure toka siku inaanzishwa.

BTW mbona sasa Warioba haongelei kuhusu hiyo kampuni kumilikiwa na CCM?
 
Back
Top Bottom